hahahahhaa akijibu nitagiNa sisi tunao ishi huku Mbagulile mwisho wetu wapi?
Mimi nafikiri hasara za kuvaa kandambili zinaweza kua kubwa kuliko faida. Nitatoa mifano:
1. Kama huna usafiri, jiandae kung'oka kucha kwa kujikwaa, au kukanyagwa kwenye daladala.
2. Kama una usafiri, ukikamatwa unaendesha gari huku umevaa ndala ni msala 30k inakuhusu
3. Ukipanda bodaboda ni rahisi ndala kuchomoka na kudondoka kitendo ambacho kinaweza sababisha ajali. Aidha, dole gumba linaweza ingia kwenye injini ya pikipiki na kuungua
4. Kwavile ndala ni laini, tegemea kwamba ukikanyaga kitu chenye ncha kali mfano msumari ni ishu
5. Mvua ikinyesha au kama kuna matope, wewe unakua huna tofauti na mtu anaetembea peku.
6. Ni ngumu kumkimbiza mwizi aliekwapua sim yako ukiwa umevaa kandambili
7. Kuna sehemu hawaruhusu kuingia na kandambili
8. Watoto wakikurushia mpira na wewe ukaupiga, kandambili utaikuta juu ya bati
Sababu dhaifu sana hizi. Ninadhani aliyezitoa hajui kanuni za mavazi. Yani, hajui mtu uvae nini na wakati gani. Hivyo, tunaposema tunavaa ndala, haimaanishi kila mahali au wakati wote. Kama ilivyo viatu vya kudumbukiza,si wakati wote ama kila mahali vinafaa. Mvaaji anapaswa kujitambua anafanya nini na kivipi. Hata ndala tunazosema hapa siyo ndala zako za kwa Mangi, ni ndala zimeenda chuo kikuu kiasi cha kuvutia machoni. Mfano, kuna hizo zipo pale Mr. Price, Mlimani City, binafsi, ninazihusudu sana, bahati mbaya saizi kubwa sijawahi kuzibahatisha.
Lakini, ukiacha kanuni, suala la hisia ni muhimu sana katika uvaaji, hivyo sisi tunashauri tu mengi hubaki kwenye maamuzi ya mtu binafsi.
Mkuu kwani wewe unaishi wapi? Ndala hizi hizi za kwa Mangi watu wanazunguka nazo mjini kila mahali we unaongea nini? Hapa hatuongelei sandals tunaongelea ndala za bafuni!
Na mimi sijasema mtu asivae, nimejaribu tu kuonyesha hasara za kuvaa ndala mjini. Still uamuzi wa kuvaa au kutovaa ni wako
Ninaishi hapahapa tz , tena ninaishi huku kwa watanzania wa kawaida tu.Ipo hivi,mimi kusema ndala za kwa Mangi ulikuwa ni mtazamo wangu kwa maana mchokoza mada hakusema ndala zipi.Sasa tupo wale tunaovaa ndala na kutembea nazo mjini,lakini ndala zinakuwa na mvuto,hata ukiwa nazo nyumbani pia baadhi hazijakaa kibafuni.
Zingatia
Sandals ni kitu kingine, sizungumzii sandals, nazungumzia kandambili, yani, flip flops.Aidha, wewe kutaja hasara za ndala haimaanishi watu tusihoji,wewe umechangia,ni sawa na mimi nachangia kwa kukosoa ulichosema. Si lazima tukubaliane nawe hasa hata kama haupo sahihi.
Mfano,unasema eti nikiwa naendesha gari, kwani nimekwambia nitavaa ndala nikiwa naendesha? Wakati wote mtu makini katika kuvaa unajua wazi kuwa nivae nini wapi na wakati gani.
Kwahiyo mkuu hua unabeba ndala kwenye pochi ukifika mjini ndio unazivaa au vipi? Au ukiwa kwenye gari unavaa viatu then ukishuka unavaa ndala? Maana wengi naowaona mimi hua wanatoka nyumbani wamevaa ndala na wanazunguka nazo kila mahali.
Mie napenda kuvaa kandambili hususan summer time nafika nazo hadi mjini.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu HATA NG'AMBO kuna SUMMER TIME.....hukuti MTU kavaa MABUTI JUA KALI,,,,,usiwalaumu wengine pengine wewe ndy KITUKO,,,usiyoenda na SEASONS...SANDLES ni aina ya KIATU CHA MAJIRA YA JOTO..,.usimpangie MTU cha KUVAA,,mbona wewe UNAVAA KAUNDA SUIT. , unajiona upo sawa?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unapata hadi muda wa kuangalia fulani kavaa hivi usawa huu wa Anko Gangachuma?
hahahahhaa akijibu nitagi
Mkuu kwani wewe unaishi wapi? Ndala hizi hizi za kwa Mangi watu wanazunguka nazo mjini kila mahali we unaongea nini? Hapa hatuongelei sandals tunaongelea ndala za bafuni!
Na mimi sijasema mtu asivae, nimejaribu tu kuonyesha hasara za kuvaa ndala mjini. Still uamuzi wa kuvaa au kutovaa ni wako
Ninaishi hapahapa tz , tena ninaishi huku kwa watanzania wa kawaida tu.Ipo hivi,mimi kusema ndala za kwa Mangi ulikuwa ni mtazamo wangu kwa maana mchokoza mada hakusema ndala zipi.Sasa tupo wale tunaovaa ndala na kutembea nazo mjini,lakini ndala zinakuwa na mvuto,hata ukiwa nazo nyumbani pia baadhi hazijakaa kibafuni.
Zingatia
Sandals ni kitu kingine, sizungumzii sandals, nazungumzia kandambili, yani, flip flops.Aidha, wewe kutaja hasara za ndala haimaanishi watu tusihoji,wewe umechangia,ni sawa na mimi nachangia kwa kukosoa ulichosema. Si lazima tukubaliane nawe hasa hata kama haupo sahihi.
Mfano,unasema eti nikiwa naendesha gari, kwani nimekwambia nitavaa ndala nikiwa naendesha? Wakati wote mtu makini katika kuvaa unajua wazi kuwa nivae nini wapi na wakati gani.
Kwahiyo mkuu hua unabeba ndala kwenye pochi ukifika mjini ndio unazivaa au vipi? Au ukiwa kwenye gari unavaa viatu then ukishuka unavaa ndala? Maana wengi naowaona mimi hua wanatoka nyumbani wamevaa ndala na wanazunguka nazo kila mahali.
Kama kweli umemaliza darasa la saba, sentensi hii kutoka post yangu ya mwisho ilipaswa kumaliza mjadala huu:
"Wakati wote mtu makini katika kuvaa unajua wazi kuwa nivae nini wapi na wakati gani"
Sasa hapo kwa muelewa sitegemei tena uulize naweka kwenye pochi,kwenye bonet, tairi au la. Baadhi yetu hata safari za mbali kama hatuendeshi tunavaa ndala.Wewe unatoka dar mpaka Bukoba au Kigoma, unalala njiani, upo kwenye basi na kiatu cha kudumbukiza, kha! Kwani wewe mwanajeshi?