Ni sahihi kuvaa kandambili au kobazi kwenye public?

Wengine tuna fungus baba... Tukivaa viatu miguu inawasha sana aisee....
Hapo hiyo ni special case unaweza kueleweka. Lakini ukienda mjini angalia viwanda mbili vinavyo rusha vumbi hadi inakera.
 
Ebu vuta picha mdada mwenye chura halafu mweupe pee chini kavalia mini skirt nyeusi, viatu vyeusi na soksi ndefu kama vya wanafunzi au askari wa kike au raba na soksi na mdada mwingine chini kavalia vindala simple

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tone yako ipo rude, unadhani unajua kumbe hujui. Kuna uwezekano wa mambo mawili kuhusu tone yako:

1.Huna maarifa ya tafakuri tunduizi(Critical thinking skills)

2.Ni mjinga tu usiejua mambo


Ipo hivi, pamoja na kwamba utamaduni hutawala sana mambo mengi tufanyayo, hali hii isikutie ujinga na kufikiri kile unachofanya au ulichofunzwa tangu utoto ni sahihi kwa kila mtu. Yaweza kitu hiki kikawa sahihi au si sahihi kwako, lakini si kwa kila mtu.Kwahiyo, pamoja na kwamba utachukia, wakati wote ujifunze kukubali mawazo mbadala. Kuna baadhi ya vitu tunaweza kukubaliana bila shida, mathalani, kuzama na kuibuka kwa jua, kwani suala kama hili mnaweza kuthibitisha kisayansi.

Kuna baadhi ya mambo ni suala la mtazamo tu, mfano, uzuri na ubaya.Na hapa ndipo hoja yako inaingia.Uvaaji wa Kandambili au vazi lolote ni suala utamaduni na mitazamo tu, chochote kinawezekana.

Zingatia

Suala hapa si faida au hasara ya kuvaa kama baadhi wanavyotoka kwenye mjadala, suala ni uvaaji tu. Hayo ya faida ama hasara ni mada nyingine kwani hata vya kudumbukiza vina faida na hasara.Baada ya kusema haya ninakutaarifu mtoa mada na uma mzima unaoshiriki uzi huu kuwa kandambili(flip-flops) huweza kuvaliwa zaidi ya bafuni. Hata hivyo, wataalamu wa styles wameshauri wapi unaweza kuvaa na wapi hapana.Pia, unapozivaa ni mavazi gani huendana nayo.

Ndala zaweza valiwa kwenye mitoko nje ya ofisi(ile isiyo rasmi), mfano kukutana na rafiki zako pale mkitazama mpira mwisho wa wiki, ufukweni n.k

Wanashauri usivae ndala ofisini(ofisi nyingi haziruhusu,japo usishangae wengine wakaruhusu, rejea suala mtazamo hapo juu), pia usivae ndala kwenye mikutano hasa iliyo rasmi , sherehe rasmi n.k

Kuhusu kuvaa na nini, inapendekezwa(hasa kwa wanaume) ndala zivaliwe kwa suruali ya jeans ama kaptula.

Hivyo, kikubwa hapa ni kujua kuwa uvaaji hutawaliwa na mitazamo, fasheni na utamaduni. Wewe umefunzwa hivi, mimi nimefunzwa vile, wewe unapenda hiki,mimi ninapenda kile, fasheni inataka hivi, wewe unasema hapana, nitabaki hivi.Pande zote,hakuna atakaekufa kwa kusimamia anachoamini hapo. Hiyo ni tofauti na sumu ya panya,ambayo ukiibugia kiasi cha kukuondoa jibu ni moja tu, ukipona basi watu tutajiuliza na kutafuta sababu iwe ya kiroho ama maabara ya kisayansi.Ili kujifunza zaidi kuhusu uvaaaji ndala rejea kiunganishi hiki hapa chini:

Are You Breaking the Rules of Flip-Flop Etiquette? Find out Here.

Ninawasilisha
 
Kwanini watu wanazurura wamevaa kandambili?! Mjini katikati mtu kavaa kandambili!

Unakuta miguu ina vumbi kupitiliza. Kwanini watu hawa wasivae viatu vinavyofunika miguu yao?!

Hizi kandambili za kuvaa huko bafuni kwenye mabafu yetu lakini kuna watu wamefanya ni kama viatu rasmi. Unakuta mtu kucha hadi zimefanana na ardhi, kwanini hawapendi kuvaa viatu?!

Kinadada wana vijikandambili wao huita simple,! Hata sielewi huu ni utamaduni au umasikini au kutokuelewa?!
Madhara ya kupata pesa baada ya kumaliza chuo, utajaribu kuuliza hata kwanini watu wanafua chupi bafuni
 
Madhara ya kupata pesa baada ya kumaliza chuo, utajaribu kuuliza hata kwanini watu wanafua chupi bafuni
Hahaha sasa ukizipata mdogo hufui kabisa nini? yani umeshazizoea au ulitaka kumaanisha nini?
 
Kandambili kwetu mwisho ni chooni ni utamaduni tu sasa kwa wengine inaweza kuwa sawa

Hii ni sawa na ile mtu kupiga mswaki huku anaongea na watu dah inakera

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani umepiga penyewe kabisa, watu wako humu wanataka iwe kawaida. Kuna jamaa chuo alikuwa anatoka Hall moja anaenda jingine anapiga mswaki, halafu akianza kujikwangua ulimi utadhani anataka kufa au mbuzi kabanwa. Yani watu wote wanacheka jamaa alivyo komaa na tabia hiyo utadhani aliisomea,hakutaka kuiacha mpaka alipo pata kabinti flani hivi.
 
We jamaa acha kutufuatilia, kabla hivyo viatu vya kufunika havijaja hizo kandambili (malapa) zilikuwa zinavaliwa na wenye nazo. Kisa viraba vimekuja ndo mtuletee dharau? Fanyeni yenu bhana. Me hata peku peku natembea
 
We jamaa acha kutufuatilia, kabla hivyo viatu vya kufunika havijaja hizo kandambili (malapa) zilikuwa zinavaliwa na wenye nazo. Kisa viraba vimekuja ndo mtuletee dharau? Fanyeni yenu bhana. Me hata peku peku natembea
Hahaha bora upekue, kuliko kandambili. Ukipekua hutimui vumbi na wala hurushi tope.
 
Mkuu HATA NG'AMBO kuna SUMMER TIME.....hukuti MTU kavaa MABUTI JUA KALI,,,,,usiwalaumu wengine pengine wewe ndy KITUKO,,,usiyoenda na SEASONS...SANDLES ni aina ya KIATU CHA MAJIRA YA JOTO..,.usimpangie MTU cha KUVAA,,mbona wewe UNAVAA KAUNDA SUIT. , unajiona upo sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nafikiri hasara za kuvaa kandambili zinaweza kua kubwa kuliko faida. Nitatoa mifano:

1. Kama huna usafiri, jiandae kung'oka kucha kwa kujikwaa, au kukanyagwa kwenye daladala.
2. Kama una usafiri, ukikamatwa unaendesha gari huku umevaa ndala ni msala 30k inakuhusu
3. Ukipanda bodaboda ni rahisi ndala kuchomoka na kudondoka kitendo ambacho kinaweza sababisha ajali. Aidha, dole gumba linaweza ingia kwenye injini ya pikipiki na kuungua
4. Kwavile ndala ni laini, tegemea kwamba ukikanyaga kitu chenye ncha kali mfano msumari ni ishu
5. Mvua ikinyesha au kama kuna matope, wewe unakua huna tofauti na mtu anaetembea peku.
6. Ni ngumu kumkimbiza mwizi aliekwapua sim yako ukiwa umevaa kandambili
7. Kuna sehemu hawaruhusu kuingia na kandambili
8. Watoto wakikurushia mpira na wewe ukaupiga, kandambili utaikuta juu ya bati
 
Back
Top Bottom