Je, ni sahihi kuweka maji badala ya coolant kwenye gari yako?

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
618
Habari za masiku wakuu bila shaka mko salama, hakika kwanza nakiri kupotea hasa kwa wale waliokuwa wanafaidika na makala zangu kuhusiana na elimu ya magari, Mambo yalikuwa mengi na changamoto za maisha lakini kikubwa ni uzima na tupo pamoja tutaendelea kupeana elimu pale unapopatikana wasaa.

Leo ningependa kuongelea kitu ambacho wengi tunafanya kwa mazoea ambacho ni kuweka maji kwenye rejeta za magari yetu, Hakika wengi tulipata kuambiwa athari za kuweka maji badala ya coolant lakini labda kwa kupuuzia, kwa mazoea ama kwa kuepuka gharama ya kununua coolant tukawa tunaendelea na kuweka maji kwenye rejeta.

JE NAWEZA KUWEKA MAJI KWENYE TANKI LA COOLANT?
Hakika ni ukweli kwamba vyote maji na coolant hufanya kazi moja ya kupoza injini ya gari lako kwa maana ya kupoza mashine pindi inapokuwa ya moto au kurekebisha kiwango cha joto kuwa sawa endapo ni kwenye mazingira ya baridi hilo lazima tukubali na ndiyo maana bado watu hutumia lakini swali linakuja je ni sahihi kutumia maji badala ya Coolant?

FAIDA ZA COOLANT AU UMUHIMU WAKE
Kuna mtu anaweza mpaka sasa akawa anajiuliza kama nimekubali hapo juu kwamba vyote maji na coolant hufanya kazi moja kwanini naandika haya? Kwanza yapaswa tukubali kuwa gari yako kwenye mfumo wa kupooza injini imeshauriwa kutumia coolant badala ya maji kwa sababu kama maji yangekuwa yanakidhi basi kusingevumbuliwa coolant unajua kwanini?

Kwenye mazingira ya baridi hasa kwa nchi za baridi au baadhi ya maeneo katika nchi yetu kama vile Makete ambapo muda mwingine hadi barafu zinashuka maji kwenye injini huwa yanaganda kama ambavyo yanavoganda kwenye Jokofu na hii ni asili ya maji kutokana na mazingira lakini coolant huwa haigandi na hii hutokana na viambata ambavyo vipo kwenye coolant.

Lakini pia katika mazingira ambayo gari inakumbana na joto kali sana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za gari lenyewe kama vile kutokuzungusha kwa feni basi maji huwa yanachemka kabisa na kutokota hii tunakumbana nayo sana madereva lakini kwa upande wa coolant huwa haiwi hivo na hii pia inatokana na viambata kwa maana ya kwamba coolant itashika moto tu lakini si kuchemka na kuanza ku evaporate.

Darasa tunalolipata hapa ni kwamba coolant imetengenezwa kubaki kwenye umbile lake la kimiminika katika hali yoyote ile iwe ya Joto jingi au ya baridi kali haita athirika tofauti na unapoweka maji.

Faida nyingine ya kutumia Coolant badala ya maji ambayo watu wengi wanaijua hii ni jinsi coolant ilivoundwa na viambata ambavyo haviharibu baadhi ya vifaa au sehemu za injini za ndani au za rejeta yenyewe.

Sote twajua penye maji hapakosi kutu lakini pia kuna aina mbalimbali za maji ambayo ya na kiwango cha chumvi au kiwango cha magadi ambayo yanakuwa na athari katika sehemu za ndani za injini ya gari yako au rejeta na ndiyo maana kuna kesi nyingi sana za rejeta kuziba na kupelekwa kuisafisha asilimia kubwa ya kesi hizo ni kutokana na kutumia maji badala ya coolant.
 
Back
Top Bottom