Aug 12, 2021
64
117
Jamii ya Sasa ina uelewa mkubwa Sana tofauti na jamii iliyowahi kuongozwa na kina Nyerere, Mkapa, Mwinyi na Kikwete. Huwa nasema kuwa Viongozi wetu wasipoijua jamii wanayoiongoza watapatwa na taabu na kudharaulika kila Siku.

Kwa Tanzania Sasa hivi haishangazi kukuta Graduate anaendesha Bodaboda au yupo Shoe Shine au anauza Juice huko mtaani. Tafsiri yake ni kuwa Wasomi ni wengi Sana mtaani hivyo hata wanaowaongoza aidha wawe na maarifa zaidi yao au wajifunze kuji position kutokana na mazingira.

Mwaka 2018 Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres alisema kuwa hakuna Mtu anayezaliwa akiwa GAIDI Bali Kuna sababu zinazomfanya Mtu kuwa GAIDI baada ya kuzaliwa. Guterres alitaja sababu hizo zikiwemo migogoro ya muda mrefu isiyotatuliwa, kutokuwepo utawala wa sheria na sababu za kijamii na kiuchumi zinazotenga baadhi ya makundi, nk.

Sababu hizo zinaweza kuwa chachu ya kubadili machungu na mitazamo ya watu kuwa ya uharibifu kama ugaidi lakini si kitu cha kuzaliwa nacho. António Guterres aliyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa 16 wa bodi ya washauri wa kituo cha Umoja wa Mataifa cha kupambana na ugaidi mjini Riyadh, Saudi Arabia.

Swali la Kujiuliza hapa ni hili:-

Je, Hamza alizaliwa akiwa GAIDI au aliathiriwa na Sababu mbalimbali?

Je, Tanzania Kuna Sababu hizi ambazo zinaweza kumbadili Mtu kutoka kuwa Raia Mwema na kugeuka kuwa GAIDI? Kama Sababu hizi zipo hatuoni kuwa tupo Hatarini Sana?

Sijaona umuhimu wa hii Press ya leo. Nadhani ingetosha kusema Hamza alikuwa Kichaa. Uchunguzi huu unaacha Ombwe kubwa ambalo lilipaswa kufungwa ili kuondoa maswali mengine na kuongeza mjadala.

Swali la pili ninalojiuliza Hamza alikuwa akimiliki Silaha Je Hatukugundua kuwa ni Gaidi Hadi tukammilikisha Silaha? Ni wangapi ambao wanamiliki silaha Kwa Sasa ambao wanaweza kuwa Magaidi nchini? Taarifa zetu za ki intelligensia zipo accurate kiasi Gani?
 
POLISI jamani
Aliyepiga RisasiTundu Lissu bado kitendawili
Aliyemteka MO bado kitendawili
Aliyepiga Risasi AKWILINA bado Kitendawili
Limeibuka la HAMZA
 
Gaidi Hamza alimilikishwa silaha na serikali ya CCM.
Gaidi Hamza alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya.
Gaidi Hamza alijenga ofisi ya tawi la CCM.
Gaidi Hamza aliwapigia kampeni na kuwapa pesa wagombea mbalimbali wa CCM.
Gaidi Hamza aliahidi kuwajengea wananchi shule.

CCM imefadhiliwa na gaidi. Katibu mkuu wa CCM anapaswa kuhojiwa. Baas
 
Mkuu graduate kuwa shoe shine au kuwa boda boda sio tafsiri ya wasomi ni wengi mtaani bali ajira hakuna.

Alamsiki
 
Mkuu graduate kuwa shoe shine au kuwa boda boda sio tafsiri ya wasomi ni wengi mtaani bali ajira hakuna.

Alamsiki
Fafanua...

Kwani mnatofautiana wapi na mleta mada?

Hujamwelewa wapi mleta mada?

Na kuwa Bodaboda au shoe shine kuna ubaya gani? Hiyo siyo ajira/kazi kwani? Nini maana na tafsiri ya "kazi?"
 
Gaidi Hamza alimilikishwa silaha na serikali ya CCM.
Gaidi Hamza alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya.
Gaidi Hamza alijenga ofisi ya tawi la CCM.
Gaidi Hamza aliwapigia kampeni na kuwapa pesa wagombea mbalimbali wa CCM.
Gaidi Hamza aliahidi kuwajengea wananchi shule.

CCM imefadhiliwa na gaidi. Katibu mkuu wa CCM anapaswa kuhojiwa. Baas
Hii ripoti si wangeipotezea tu kama ile ripoti ya Lisu wangetueleza kuwa bado wanachunguza na Watanzania wala tusingehangaika nao.
 
Back
Top Bottom