Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

hivi teofil makunga nae amefikia kujidhalilisha namna hii.
au anataka ukuu wa wilaya,naombeni namba yake nina maswali akishindwa kuyajibu nitapiga kampeni wazalendo walisusie gazeti la mwananchi.
 
jana niliweka post mbili nikionyesha upeo duni wa ripoti kuanzia hadidu za rejea zisizo na focus, kuripoti badala ya kuchunguza, wahusika wakuu kutohojiwa, mapendekezo dhaifu na mengine.

Hakuna post hata moja kati ya nilizotuma imetoka hapa JF!

jf ya sasa ukitaka post yako idumu, deal na mambo ya "kuipamba" serikali
Hata hii aliyoileta mkuu mwana kijiji sidhani kama itahimili upeo duni wa mo**0„6s.
Tafadhali nsije nkapigwa ban. Ni mawazo tu.
 
Na bado, kinachofuatia ni kila atakaetaka kuzungumza ataambiwa "unaingilia uhuru wa mahakama, kaa chini."

Hapa analindwa Kamuhanda pia, unakumbuka alivyosema kuhusu tarehe yake ya kustaafu imekaribia! Hakutaka kuwakera wakubwa kwa kutotii amri zao.
 
Yule police alitumwa kuua na huo ni mpango maalum wa magamba unategemea hiyo kamati ingekuja na jipya? Vua gamba, vaa gwanda could be the only solution..!
 
Mzee Mwanakijiji

Umemnukuu Mwalimu "mtu mwenye akili akijua kuwa na wewe una akili akakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau"

"Mtu mwenye akili akijua na wewe una akili ahalafu akakuandikia jambo la kijinga na wewe ukalikubali atakudharau!"



Kwa mtazamo wako unadhani:
1. Serikali ya CCM inatuona au inajua watanzania tuna akili??
2. Waandishi wa ripoti hii wana akili??

Kama majibu (1 na 2 ) yatapishana basi nukuu yako si sahihi katika muktadha huu...
 
kuanzia jana, nimeamini tanzania ni nchi ya ajabu na kijinga. Ihema kaleta ripoti ya kijinga. Ihema=mjinga, hajaelimika.
 
jf ya sasa ukitaka post yako idumu, deal na mambo ya "kuipamba" serikali
Hata hii aliyoileta mkuu mwana kijiji sidhani kama itahimili upeo duni wa mo**0„6s.
Tafadhali nsije nkapigwa ban. Ni mawazo tu.

Uwongo dhahiri hapa ukitaka post idumu kuwa pro chadema hakuna lazaidi; hii haiwezi kudumu mdau anasema ripoti ni ya kijinga lakini haonyeshi ujinga wenyewe, kwa mantiki itakuwa ni ujinga kujadili ujinga
 
Msingi wa haya yote ni dharau dhidi ya wananchi (contempt of the people). Watawala wanaamini wanaweza kusema lolote, vyovyote, kwa yeyote bila kujali matokeo yake. Hawataki kuulizwa na wakiulizwa wanaona unaleta vurugu.

nakubaliana na wewe Mzee Mwanakijiji kuwa hii ni dharau ya hali ya juu, na sio mara moja hawa jamaa na tume zao wanafanya hivi. Nadhani muda si mrefu watu watachoka na hii dharau na watafanya mambo ya ajabu.
 
Last edited by a moderator:
Mambo mengine yanayofanyika katika nchi hii ni ya kusikitisha sana, nautilia shaka sana uwezo wa kufikiri wa Watanzania, ripoti ya kijinga namna ile huwezi kuileta kwa watu mpaka uwe una uhakika kwamba uwezo wao wa kufikiri ni duni sana, nawapeni pole sana Watanzania, poleni sana ndugu zangu Watanzania.

Stunted brains; hii ripoti ilipaswa iibue outrage ya kutisha itakayomfanya kikwete asikae ikulu! Wanatuona sisi malofa!
 
Nchi inaongozwa kisanii! sharobaro dhaifu ni msanii sana! Ripoti ya kamati ya nchimbi chini ya jaji dhaifu Steven Ihema na wapambe wao akina makunga ulitegemea nini?

RPC kamuhanda ndio alitoa amri ya kuuawa kwa Daudi Mwangosi.

My take. Wafuatao wawajibishwe mara moja.
1.IGP said mwema
2.Paul Chagonja
3.RPC michael Kamuhanda
4.Askari wote waliomzunguka marehemu excluding OSS mwampamba
 
Mwanakijiji tulijua kuwa hii tume a.k.a kamati itatetea upuuzi na unyama ulioufanywa na polisi. Hatukutegemea kitu tofauti ndiyo maana tulilalamika sana kuwa wapoteza pesa za walipa kodi bure kwa vile ushahidi wote wa nini kilitokea tulishawekewa hapa jamvini. Isitoshe kwenye kesi za mauaji tume huwa zinaundwa?? Hii ilikuwa changa la macho kutudanganya wa tanganyika. Ila damu ya mtu haipote bure na wote waliohusika na kifo cha ndugu yetu wamejiletea laana wao na ndugu zao. Mungu amesema ataleta laana hadi kizazi cha tatu na cha nne kwa wamchukizao-Kumbukumbu ya Torati 5:9-10. Kifo cha mwangosi hakika kimemchukiza Mungu.Tutasugua magoti hadi Mungu wetu atashughulika nao tu. Huu udhalimu lazima ukome. Maskini mke wa marehemu wamempa ujane bure na watoto sasa wamekuwa yatima. Hata kama watasomeshwa haitoshi kulinganisha na baba waliompoteza.
Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akijua kuwa na wewe una akili akakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau". Hili ni kweli pia kwenye suala hili. Mtu mwenye akili akijua na wewe una akili ahalafu akakuandikia jambo la kijinga na wewe ukalikubali atakudharau!

Hii ripoti ni ushahidi wa kile ambacho wengine tunaamini ni kweli; CCM na serikali yake ni lazima waondolewe madarakani sooner kwa sababu wanatudharau! Ni dharau ya ajabu sana hii. Fikiria mtu anaandika hivi kwenye ripoti:

Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?


Hili swali ni la msingi sana katika tukio zima.

Lakini Kamati imeshindwa kujibu swali ambalo kwa walioona iile video ya mauaji wanalikumbuka sana yaani linalohusiana na kukatazwa kufanyika kwa mikutano ya ndani ya chama. Kamati inatuambia kuwa barua ya zuio hilo inasema hivi:


Kumbe zuio lilihusu "mikutano na maandamano". Kwamba inaweza kujengwa hoja ya kuwa "mikutano" ilimaanisha "mikutano yote" ni vigumu kutetea hasa kwa vile wakati huo huo mikutano mingine ya kisiasa ilikuwa ikifanyika sehemu mbalimbali nchini bila kuzuiwa. Kamati ili kuonesha ulinganifu ingejaribu kutafuta maelezo ya Polisi Zanzibar kwanini waliruhusu CCM kufanya mkutano wake kule wakati kuna zuio. Lakini vile vile ni vigumu kusema kuwa mikutano yote ya kisiasa ya ndani haikuwa imeruhusiwa! Ni vyama vingapi ambavyo vilikuwa na mikutano ya ndani ya kamati zake mbalimbali kati ya August 26-Septemba 8?

Kamati ingeweza ili kulinganisha "utii wa sheria" kwa vyama vingine kuelezea kuwa vyama vingine havikufanya mikutano yoyote kati ya tarehe hizo na ni CHADEMA tu ambao walikuwa na mkutano Iringa. Hoja kuwa CDM hawakuwa watii ingekuwa na nguvu! Nje ya hapo ni kutuandikia ujinga.

Lakini kuthibitisha upuuzi wa kamati hii imeshindwa kuelezea kuwa kwanini katazo hilo liwe halali Iringa lakini Zanzibar lisiwe halali wakati CCM walipofanya uzinduzi wa kampeni yao ya Bububu? Hiki ndio kipimo cha upuuzi wa ripoti hii. Kama amri ambazo zilitolewa zilihusu vyama vyote kwanini Zanzibar waliendelea na mikutano ya kisiasa? Au wao hawakutakiwa kutiia sheria hiyo au kwa vile hakukutokea machafuko yoyote (na hayajawahi kutokea yakisababishwa na polisi!) huko Zanzibar?

Ikumbukwe kuwa uhalali wote wa polisi kutumia nguvu kuwatanya CHADEMA pale Nyololo unatokana na ukweli kuwa mkutano ule ulikuwa haramu. Lakini kama mkutano ulikuwa halali (kwa maana ya mkutano wa ndani ambao haukukatazwa) uhalali wa kutumia polisi unatoka wapi?

Ili kuthibitisha kuwa ilikuwa ni ripoti ya kijinga ni kuwa Kamati haikuwahoji wale polisi waliokuwa wamemzunguka Mwangosi na haijamhoji yule mtuhumiwa ili aelezee ilikuwaje yeye na wenzake wamshambulie Mwangosi na kwanini atumie nguvu zaidi. Inashangaza tu kuwa ripoti inataka wachukuliwe hatua za kisheria. Na kamati inaonekana haikuchukua muda kuangalia ile video au hata kuitisha watu waliokuwepo kuwapatia picha za video za tukio hilo zima. Na cha kushangaza Kamati hii iliyofanya mambo mengi ya uchunguzi imeshindwa kutoa jibu au hata dokezo la vilikopotelea vifaa vya kazi vya Mwangosi (kamera na laptop)!!

Lakini vile vile ripoti hii ambayo nina uhakika imetumia fedha ya kutosha tu (sijui nani atauliza Bungeni tuambiwe) imeshindwa kumhoji au hata kutuambia maoni ya shahidi muhimu sana katika sakata hili. Ripoti inatutajia kitu muhimu kumhusu:



Huyu Godrey Mushi ni mzima? kwanini alipigwa? Kwanini alikamatwa baada ya kupigwa? Hivi hawa watu hawakuona kuwa kulikuwa na kashfa mbili pale? ile ya Mwangosi na ile ya Mushi? Hivi ingekuwa Mwangosi hajafa pale hii kamati ingechunguza nini kama siyo kupigwa na polisi kwa Mushi?

Hata hivyo kuna ujinga mwingine katika ripoti hii. Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Nchimbi akiokoa jahazi alisema kuwa kuna taarifa ambazo kamati yake (ya serikali) imeweka kibindoni kwa sababu za kimahakama. Ameeleza kuwa mambo hayo yamefichwa ili kuzuia mtu aliyeshtakiwa asije kuitumia kujinusuru. Kwa maneno yake amesema hivi:



Sasa mwenyewe Nchimbi hapa inawezekana aliamini kuwa amezungumza "pointi" sana. Katika mawazo yake haki ya adui yake siyo haki. Kumbe yule mtuhumiwa anayo haki ndio maana mahakamani kwenye kesi hizi wale wa upande wa mashtaka wanatakiwa waweke wazi ushahidi wote ambao wanao hata ule unaoweza kutumiwa kumtoa mtuhumiwa hatiani katika kile kinachoitwa "discovery" kabla ya kesi kuanza. Lengo ni kuhakikisha kuwa ushahidi wowote - wa kumtia mtu hatiani au kumtoa - unawekwa wazi kwa upande mwingine ili kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapewa nafasi ya haki.

Kwa maneno ya Nchimbi serikali inao ushahidi wenye kuonesha kuwa yule mtuhumiwa wa polisi inawezekana asiwe na hatia (hata kama picha zinaonesha kashika bunduki au kweli aliua) na serikali iko tayari kuficha ushahidi huo ili mtuhumiwa yule atiwe hatiani. Sijui wanasheria wetu wanaweza kusema vipi kuhusu haki ya yule mtuhumiwa kuweza kumuita Waziri Nchimbi, Mwenyekiti wa Kamati pamoja na ripoti kamili kama sehemu ya utetezi wake ili waweze kuona kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kumsaidia. Haki ni haki hata kama ni ya adui yako. Si ndio wanasema "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"? Kama kuna ushahidi unaoweza kumtoa yule kijana Polisi hatiani kwanini Nchimbi na Kamati wauweke pembeni?

Si ndio uvunjaji mkubwa zaidi wa haki kwenda kumhukumu mtu kwa sababu hatutaki aachiwe hata kama sababu ya kumwachia ipo?

Simply put, Ni ripoti ya kijinga.
 
Back
Top Bottom