Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

Msingi wa haya yote ni dharau dhidi ya wananchi (contempt of the people). Watawala wanaamini wanaweza kusema lolote, vyovyote, kwa yeyote bila kujali matokeo yake. Hawataki kuulizwa na wakiulizwa wanaona unaleta vurugu.

Tunachezewa, uongo kama huu ni wa kijinga sana, lazima ukemewe
 
Kwa hili wamejivua nguo na wamechezea pesa za walipa kodi,ni dharau hata kwa Rais ambae amekaa kimya kama hajawahi kusikia yote haya,anakamilisha nchi zake ambazo hajafika bado ili kuweka rekodi ya dunia!VDG
 
Wanajua wabongo kama walivyotuzoea ni wajinga. Tutapiga kelele siku mbili tatu yanaisha and will be business as usual. Wala siwalaumu wao, wa kulaumiwa ni Watanzania wenyewe ambao ni wasahaulifu kupita kiasi. Ripoti za kijinga huwa zinatokana na ujinga wa Watanzania. Kama Watanzania wasingekuwa wajinga wasingeandaliwa ripoti za kijinga kama hizi. Mjinga ndiye aliwaye.

Ni ripoti ya kijinga kwa sababu Watanzania ni wajinga. Huo ndio ukweli ulio uchi.
 
Waziri Emmanuel Nchimbi anadai ripoti hiyo imesomwa kwa kuchambua chambua ni kipi kwa sasa kitolewe kama habari kwa umma kwa vile tayari kesi imeshafunguliwa Mahakamani na serikali inaogopa kubanwa na wanasheria na mtuhumiwa kushinda kesi kwa kutumia mgongo wa ripoti ya Kamati ya waziri, sikiliza clip hii Waziri Nchimbi akijaribu kufafanua:



Duh, yetu macho maana wajumbe wa kamati hawaonyeshi kuwa na uwezo wa kuchambua masuala mazito kama haya na kutoa ripoti kwa umma
 
Last edited by a moderator:
Waziri Emmanuel Nchimbi anadai ripoti hiyo imesomwa kwa kuchambua chambua ni kipi kwa sasa kitolewe kama habari kwa umma kwa vile tayari kesi imeshafunguliwa Mahakamani na serikali inaogopa kubanwa na wanasheria na mtuhumiwa kushinda kesi kwa kutumia mgongo wa ripoti ya Kamati ya waziri, sikiliza clip hii Waziri Nchimbi akijaribu kufafanua:



Danganya toto hii,
Hamna kitu hapa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akijua kuwa na wewe una akili akakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau". Hili ni kweli pia kwenye suala hili. Mtu mwenye akili akijua na wewe una akili ahalafu akakuandikia jambo la kijinga na wewe ukalikubali atakudharau!

Hii ripoti ni ushahidi wa kile ambacho wengine tunaamini ni kweli; CCM na serikali yake ni lazima waondolewe madarakani sooner kwa sababu wanatudharau! Ni dharau ya ajabu sana hii. Fikiria mtu anaandika hivi kwenye ripoti:

Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?


Hili swali ni la msingi sana katika tukio zima.

Lakini Kamati imeshindwa kujibu swali ambalo kwa walioona iile video ya mauaji wanalikumbuka sana yaani linalohusiana na kukatazwa kufanyika kwa mikutano ya ndani ya chama. Kamati inatuambia kuwa barua ya zuio hilo inasema hivi:


Kumbe zuio lilihusu "mikutano na maandamano". Kwamba inaweza kujengwa hoja ya kuwa "mikutano" ilimaanisha "mikutano yote" ni vigumu kutetea hasa kwa vile wakati huo huo mikutano mingine ya kisiasa ilikuwa ikifanyika sehemu mbalimbali nchini bila kuzuiwa. Kamati ili kuonesha ulinganifu ingejaribu kutafuta maelezo ya Polisi Zanzibar kwanini waliruhusu CCM kufanya mkutano wake kule wakati kuna zuio. Lakini vile vile ni vigumu kusema kuwa mikutano yote ya kisiasa ya ndani haikuwa imeruhusiwa! Ni vyama vingapi ambavyo vilikuwa na mikutano ya ndani ya kamati zake mbalimbali kati ya August 26-Septemba 8?

Kamati ingeweza ili kulinganisha "utii wa sheria" kwa vyama vingine kuelezea kuwa vyama vingine havikufanya mikutano yoyote kati ya tarehe hizo na ni CHADEMA tu ambao walikuwa na mkutano Iringa. Hoja kuwa CDM hawakuwa watii ingekuwa na nguvu! Nje ya hapo ni kutuandikia ujinga.

Lakini kuthibitisha upuuzi wa kamati hii imeshindwa kuelezea kuwa kwanini katazo hilo liwe halali Iringa lakini Zanzibar lisiwe halali wakati CCM walipofanya uzinduzi wa kampeni yao ya Bububu? Hiki ndio kipimo cha upuuzi wa ripoti hii. Kama amri ambazo zilitolewa zilihusu vyama vyote kwanini Zanzibar waliendelea na mikutano ya kisiasa? Au wao hawakutakiwa kutiia sheria hiyo au kwa vile hakukutokea machafuko yoyote (na hayajawahi kutokea yakisababishwa na polisi!) huko Zanzibar?

Ikumbukwe kuwa uhalali wote wa polisi kutumia nguvu kuwatanya CHADEMA pale Nyololo unatokana na ukweli kuwa mkutano ule ulikuwa haramu. Lakini kama mkutano ulikuwa halali (kwa maana ya mkutano wa ndani ambao haukukatazwa) uhalali wa kutumia polisi unatoka wapi?

Ili kuthibitisha kuwa ilikuwa ni ripoti ya kijinga ni kuwa Kamati haikuwahoji wale polisi waliokuwa wamemzunguka Mwangosi na haijamhoji yule mtuhumiwa ili aelezee ilikuwaje yeye na wenzake wamshambulie Mwangosi na kwanini atumie nguvu zaidi. Inashangaza tu kuwa ripoti inataka wachukuliwe hatua za kisheria. Na kamati inaonekana haikuchukua muda kuangalia ile video au hata kuitisha watu waliokuwepo kuwapatia picha za video za tukio hilo zima. Na cha kushangaza Kamati hii iliyofanya mambo mengi ya uchunguzi imeshindwa kutoa jibu au hata dokezo la vilikopotelea vifaa vya kazi vya Mwangosi (kamera na laptop)!!

Lakini vile vile ripoti hii ambayo nina uhakika imetumia fedha ya kutosha tu (sijui nani atauliza Bungeni tuambiwe) imeshindwa kumhoji au hata kutuambia maoni ya shahidi muhimu sana katika sakata hili. Ripoti inatutajia kitu muhimu kumhusu:



Huyu Godrey Mushi ni mzima? kwanini alipigwa? Kwanini alikamatwa baada ya kupigwa? Hivi hawa watu hawakuona kuwa kulikuwa na kashfa mbili pale? ile ya Mwangosi na ile ya Mushi? Hivi ingekuwa Mwangosi hajafa pale hii kamati ingechunguza nini kama siyo kupigwa na polisi kwa Mushi?

Ni ripoti ya kijinga.

Mkuu thanks for the good take. Lakini hapo kwenye RED', jambo moja inabidi tujue Serikali ya CCM imekuwa haikosi majibu ya kutetea upuuzi wake. Mara nyingi imekuwa ikitumia silaha ya majibu mepesi (unaweza kuyaita ya kijinga) katika maswali magumu na ya msingi kwa mustakabali wa taifa.

Utakumbuka katika Bunge lililopita kwenye maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Mchungaji Msigwa aliuliza kwa nini katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Zanzibar ilipiga marufuku watu kuuza vyakula mchana, kula mchana na kuvaa mavazi yasiyo ya kustili mwili. Msigwa alikuwa anashangazwa nai katazo hilo kwani ni wazi lina mlengo wa kidini na kwa kweli ni kama kuutangazia Ulimwengu kuwa Zanzibar ni nchi ya kidini ukiacha ukweli kwamba zuio hilo lilikuwa kinyume cha haki na uhuru binafsi wa raia.

Waziri Mkuu Pinda alijibu majibu mepesi (ya kipuuzi) kwamba, Zanzibar ina utaratibu wake na ina Serikali yake. Ni kama vile Serikali ya Muungano na kwa maana hiyo Waziri Mkuu hana mamlaka juu ya Zanzibar. Sasa haitashangaza hata hiyo oja ya Mikutano ya CCM Bububu ikawa na majibu yake ya kipuuzi kama haya. Majibu mepesi katika masuala mazito ndiyo imekuwa silaha ya CCM na viongozi waliochoka muda wote.

Kitu kinacholeta kichekesho ni namna kamati hiyo inapokubaliana na makatazo ya Polisi na Tendwa bila hata kuchimbua uhalali wake kisheria na kikatiba. Yaani wamebase kwenye katazo lolote linalotoka kwenye mamlaka fulani lazima litekelezwe hata kama lina walakini kisheria na uhalali wake unatiliwa shaka hasa kutokana kutokana na katazo hilo kulenga chama fulani tu.
 
Mkuu MKJJ,
You nailed it. Hainingii kichwani kwa mtu kama Makunga kukubali kuharibu credibility kwa manufaa ya kikundi fulani cha watu. Ni upuuzi kwa so called "KAMATI" kushindwa kupata majibu ya kile kilichotokea Nyololo, sasa wangewezaje kupata majibu wakati wahusika wakuu IGP, RPC Iringa (Kamuhanda), Chagonja, na yule PC aliyefumua lile bomu hawakuweza kuhojiwa?? Huku ni kuchezea akili ya watanzania na kutuonyesha dharau. Kuna umuhimu gani wa kuendelea kusoma magazeti ya mwananchi? NIMESUSIA KUSOMA MWANANCHI.
 
Mkuu thanks for the good
take. Lakini hapo kwenye RED', jambo moja inabidi tujue Serikali ya CCM
imekuwa haikosi majibu ya kutetea upuuzi wake. Mara nyingi imekuwa
ikitumia silaha ya majibu mepesi (unaweza kuyaita ya kijinga) katika
maswali magumu na ya msingi kwa mustakabali wa taifa.

Utakumbuka katika Bunge lililopita kwenye maswali ya papo kwa papo kwa
Waziri Mkuu, Mchungaji Msigwa aliuliza kwa nini katika mfungo wa mwezi
mtukufu wa Ramadhan Zanzibar ilipiga marufuku watu kuuza vyakula mchana,
kula mchana na kuvaa mavazi yasiyo ya kustili mwili. Msigwa alikuwa
anashangazwa nai katazo hilo kwani ni wazi lina mlengo wa kidini na kwa
kweli ni kama kuutangazia Ulimwengu kuwa Zanzibar ni nchi ya kidini
ukiacha ukweli kwamba zuio hilo lilikuwa kinyume cha haki na uhuru
binafsi wa raia.

Waziri Mkuu Pinda alijibu majibu mepesi (ya kipuuzi) kwamba, Zanzibar
ina utaratibu wake na ina Serikali yake. Ni kama vile Serikali ya
Muungano na kwa maana hiyo Waziri Mkuu hana mamlaka juu ya Zanzibar.
Sasa haitashangaza hata hiyo oja ya Mikutano ya CCM Bububu ikawa na
majibu yake ya kipuuzi kama haya. Majibu mepesi katika masuala mazito
ndiyo imekuwa silaha ya CCM na viongozi waliochoka muda wote.

Kitu kinacholeta kichekesho ni namna kamati hiyo inapokubaliana na
makatazo ya Polisi na Tendwa bila hata kuchimbua uhalali wake kisheria
na kikatiba. Yaani wamebase kwenye katazo lolote linalotoka kwenye
mamlaka fulani lazima litekelezwe hata kama lina walakini kisheria na
uhalali wake unatiliwa shaka hasa kutokana kutokana na katazo hilo
kulenga chama fulani tu.

ulitegemea nini wakati katibu ni ofisa mwandamizi wa polisi?
 
jana niliweka post mbili nikionyesha upeo duni wa ripoti kuanzia hadidu za rejea zisizo na focus, kuripoti badala ya kuchunguza, wahusika wakuu kutohojiwa, mapendekezo dhaifu na mengine.

Hakuna post hata moja kati ya nilizotuma imetoka hapa JF!
 
Mwanakijiji, ulitarajia kitu tofauti?

Hujui ccm wamewachukulia wananchi kama mizombie isiyoelewa lolote?

Wanadhani wanaweza waeleza lolote nao wanakubali tu?

Na dharau hawakuanza leo ndugu.............. Na hayo ndo malipo ya kosa wafanyalo watanzania kwenye sanduku la kupigia kura.....
 
Last edited by a moderator:
Mambo mengine yanayofanyika katika nchi hii ni ya kusikitisha sana, nautilia shaka sana uwezo wa kufikiri wa Watanzania, ripoti ya kijinga namna ile huwezi kuileta kwa watu mpaka uwe una uhakika kwamba uwezo wao wa kufikiri ni duni sana, nawapeni pole sana Watanzania, poleni sana ndugu zangu Watanzania.

dharau nyingine za kipuuzi, matumizi yake yaweyanaishia kwenye uvungu wa kitanda chako unachotumia na mwenza wako.
 
Mkuu kuna wakati kweli hapa JF kuna vituko. Katika kumbukumbu zangu za utu uzima sikumbuki hata siku moja kama kuna tume iliyoundwa na kuleta matokeo yanayotakiwa. Kuna tume nyingi zimewahi kuundwa, nyingine zilifanya exellent job, lakini matokeo ya baadhi hadi leo yamefichwa, nyingine zikapuuzwa kwa kusema zilikwenda kinyume na "hadidu za rejea", na nyingine zilikuwa za kitoto kitoto kama hii tunayoizungumzia sasa. Ambazo watu walikwenda kutembea tu, kula, kulala na kuandika "makala" ya kufikirika na kuiita ripoti.

Kama tunakumbuka toka mwanzo tulisema kuwa imetoka hiyo, Mwangosi ameuawa hakuna haki itakayotendeka......the fate will be similar to many others, kama ile ya Lunkombes waliouawa Sinza....... sana sana wauaji watapewa promotion au zawadi nyingine kwa kazi "nzuri' waliyofanya. This is the reality.

.









.






.
Kaka inakera!!

Hata ripoti ya mwakyembe ya richmond, Mwakyembe mwenyewe amekiri kuwa kuna vitu vilifichwa!!!

Ripoti nzima... hakuna sehemu ilipozungumzia kitu kinachoitwa HAKI!!!

Ni ***** tu!! *****!!!







..


..
 
Mukama alikuwa mmoja wa wahojiwa na aliyoyasema ndiyo ikawa major concluding point...kuhusu vyama vya siasa kutofanya siasa za nje bali bungeni ili watu wafanye kazi
 
Back
Top Bottom