Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 10, 2012.

  1. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #1
    Oct 10, 2012
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 31,077
    Likes Received: 5,241
    Trophy Points: 280
    Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akijua kuwa na wewe una akili akakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau". Hili ni kweli pia kwenye suala hili. Mtu mwenye akili akijua na wewe una akili ahalafu akakuandikia jambo la kijinga na wewe ukalikubali atakudharau!

    Hii ripoti ni ushahidi wa kile ambacho wengine tunaamini ni kweli; CCM na serikali yake ni lazima waondolewe madarakani sooner kwa sababu wanatudharau! Ni dharau ya ajabu sana hii. Fikiria mtu anaandika hivi kwenye ripoti:

    Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?


    Hili swali ni la msingi sana katika tukio zima.

    Lakini Kamati imeshindwa kujibu swali ambalo kwa walioona iile video ya mauaji wanalikumbuka sana yaani linalohusiana na kukatazwa kufanyika kwa mikutano ya ndani ya chama. Kamati inatuambia kuwa barua ya zuio hilo inasema hivi:
    Kumbe zuio lilihusu "mikutano na maandamano". Kwamba inaweza kujengwa hoja ya kuwa "mikutano" ilimaanisha "mikutano yote" ni vigumu kutetea hasa kwa vile wakati huo huo mikutano mingine ya kisiasa ilikuwa ikifanyika sehemu mbalimbali nchini bila kuzuiwa. Kamati ili kuonesha ulinganifu ingejaribu kutafuta maelezo ya Polisi Zanzibar kwanini waliruhusu CCM kufanya mkutano wake kule wakati kuna zuio. Lakini vile vile ni vigumu kusema kuwa mikutano yote ya kisiasa ya ndani haikuwa imeruhusiwa! Ni vyama vingapi ambavyo vilikuwa na mikutano ya ndani ya kamati zake mbalimbali kati ya August 26-Septemba 8?

    Kamati ingeweza ili kulinganisha "utii wa sheria" kwa vyama vingine kuelezea kuwa vyama vingine havikufanya mikutano yoyote kati ya tarehe hizo na ni CHADEMA tu ambao walikuwa na mkutano Iringa. Hoja kuwa CDM hawakuwa watii ingekuwa na nguvu! Nje ya hapo ni kutuandikia ujinga.

    Lakini kuthibitisha upuuzi wa kamati hii imeshindwa kuelezea kuwa kwanini katazo hilo liwe halali Iringa lakini Zanzibar lisiwe halali wakati CCM walipofanya uzinduzi wa kampeni yao ya Bububu? Hiki ndio kipimo cha upuuzi wa ripoti hii. Kama amri ambazo zilitolewa zilihusu vyama vyote kwanini Zanzibar waliendelea na mikutano ya kisiasa? Au wao hawakutakiwa kutiia sheria hiyo au kwa vile hakukutokea machafuko yoyote (na hayajawahi kutokea yakisababishwa na polisi!) huko Zanzibar?

    Ikumbukwe kuwa uhalali wote wa polisi kutumia nguvu kuwatanya CHADEMA pale Nyololo unatokana na ukweli kuwa mkutano ule ulikuwa haramu. Lakini kama mkutano ulikuwa halali (kwa maana ya mkutano wa ndani ambao haukukatazwa) uhalali wa kutumia polisi unatoka wapi?

    Ili kuthibitisha kuwa ilikuwa ni ripoti ya kijinga ni kuwa Kamati haikuwahoji wale polisi waliokuwa wamemzunguka Mwangosi na haijamhoji yule mtuhumiwa ili aelezee ilikuwaje yeye na wenzake wamshambulie Mwangosi na kwanini atumie nguvu zaidi. Inashangaza tu kuwa ripoti inataka wachukuliwe hatua za kisheria. Na kamati inaonekana haikuchukua muda kuangalia ile video au hata kuitisha watu waliokuwepo kuwapatia picha za video za tukio hilo zima. Na cha kushangaza Kamati hii iliyofanya mambo mengi ya uchunguzi imeshindwa kutoa jibu au hata dokezo la vilikopotelea vifaa vya kazi vya Mwangosi (kamera na laptop)!!

    Lakini vile vile ripoti hii ambayo nina uhakika imetumia fedha ya kutosha tu (sijui nani atauliza Bungeni tuambiwe) imeshindwa kumhoji au hata kutuambia maoni ya shahidi muhimu sana katika sakata hili. Ripoti inatutajia kitu muhimu kumhusu:

    Huyu Godrey Mushi ni mzima? kwanini alipigwa? Kwanini alikamatwa baada ya kupigwa? Hivi hawa watu hawakuona kuwa kulikuwa na kashfa mbili pale? ile ya Mwangosi na ile ya Mushi? Hivi ingekuwa Mwangosi hajafa pale hii kamati ingechunguza nini kama siyo kupigwa na polisi kwa Mushi?

    Hata hivyo kuna ujinga mwingine katika ripoti hii. Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Nchimbi akiokoa jahazi alisema kuwa kuna taarifa ambazo kamati yake (ya serikali) imeweka kibindoni kwa sababu za kimahakama. Ameeleza kuwa mambo hayo yamefichwa ili kuzuia mtu aliyeshtakiwa asije kuitumia kujinusuru. Kwa maneno yake amesema hivi:

    Sasa mwenyewe Nchimbi hapa inawezekana aliamini kuwa amezungumza "pointi" sana. Katika mawazo yake haki ya adui yake siyo haki. Kumbe yule mtuhumiwa anayo haki ndio maana mahakamani kwenye kesi hizi wale wa upande wa mashtaka wanatakiwa waweke wazi ushahidi wote ambao wanao hata ule unaoweza kutumiwa kumtoa mtuhumiwa hatiani katika kile kinachoitwa "discovery" kabla ya kesi kuanza. Lengo ni kuhakikisha kuwa ushahidi wowote - wa kumtia mtu hatiani au kumtoa - unawekwa wazi kwa upande mwingine ili kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapewa nafasi ya haki.

    Kwa maneno ya Nchimbi serikali inao ushahidi wenye kuonesha kuwa yule mtuhumiwa wa polisi inawezekana asiwe na hatia (hata kama picha zinaonesha kashika bunduki au kweli aliua) na serikali iko tayari kuficha ushahidi huo ili mtuhumiwa yule atiwe hatiani. Sijui wanasheria wetu wanaweza kusema vipi kuhusu haki ya yule mtuhumiwa kuweza kumuita Waziri Nchimbi, Mwenyekiti wa Kamati pamoja na ripoti kamili kama sehemu ya utetezi wake ili waweze kuona kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kumsaidia. Haki ni haki hata kama ni ya adui yako. Si ndio wanasema "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"? Kama kuna ushahidi unaoweza kumtoa yule kijana Polisi hatiani kwanini Nchimbi na Kamati wauweke pembeni?

    Si ndio uvunjaji mkubwa zaidi wa haki kwenda kumhukumu mtu kwa sababu hatutaki aachiwe hata kama sababu ya kumwachia ipo?

    Simply put, Ni ripoti ya kijinga.
     
  2. kookolikoo

    kookolikoo JF-Expert Member

    #2
    Oct 10, 2012
    Joined: Mar 9, 2012
    Messages: 2,524
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 135
    ndo maana chadema hawakuipa ushirikiano!
     
  3. Inkoskaz

    Inkoskaz JF-Expert Member

    #3
    Oct 10, 2012
    Joined: Nov 6, 2010
    Messages: 6,292
    Likes Received: 315
    Trophy Points: 180
    Watu walienda kutalii Iringa,ripoti imetungwa hapa hapa Dar
     
  4. Matola

    Matola JF-Expert Member

    #4
    Oct 10, 2012
    Joined: Oct 18, 2010
    Messages: 33,789
    Likes Received: 8,361
    Trophy Points: 280
    Hata wewe brother ni kweli ulikuwa unatalajia ripoti tofauti na hii!!?? pole sana
     
  5. Viol

    Viol JF-Expert Member

    #5
    Oct 10, 2012
    Joined: Dec 15, 2009
    Messages: 18,643
    Likes Received: 573
    Trophy Points: 280
    Polisi hawajahojiwa,mtuhumiwa hajahojiwa,na hawajui waliowatuma wauaji,sasa uchunguzi gani wamefanya!
    aibu kweli
     
  6. A

    Africa_Spring JF-Expert Member

    #6
    Oct 10, 2012
    Joined: Jun 16, 2012
    Messages: 428
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Lisu aliisha sema...hii sio kamati ya kweli. Nchimbi hawezi kutengeneza kamati ya ukweli coz itakuja kumuondoa yeye na sio watu wadogo wa chini. Nchimbi anatakiwa kujiuzuri thats only solution. Anatapa tapa huku kule lakini watu wenye akili zao wameisha muona Nchimbi hasafishiki.
     
  7. t

    tenende JF-Expert Member

    #7
    Oct 10, 2012
    Joined: Jan 10, 2012
    Messages: 6,560
    Likes Received: 6
    Trophy Points: 135
    Walioshiriki kuandaa ripoti hii wao wenyewe ni janga la taifa, ni lazima tufanye kitu (mf. maandamano) kupinga ujinga huu. Vinginevyo tunatengeneza taifa la visasi dhidi ya wauaji na watetezi wa wauaji kama hawa!. Je, ninani anayeweza vumilia ujinga huu pale mtu anayemhusu kauawa na watu wanalindana kipuuzi puuzi namna hii?
     
  8. M

    Msemakweli Daima Member

    #8
    Oct 10, 2012
    Joined: Jul 16, 2012
    Messages: 55
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 13
    Mambo mengine yanayofanyika katika nchi hii ni ya kusikitisha sana, nautilia shaka sana uwezo wa kufikiri wa Watanzania, ripoti ya kijinga namna ile huwezi kuileta kwa watu mpaka uwe una uhakika kwamba uwezo wao wa kufikiri ni duni sana, nawapeni pole sana Watanzania, poleni sana ndugu zangu Watanzania.
     
  9. Bongolander

    Bongolander JF-Expert Member

    #9
    Oct 10, 2012
    Joined: Jul 10, 2007
    Messages: 4,882
    Likes Received: 33
    Trophy Points: 135
    Mkuu kuna wakati kweli hapa JF kuna vituko. Katika kumbukumbu zangu za utu uzima sikumbuki hata siku moja kama kuna tume iliyoundwa na kuleta matokeo yanayotakiwa. Kuna tume nyingi zimewahi kuundwa, nyingine zilifanya exellent job, lakini matokeo ya baadhi hadi leo yamefichwa, nyingine zikapuuzwa kwa kusema zilikwenda kinyume na "hadidu za rejea", na nyingine zilikuwa za kitoto kitoto kama hii tunayoizungumzia sasa. Ambazo watu walikwenda kutembea tu, kula, kulala na kuandika "makala" ya kufikirika na kuiita ripoti.

    Kama tunakumbuka toka mwanzo tulisema kuwa imetoka hiyo, Mwangosi ameuawa hakuna haki itakayotendeka......the fate will be similar to many others, kama ile ya Lunkombes waliouawa Sinza....... sana sana wauaji watapewa promotion au zawadi nyingine kwa kazi "nzuri' waliyofanya. This is the reality.
     
  10. c

    chama JF-Expert Member

    #10
    Oct 10, 2012
    Joined: Aug 6, 2010
    Messages: 8,006
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 0
    Yakhe andika yako utupe yao huitaki
     
  11. n

    nemasisi JF-Expert Member

    #11
    Oct 10, 2012
    Joined: Oct 4, 2012
    Messages: 1,841
    Likes Received: 65
    Trophy Points: 145
    Ni utoto tu make mimi ningetegemea watupe ufafanuzi kwa nini walizuia mikutano ya siasa na wakati huo huo mikusanyiko mingine kama mechi za soka, sherehe za harusi nk vikaachwa viendelee? Kikubwa hapa nadhani wana hamu ya kupiga marufuku vyama vya upinzani na hasa cdm kufanya siasa baada ya uchaguzi, hii ni dhambi sawa tu na ubakaji.
    Hivi kusema siasa zihamie bungeni maana yake nini? kwa mtizamo wangu ni kwamba kamati inataka kuiokoa ccm kwa sababu wamegundua kuwa wananchi walio wengi wanawaamini na kuwasuport chadema kuliko ilivyo kwao, ni kama wanakiri kuzidiwa majukwaani na kwahiyo wanajua mahali pekee wanapoweza kutamba kwa urahisi ni bungeni ambako ni wengi na wanahodhi maamuzi ya kipi wangependa kizungumzwe ambacho hakitishii maslahi ya chama hicho.

    Naamini kabisa kamati hii ni sehemu ya maandalizi ya mkakati wa ccm kuzima nguvu za vyama vya upinzani kabla ya uchaguzi ujao, ndiyo, lengo ni hilo kwa sababu hoja ya kwamba wananchi waachwe wafanye kazi ni ya kijinga kama sio ya kipumbavu maana sijawahi kusikia wananchi wakilazishwa kuacha kazi zao ili wahudhurie mkutano wa siasa. Lakini zaidi hii mikutano inafanyika mara ngapi kwa eneo moja mpaka ifikie mahala tukasema inaathiri shughuli za wananchi? Au ndo haya aliyosema wassira kwamba chadema haitafika 2015? yangu macho!
     
  12. P

    Precise Pangolin JF-Expert Member

    #12
    Oct 10, 2012
    Joined: Jan 4, 2012
    Messages: 11,838
    Likes Received: 1,311
    Trophy Points: 280
    Hii report ilivyowekwa Jana hapa jamvin na mkuu n00b nilicomment kamwe sitaisoma kwasababu nilikuwa nimeshajua report itakuwaje tokea kuanzishwa kwake nikaenda zangu bar kupiga tursker za baridiii Huku nikiwa na browse kwenye jukwaa la MMU na wakina Smile kukwepa stress na kufa kwa mihasira
     
    Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
  13. Mtambuzi

    Mtambuzi Platinum Member

    #13
    Oct 10, 2012
    Joined: Oct 29, 2008
    Messages: 8,752
    Likes Received: 1,134
    Trophy Points: 280
    Mnapiga kelele wakati ripoti ina baraka za wanahabari..... (watu wamegeuka wachumia tumbo)
     
  14. Edson Zephania

    Edson Zephania Verified User

    #14
    Oct 10, 2012
    Joined: Apr 8, 2011
    Messages: 507
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    Ila SHIBUDA alihojiwa na hii kamati
     
  15. Keen

    Keen JF-Expert Member

    #15
    Oct 10, 2012
    Joined: Sep 27, 2007
    Messages: 620
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 35
    Nashindwa kuelewa jambo moja. Kama kifo cha mwangosi hakihusiani na nguvu ya polisi kama ripoti inavyosema, kwani anayetuhumiwa kwa kumuua mwangosi si askari polisi? Au mimi niko nje ya network!!?
     
  16. MpigaFilimbi

    MpigaFilimbi JF-Expert Member

    #16
    Oct 10, 2012
    Joined: Apr 30, 2008
    Messages: 1,171
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 133
    ...Hii ndiyo Tanzania yetu..watu wamebakia kupiga dili tu.
     
  17. hovyohovyo

    hovyohovyo JF-Expert Member

    #17
    Oct 10, 2012
    Joined: Jul 8, 2012
    Messages: 540
    Likes Received: 17
    Trophy Points: 35
    Yaani imelenga na kurudia kauli ya Tambwe Hiza. Useless report.
     
  18. tanira1

    tanira1 JF-Expert Member

    #18
    Oct 10, 2012
    Joined: Nov 18, 2011
    Messages: 938
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    mkuu hama hakika ni ripoti ya kijinga ccm na serikali yake ilishatudharau siku nyingi sana na ndio maana hawaishiwi wala hawaoni aibu kutoa lipoti zao za ovyo ovyo wakiamini mitanzania ni mijitu mijinga na ya kuburuza tuu wizi wa epa wanatoa ripoti hakuna muhusika wizi wa fedha za rada wanakwambia hakuna haliyeusika ilihali wanagawana fedha zilizo rejeshwa tena bungeni kwa kununulia vitabu huu ni ujinga na dharau iliyokubuu kwa watanzania, mtu anauawa na polisi tena kwa risasi unakuta mkuu wa polisi anasema marehemu alidondokewa na kitu kizito huu ni ujinga unaopaswa kuelezwa kwa wajinga sasa kama ndivyo tulitegemea kupata ripoti hiyo ya kijinga na hakika kila mtanzania hata wa kijijini alitegemea kusikia ujinga huo walisubiri tu wathibitishe ya kuwa wataleta ujinga tunaoutarajia? na ndivyo ilivyokuwa kwa kifupi wanajidanganya na mapambano yataendelea
     
  19. Duble Chris

    Duble Chris JF-Expert Member

    #19
    Oct 10, 2012
    Joined: May 28, 2011
    Messages: 3,490
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 135
    Mzee Mwanakijiji umenena

    Tukumbuke pia kuwa wakati huo kulikuwa na Uzinduzi huko Bububu wa kampeni za CCM, Fiesta Mwanza na mikutano mingi ya ndani ya CCM iliyo kuwa maalmu kwa kuteua wagombea. Lakini kamati haikutaka kuumiza kichwa kwa nini hawa waliendelea bila shida

    swali lililo waudhi polisi ni pale walipo ulizwa maana ya mkutano wa ndani " Je, mkutano wa ndani ni atu kujifungia ndani au ni ule unao wahusu wanachama tu, " kamati haikutaka pia kuumiza kicha kuwa huo mkutano wa Chadema ulikuwa a ndani au wa nje.

    Mambo mengine lazima busara zitawale/ziongoze hivi ni sensa gani ya kutafuta watu 5% tu kuanzia saa 10 jioni tena kijijini ingewezekana> Makarani wa sensa walifanyakazi hadi saa ngapi katika muda huo wa ziada ??

    Pia kamati haijajibu swali Chama cha siasa kifanyenini kinapo onaknaonewa je, kuna nafasi ya kukata rufaa ? kwa nani ? Ndugu wana JF naomba sana na hili tuliangalie kwa kina :

    " kimsingi mikutano inagharama sana, fikiria kuwa chama kimeandaa mkutano kwa muda mrefu kwa gharama kubwa, halafu siku 1 kabla ya mkutano anakuja mtu anatoa amri marufuku kufanya mkutano hapo hafikirii gharama walizo tumia " kamati yangu haikuliona hili
     
  20. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #20
    Oct 10, 2012
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 31,077
    Likes Received: 5,241
    Trophy Points: 280
    Msingi wa haya yote ni dharau dhidi ya wananchi (contempt of the people). Watawala wanaamini wanaweza kusema lolote, vyovyote, kwa yeyote bila kujali matokeo yake. Hawataki kuulizwa na wakiulizwa wanaona unaleta vurugu.
     
Loading...