Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,520
- 830,064
Waulize watalaka na watalikiwa watakuambia. Kwenda kwenye ndoa ni rahisi kuliko kurudi kwenye ndoa baada ya kuondoka kwenye ndoa.
Kijana wangu alipewa suspension shuleni nikaambiwa nikamchukue nirudi naye nyumbani. Kwenda kumchukua ilikuwa rahisi. Kumrudisha imekuwa ngumu sana.
Mambo yalipoharibika Sodoma Lutu aliondoka na familia yake lakini mkewe akataka kurudi hivyo akageuka nyuma na kugeuka kuwa jiwe la chumvi.
Kipigo kwenye ulingo wa ndondi kikikupeleka chini na ukachelewa kusimama hutaweza tena kurejea ulingoni uendelee na mapigano. Hata mpiganishi akikuhesabia mpaka kumi.
Kuna kitu kwenye saikolojia kinaitwa confidence. Wana usalama wanalifundishwa sana. Kumwangalia mtu usoni machoni bila kupepesa, akiangusha tu macho chini hawezi kurudi kukuangalia tena!
Mashindano hayakimbiwi. Ukiyakimbia tambua umekubali kutema bungo
Mtunzi mahiri JAMES HADLEY CHASE ana riwaya yake moja inaitwa THE GUILTY ARE AFRAID! yaani wenye hatia wana hofu na hukimbia hata wasipokimbizwa.
Hatia humfanya mtu akimbie hata kivuli chake mwenyewe!
Ni sawa tu na, kunguru mwoga ambaye hukimbiza bawa lake. Maana hajiamini amejawa hofu na kujihisi mwenye hatia
Kwenda ni rahisi kuliko kurudi!!!