Ni nini kilichokuleta kwa mara ya kwanza kabisa jijini Dar-es-salaam!

Hahahaaa, wee sema umefyatuliwa Wodi namba ngapi? Unajua manesi wa Dar walivyo wakorofi? Sijui matusi aliyoyapata mama wakati unafyatulia..... "Wanaume basi tena? You will be back Honey........."

Ila hujatuambia Wazazi waliku-CONCEIVE wapi? Kwenye Kivuko kwenda Chuo Cha CCM Kigamboni au Chuoni penyewe?

Au ndiyo ile mitaa ya HQ za CCM pale Mnazimmoja? Pole sana maana Lowassa kashauza hilo jengo ulipoanzia maisha.

Mie wa shamba hata sijui maana si unafahamu Shamba kila kitu ni TABU. Huwezi kuambiwa hata jina la MAMA/BABA. Ndiyo maana ukienda shule unasikia UNENE UBABA nyingi sana maana ukiulizwa jina lako unajibu (Unene - yaani MIMI) na jina la baba unajibu (Uvava).

Alitokea kijana akawa anaitwa Seleman VAVAVA kwani jina la baba alijibu ni BABA.

Mitaa ya Sikonge huko ndaaani kabisa, unaenda hadi Chabutwa na ukifika pale unashuka na kutembea kilomoita kama 5 ndani huko hata barabara hamna zaidi ya Punda na hapo kuna kitongoji kinaitwa NKEKI. Probably nilizaliwa hapo kama mama aliwahi maana vinginevyo, wengi huwa wanazaliwa shamba, kwenye kuchuma uyoga au kukata kuni.

Overly talkative...Ha! Ha! Ha!
 
nilikuja kusoma DIT enzi hizo Dsm Tech. College miaka ya 90 na baada ya hapo nimelikimbia jiji, niko mikoani maana hapo deal ilinishinda
 
nilikuja kusoma DIT enzi hizo Dsm Tech. College miaka ya 90 na baada ya hapo nimelikimbia jiji, niko mikoani maana hapo deal ilinishinda
 
Teteteee, kumbe ndipo walipokuFYATULIA................ hihiiiiii...... Mie nilipotea kwenye TRAIN na kuja kuibukia Dar. Kwa bahati wakaniokota na kunirudisha Shamba Sikonge. Huwa narudi kwa nadra sana hapo Dar maana naogopa wingi wa magari.[/QU umetisha sikonge..tehtehtehteh...!
 
Mimi nimezaliwa Ocean Road, Aga Khan Hospital..

Mita mia karibia na Ikulu, mita mia karibia na bahari, mita mia karibia na uwanja wa gofu..

Tukitoka Dar tunaenda Ulaya na Marekani then tunarudi tena hapa hapa Dar...karibuni sana wakuja
Kweli wewe noma hapo kwenye red.Umezaliwa mara mbili kwenye hosiptali tofauti.LOLOOOOL JF KWELI KUNA WATU..ritz kweli kiboko
 
Aga Khan Hospital ipo katikia barabara ya ocean (ocean road) ....sio hospitali mbili hizo
 
Nilikuja kusoma tuition mchikichinini nilikuwa combination ya sayansi,nilishangaa sana nilipokuta bongo hadi kiswahili watu wanasoma tuition.
 
Nilikuja kusoma tuition mchikichinini nilikuwa combination ya sayansi,nilishangaa sana nilipokuta bongo hadi kiswahili watu wanasoma tuition.

unashangaa kiswahili watu primary somo la sanaa watu wanasoma tuition!bongo ni zaidi ya uijuavyo!!!!!sema kwa TZ hamna kama dar es salaam!tena kinondoni ndo dar es salaam yenyewe!
 
Sijawahi kufika na sina hakika kama nitakuja huko, mimi hapahapa Kavifuti pananitosha napata kila kitu!
 
nimezaliwa jijini dar....ila maisha yamenisukuma kijijini na sitegemei kurudi mjini hahahahaahah!
 
Mshua alipewa transfer kuja kwenye hili lijiji la watu wa ajabu na washamba.
Ilikuwa 1986!
 
aaagh! mmenikumbusha mbali sana aisee, enzi hizo jiji linajulikana kama mzizima duka la kuuza sigara lilikuwa moja tu maeneo ya shekilango na ukitaka fegi lazima uende na barua ya balozi wa nyumba 10, nilifika mara ya kwanza kuleta biashara ya mijusi kutoka lushoto kuwauzia masingasinga, dah! nilipata shida sana kutafuta fegi, siku 4 nafuatilia fegi 1 tu ya tropical.
 
Back
Top Bottom