Ni nini kilichokuleta kwa mara ya kwanza kabisa jijini Dar-es-salaam!

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
WanaJF wenzangu habari za mida nimekumbuka mbali sana mara tuu nilipomkumbuka marehemu mjombaangu aliyekimbilia jijini hapa tangu miaka ya 1987 baada ya kukorofishana na baba yake mzazi juu ya suala zima la kumshinikiza kuoa na kuishi kijijini mara baada ya kuhitimu elimu yake ya msingi ambayo hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari.

Kwa hiyo hapa jijini kuna wengi ambao si wazaliwa wa hapa ambao kila mmoja alikuja kwa namna yake.Kuna aliyekuja kwa kheri kuna waliokuja kwa shari kama mjombaangu, kwa matumaini ya kutafuta maisha na kufanikiwa mara baada ya kufika Dar es salaam.Kuna waliofanikiwa na kuwa matajiri wakubwa na wengine hawajafanikiwa hadi hivi sasa lakini tumaini lao likiwa ni moja tuu kuwa ipo siku watajaaliwa na mwenyezi mungu.

Hivyo basi nikaona ni vyema wanaJF wenzangu tukakumbushana kila mmoja kwa mara yako ya kwanza ulifikafikaje Dar es salaam na ulikuja kutafuta nini na kwanini na jee umekwishafanikiwa?
 
Lol, mie nilikuja kutuma maombi chuo kikuu miaka ile ya 90,s si unajua enzi zile kila kitu ili ukifanye kwa ufanisi, lazima ufike Dar! Sikufanikiwa kwa mara ya kwanza japo baadae Mola alijaalia. Umenikumbusha mbaaaaaaaaali!
 
WanaJF wenzangu habari za mida nimekumbuka mbali sana mara tuu nilipomkumbuka marehemu mjombaangu aliyekimbilia jijini hapa tangu miaka ya 1987 baada ya kukorofishana na baba yake mzazi juu ya suala zima la kumshinikiza kuoa na kuishi kijijini mara baada ya kuhitimu elimu yake ya msingi ambayo hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari.

Kwa hiyo hapa jijini kuna wengi ambao si wazaliwa wa hapa ambao kila mmoja alikuja kwa namna yake.Kuna aliyekuja kwa kheri kuna waliokuja kwa shari kama mjombaangu, kwa matumaini ya kutafuta maisha na kufanikiwa mara baada ya kufika Dar es salaam.Kuna waliofanikiwa na kuwa matajiri wakubwa na wengine hawajafanikiwa hadi hivi sasa lakini tumaini lao likiwa ni moja tuu kuwa ipo siku watajaaliwa na mwenyezi mungu.

Hivyo basi nikaona ni vyema wanaJF wenzangu tukakumbushana kila mmoja kwa mara yako ya kwanza ulifikafikaje Dar es salaam na ulikuja kutafuta nini na kwanini na jee umekwishafanikiwa?

Kwanza kabisa Elimu
 
Nilipochaguliwa kwenda shule ya Pugu sec hapo ndio mwanzo wangu kufika mjini lakini leo nimeshindwa kuondoka..
 
nlikuja kufanya matriculation kwa ajili ya kujoin chuo, ndo sijarudi hadi leo, nimenogewa na jiji hili,
 
wengine tushaondoka huko bana
nilikuja kwa ajili ya elimu pale jitegemee na then chuo ila baada ya hapo tukalikimbia jiji lenu
 
Nilipokuja Azania Secondary kufanya PCM.Looooh umenikumbusha mbali sana maeneo ya Faya na Kariakoo.Siku za Ijumaa mpaka J2 Midundiko na michiriku kwa sanaaaaaa.
 
Nilitoka iringa kumfuata mupenzi then deal zingine zikajitokeza ,tumeshasalitiana long time ila nafurai kuwa naye sababu nlijipanga sana !
 
Kiukweli chuo cha udsm ndo kimeleta wengi, unajua zamani chuo kikuu kilikuwa kimoja tu chenye kutoa shahada ya kwanza. Mjini kuzuri jamani tuiendeleze TZ yetu namtumbo nako kuwe town watu wasikimbilie huku tu maana sasa ukifika mlandizi ndo ushafika dar wakati enzi za 80's bango la 'SASA UNAINGIA DAR' Lilikuwa hapo ubungo. TZ after 50 years! Ila tumetoka mbali wajemeni.
 
tathmini yangu ya haraka haraka watu waliokuja dar es salaam wengi wao wamepiga bao kimaisha kuliko wazawa!
 
Mi bado nipo kijijini ila naenda dar kuwatembelea wakwe zangu, wanahishi huko
 
Mimi nimezaliwa Ocean Road, Aga Khan Hospital..

Mita mia karibia na Ikulu, mita mia karibia na bahari, mita mia karibia na uwanja wa gofu..

Tukitoka Dar tunaenda Ulaya na Marekani then tunarudi tena hapa hapa Dar...karibuni sana wakuja
 
Teteteee, kumbe ndipo walipokuFYATULIA................ hihiiiiii......

Mie nilipotea kwenye TRAIN na kuja kuibukia Dar. Kwa bahati wakaniokota na kunirudisha Shamba Sikonge.

Huwa narudi kwa nadra sana hapo Dar maana naogopa wingi wa magari.

Mi nimejikuta nipo Dar baada ya manesi kumwambia b.mkubwa push push push,kidume nipo Dar mishe zote Dar,nitazikwa Dar,karibuni wagilagila wakuja,ukiwa mgeni unafanikiwa Dar lakn hunizid.
 
Teteteee, kumbe ndipo walipokuFYATULIA................ hihiiiiii......

Mie nilipotea kwenye TRAIN na kuja kuibukia Dar. Kwa bahati wakaniokota na kunirudisha Shamba Sikonge.

Huwa narudi kwa nadra sana hapo Dar maana naogopa wingi wa magari.

Wewe wamekufyatulia wapi Mkuu? sikonge au Tabora mjini mitaa ya Bachu au Mwanaisungu, au Ng'ambo?
 
Hahahaaa, wee sema umefyatuliwa Wodi namba ngapi? Unajua manesi wa Dar walivyo wakorofi? Sijui matusi aliyoyapata mama wakati unafyatulia..... "Wanaume basi tena? You will be back Honey........."

Ila hujatuambia Wazazi waliku-CONCEIVE wapi? Kwenye Kivuko kwenda Chuo Cha CCM Kigamboni au Chuoni penyewe?

Au ndiyo ile mitaa ya HQ za CCM pale Mnazimmoja? Pole sana maana Lowassa kashauza hilo jengo ulipoanzia maisha.

Mie wa shamba hata sijui maana si unafahamu Shamba kila kitu ni TABU. Huwezi kuambiwa hata jina la MAMA/BABA. Ndiyo maana ukienda shule unasikia UNENE UBABA nyingi sana maana ukiulizwa jina lako unajibu (Unene - yaani MIMI) na jina la baba unajibu (Uvava).

Alitokea kijana akawa anaitwa Seleman VAVAVA kwani jina la baba alijibu ni BABA.

Mitaa ya Sikonge huko ndaaani kabisa, unaenda hadi Chabutwa na ukifika pale unashuka na kutembea kilomoita kama 5 ndani huko hata barabara hamna zaidi ya Punda na hapo kuna kitongoji kinaitwa NKEKI. Probably nilizaliwa hapo kama mama aliwahi maana vinginevyo, wengi huwa wanazaliwa shamba, kwenye kuchuma uyoga au kukata kuni.
Wewe wamekufyatulia wapi Mkuu? sikonge au Tabora mjini mitaa ya Bachu au Mwanaisungu, au Ng'ambo?
 
Back
Top Bottom