Huyu ndiye Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, Rais ajaye wa IPU na miujiza aliyotendewa na Mungu wake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Mpaka muda huu pasipo hofu wala mashaka unaweza ukasema bila kusita wala wasiwasi kuwa Dr Tulia ndiye Rais ajaye wa umoja wa mabunge Duniani yaani IPU.Hii ni kutokana na uungwaji mkono uliopo kwa Dr Tulia kutoka kila kona ya Dunia, ushawishi wa Tanzania kimataifa,kukubalika kwa Dr Tulia dhidi ya wagombea wenzake,uwezo mkubwa wa kiuongozi alio nao na aliouonyesha Dr Tulia katika maeneo mbalimbali,Heshima na Taswira nzuri iliyonayo Tanzania katika anga la kimataifa pamoja na historia yetu ya kuongoza Taasisi mbalimbali za kimataifa kama ambavyo tumewahi kufanya katika umoja wa mataifa kupitia watu kama akina Dr Asha Rose migiro,Salim Ahmed Salim,marehemu Agustino Mahiga prof Anna Tibaijuka na wengine wengi tu.

Kitaaluma Dr Tulia ni mwanasheria na wakili ambaye pia amekuwa mwalimu ambaye amefundisha sheria kwa muda mrefu katika chuo kikuu cha Dar es salaam yaani udsm pamoja na shule ya sheria,Ndio maana mimi hapa jukwaani hupenda kumwita mwalimu wa waalimu wa sheria na wakili wa mawakili. Ni kiongozi mwenye shahada ya uzamivu yaani PHD kutoka chuo kikuu cha cape Town nchini Afrika kusini,ambapo shahada ya kwanza na ya pili alizipatia kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam.,huku Elimu ya sekondari akisoma shule za wasichana loleza na zanaki.

Dr Tulia amewahi kuwa Naibu mwanasheria mkuu wa serikali nafasi aliyoteuliwa na mh Dr Jakaya Mrisho Kikwete. Dr Tulia ni kiongozi mwenye maajabu yake na aliyeona na kushuhudia miujiza ya kipekee sana Aliyotendewa na Mwenyezi Mungu. Naita miujiza kwasababu zifuatazo.

Licha ya uwezo wake mkubwa kiuongozi,uchapa kazi wake,umahiri wake katika kujenga hoja na kupangua hoja kwa hoja,Elimu yake kubwa na Taaluma yake ya sheria aliyo nayo ni lazima utakubaliana nami kuwa Ni kwa Neema na mipango ya Mungu katika kumuinua Dr Tulia na kumuweka hapo juu alipofika leo hii kuongoza mhimili wa Bunge.

Embu jiulize mtanzania mwenzangu namna Dr Tulia alivyopaa na kukwea ngazi haraka haraka kila eneo alipopita, jiulize kabla ya kuwa naibu mwanasheria Mkuu wa serikali ni wangapi walikuwa na PHD za sheria? Walimu wake wangapi waliomfundisha wangeweza kupewa nafasi hiyo? Wangapi waliokuwa katika ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali wangeweza kupewa nafasi hiyo? Kwanini Akapewa yeye? Kwanini akaaminiwa yeye tu? Vipi kuhusu uteuzi wake wa ubunge kutoka kwa Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli? Nani alitegemea uteuzi ule? Nani aliwaza? Nani alijuwa atakuwa naibu speaker?wangapi walikuwa wana sifa ya kushika nafasi hiyo? Wangapi walikuwa wameshika nafasi za ubunge kwa muda mrefu hadi uenyekiti wa bunge? Kwanini waliachwa na akateuliwa Dr Tulia? Vipi kuhusu u speaker? Nani alijuwa kabla ya 2025 Dr Tulia angeukwaa na kuwa speaker wa Bunge? Wangapi walikuwa na uzoefu na sifa za kuwa ma speaker? Wangapi walichukua Fomu? Mlisoma uzito wa wasifu au CV zao? Kwanini iwe Dr Tulia?

Jibu ni kuwa ni kwa Neema tu ya Mungu na siyo kwa uwezo au ujanja wa Dr Tulia uliomfikisha hapo alipofika kiuongozi. Ni mipango ya Mungu ndivyo ilipangwa iwe hivyo Tokea akiwa Tumboni mwa mama yake,Ndivyo Agano la Mungu lilivyokuwa katika ulimwengu wa kiroho katika uumbaji wake kumfikisha hapo alipo. Dr Tulia ni mpango wa Mungu,Ni Mungu ambaye amempatia njia na maarifa.ni Mungu ndiye aliyempa kibali cha uongozi na kupitisha katika mikono ya wanadamu ili Agano lake litimie.ikumbukwe ya kuwa Mungu hutenda miujiza kupitia watu na watu hao ndio wamekuwa wakimteua katika nafasi mbalimbali na kumchagua kuwa kiongozi.

Mungu hutumia watu kuokoa watu wake,Kusaidia watu wake,kuponya watu wake,kuvusha watu wake na kuwainua watu wake. Mungu anaweza Muinua mtu au kumdondosha mtu kwa kutumia watu. Anaweza kumpa mtu upofu wa kimaarifa na kiakili asione kitu na kuwaza kitu ili achukiwe na watu na mwisho kuangushwa na watu,lakini anaweza Muinua mtu kwa kumpa kibali cha kukubalika mbele za watu na kuungwa mkono na watu wengi. Kwa kila jambo na kila muujiza aufanyao Mungu juu ya mtu fulani hufanya kwa kusudi maalumu,humuinua mtu fulani katikati ya kundi fulani bila kujali hali yake au kipato chake ili akatimize kazi fulani aliyopanga na kukusudia kwa ajili ya watu wake.

Hivyo Naamini Mungu ayemuinua Dr Tulia kumfikisha hapo alipofika kiuongozi anakwenda kumshindia vita hii ya kinyang'anyiro cha Urais wa umoja wa mabunge Duniani,kwa kuwa uwezo anao,.Kama Taifa Tuendelee kusimama upande wa Dr Tulia pasipo kujali itikadi zetu za kisiasa ,kwa kuwa Dr Tulia haendi kuwakilisha chama bali Taifa letu. Akishinda Dr Tulia tuna kuwa tumeshinda sote watanzania kwa pamoja kama Taifa na heshima tutapata Taifa letu na fursa mbalimbali za Sauti ya watanzania kusikika kimataifa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
man-driving-at-afraid-of-truck-ahead-dog-not-worried-at-all.jpg
 
Nikushauri kitu Kaka,,,kuweka mawasiliano yako si dhambi Lakini ombi langu kwako,,hayo mawasiliano embu jaribu kubadilisha weka mawasiliano ya mitandao mingine au la weka ya huo huo mtandao lakini namba tofauti,,hii ya sasa ina kamkosi umeitumia Sana lakini Wapi,,sifa nyingi Kwa viongozi lakini mkeka ukitoka Lucas Mashambwa holaa!!fanyia kazi wazo lango kama hutojali!!
 
Nikushauri kitu Kaka,,,kuweka mawasiliano yako si dhambi Lakini ombi langu kwako,,hayo mawasiliano embu jaribu kubadilisha weka mawasiliano ya mitandao mingine au la weka ya huo huo mtandao lakini namba tofauti,,hii ya sasa ina kamkosi umeitumia Sana lakini Wapi,,sifa nyingi Kwa viongozi lakini mkeka ukitoka Lucas Mashambwa holaa!!fanyia kazi wazo lango kama hutojali!!
Hapana mimi sitafuti uteuzi hapa jukwaani
 
Cjasoma bandiko lote ila wew una tia aibu unajikomba hadi kwa wanawake ..... na utabaki hivyo hivyo ..... utabaki kuwa chawa with zero brain
 
Back
Top Bottom