Rais Samia na Dkt. Tulia wajengewe sanamu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Mtakubaliana nami kuwa Rais Samia na Dr Tulia wanastahili heshima ya kipekee kupewa na kutambuliwa na Taifa letu kwa kujengewa sanamu zitakazoishi miaka na miaka na kubakia kama alama na kumbukumbu kwa vizazi na vizazi, juu ya historia kubwa na ya kipekee waliyoiandika katika Taifa letu na Dunia nzima kwa ujumla wake pamoja na mchango na heshima waliyolipatia Taifa letu. Watu wenye kuelewa na kuthamini michango na heshima ya watu hufanya haya kwa kuwajengea sanamu watu wanaoona wanastahili heshima hii.

Ndio maana ukienda uingereza katika uwanja wa old Trafford unaikuta sanamu ya sr Alex Ferguson kocha aliyeifundisha Manchester United kwa takribani miaka 26 na kuipatia mafanikio mengi na mataji mengi tu,lakini pia kuna sanamu kule india ya Christiano Ronaldo aliyecheza kwa mafanikio makubwa sana na mchezaji bora wa Dunia kwa nyakati tofauti,ukienda Afrika kusini katika mji wa Pretoria unaikuta Sanamu ya Hayati Nelson Mandela.

Ni vipi Watanzania tushindwe kutambua mchango wa Rais samia kiongozi aliyeliheshimisha Taifa letu,Taifa ambalo kwa sasa sauti yake inasikika na kusikilizwa kila kona ya Dunia,sauti inayofunguliwa milango yote ya ulimwengu huu,kiongozi aliyeleta mapinduzi katika kila Secta kuanzia elimu,afya, miundombinu, usambazaji wa maji safi na salama,uchumi,ajira, diplomasia,utawala bora na kujenga umoja wa kitaifa? Utaanzia wapi kusema hastahili wakati unaona namna alivyojenga uchumi unaogusa maisha ya kila mtanzania mwenye kufanya kazi kwa bidii na kujituma? Unaanzia wapi kusema hastahili mama aliyetufanya leo watanzania tutembee vifua mbele popote pale Duniani?

Pamoja na uwezo mkubwa wa Dr Tulia lakini ni nguvu ,ushawishi ,kusikilizwa na kupendwa na kupendwa kwa Rais samia na viongozi mbalimbali Duniani kote kulikompatia ushindi Dada yetu fahari ya nyanda za juu kusini na Nembo ya Mbeya Dr Tulia Acksoni mwansasu,baada ya serikali zao kukubali maombi ya Rais samia ya kumuunga mkono mwanae Dr Tulia na kuomba wampigie kura za ndio.

Dr Samia Suluhu Hasssan anastahili kujengewa Sanamu katikati ya jiji la Dar es salaam ambalo litaonekana kila kona ya jiji letu na kila mgeni akifika jijini atasimama kulitazama na kupata tabasamu kuwa Tanzania imepata bahati ya kuwa na Rais huyu mwanamke na mama wa shoka na aliyemadhubuti na imara kama simba awapo mbugani.

Leo Dr Tulia amekuwa Rais wa kwanza mwanamke kutoka Barani Afrika kuongoza umoja wa mabunge Duniani na mwanamke wa Tatu tangia kuanzishwa kwa umoja huo.je hatuoni hii ni heshima kubwa aliyolipatia Taifa letu? Hatuoni kuwa anastahili kujengewa Sanamu pale katikati ya jiji la Mbeya? Sanamu itakayotoa na kuleta hamasa ,morali na nguvu kwa watoto wa kike na wasichana kuinua matumaini yao na kuona kuwa kumbe inawezekana kuwa yeyote yule katika ulimwengu huu ikiwa utafanya bidii?sanamu itayowapa nguvu wanafunzi wa kike mkoani Mbeya na Tanzania nzima kwa ujumla wake kuona kuwa kumbe wanaweza kutimiza na kufikia ndoto zao na kufika alipofika Dada yao Dr Tulia?

Mtanzania gani amewahi kuwa Rais wa IPU? Kwanini tusione Dr Tulia anastahili heshima hii? Kwa umri wake mtanzania gani amewahi kupata ushindi wa kishindo na kukwea kimadaraka kama Dr Tulia? Kwanini tusione anastahili kujengewa Sanamu ili kila mtoto wa kike akiinua macho yake na kuitazama sanamu hiyo ajipige kifuani mara tatu kijasiri na kusema kuwa hata kama natoka familia maskini na wazazi wangu hawajiwezi lakini nataka kuwa kama Dr Tulia na kutimiza ndoto zangu?

Leo ni kwa ushawishi wa Dr Tulia kwa Serikali yetu tunaona Mbeya inakwenda kujengwa Barabara za njia nne kutoka igawa Mbeya hadi Tunduma mkoani Songwe,ni kwa uwepo wa Dr Tulia tumeona akijenga mabweni shule ya Samora mkoani Mbeya,kusaidia vikundi vya vijana na akina mama kwa kuwapatia mitaji, bodaboda na bajaji kwa vijana ambapo sasa wanajipatia pesa,ni Dr Tulia amekuwa akisaidia sana na kuwa karibu na wazee pamoja na wengi wasio jiweza na kuwapa misaada ya hali na mali.

Nashauri pia kwa chochote kitakachojengwa mkoani Mbeya kuanzia sasa kati ya shule au kituo cha afya au barabara kipewe jina la Dr Tulia,lakini pia viongozi wa serikali za mitaa mnaweza kumzawadia mtaa mmoja ukaitwa mtaa wa Dr Tulia kama sehemu ya kumpa heshima Dr Tulia na kutambua mchango wake katika mkoa wa mbeya na Taifa zima kwa ujumla wake.Dr Tulia ni fahari yetu wana nyanda za juu kusini na Nembo ya wana Mbeya, Tuendelee kumuombea na kumtia moyo katika majukumu yake ya kitaifa na kimataifa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,
Nilishakushauri, kunyamaza mara nyingine ni kuficha ujinga. Ulishaanza kujikomba kwa Makonda, ambae sidhani kama atamaliza mwezi kwenye hiyo nafasi yake mpya bila kutimuliwa. Tulia anavyoliongoza bunge kiasi cha kulifanya lisiwe na tija kwa wananchi bado unakomaa nae apewe maua. Kwa lipi la maana alilolifanyia taifa hili yeye kama spika?
 
Nilishakushauri, kunyamaza mara nyingine ni kuficha ujinga. Ulishaanza kujikomba kwa Makonda, ambae sidhani kama atamaliza mwezi kwenye hiyo nafasi yake mpya bila kutimuliwa. Tulia anavyoliongoza bunge kiasi cha kulifanya lisiwe na tija kwa wananchi bado unakomaa nae apewe maua. Kwa lipi la maana alilolifanyia taifa hili yeye kama spika?
Tulia mwenyewe anajua jamii haimkubali hata kidogo sababu ya kutokujali maslahi ya wanananchi
 
Hio Nishati (Umeme) wa kujenga vitu au gharama za materials zitatoka wapi ? (Kila kitu bei Juu)...., Anyway wataenda kukopa na kuomba hilo ndio wanaloweza...
 
Tulia mwenyewe anajua jamii haimkubali hata kidogo sababu ya kutokujali maslahi ya wanananchi
Dr Tulia anakubalika sana na wananchi na ndio maana Anaendelea kupata baraka na kubarikiwa kutokana na maombi mazuri anayoendelea kuombewa kutoka kila sehemu ya Taifa letu.kwa kuwa ni kupitia yeye kuna wananchi wengi sana wamesaidiwa na kuwezeshwa mitaji.amewapa vijana na akina mama mitaji kupitia vikundi vyao.amesaidia yatima na wajane mbalimbali bila ubaguzi wa aina yoyote ile.
 
We mjinga huna hata baiskel utajulia wapi hizi mambo
Tulia mwenyewe anajua jamii haimkubali hata kidogo sababu ya kutokujali maslahi ya wanananchi
Tulia amepata nafasi ya kuwa Rais wa IPU si kwa Sababu ya umairi wake, kabebwa na jina la nchi baada ya kushindanishwa na wagombea kutoka nchi dhaifu. After all nchi itagain nini kutokana na hicho cheo chake?
 
Back
Top Bottom