Ni nani aliyewahi kuuelewa mziki wa Michael Jackson?

Wewe umezaliwa 2009 unataka kumuelewa msanii ambaye alikuwa anatumbuiza enzi baba yako na mama yako wako vidudu. Huna adabu kabisa wewe mtoto. Tena ukome kama ulivyokoma ziwa la mama yako.

Mwaka 1988 pale Drive in ( kwasasa ni ubalozi wa Marekani) kulikuwa na bonge la screen. Nyimbo ya Michael Jackson, Thriller ilikuwa ndio inawekwa mida ya saa sita usiku. Aiseeee acha wewe mbwa. Yaani sikulala nyumbani siku hiyo nilikojoa kupitia dirishani aisee acha kabisa.

Wewe dogo naomba kwanza ukatubu hii dhambi umetutukania historia yetu kwamba msanii ambaye alikuwa anatusisimua na kututoa machozi leo hii unasema hakuna alilofanya. Wewe mtoto shika adabu yako aiseeee.
 
NImetamani kuandika mambo mengi lkn nilipoona joined 2022 nikaona nitaua mende kwa nyundo huku mimi nikipoteza nguvu nyingi zaidi.
 
Michael Jackson atabaki kuwa extraordinary human being.. Na ni ngumu sana kupata Tena binadamu kama yeye kwa kizazi chetu

Ingawa kama binadamu alikuwa na mapungufu yake n.k lakini kimziki jamaa ni kama Einstein au Tesla kwenye umeme
 
Umesahau ngoma mbili

1. Heal the word
2. Earth Song.

Sauti za humu ndani ni balaa tupu.
 
Umefanya niingie YouTube nisikilize liberian girl kuclear huu upupu wako uliouandika apo juu
 
Dah we nguruwe huu uzi wako umenichefua sana. Maana umekosa adabu kupita maelezo na umetukosea adabu wakubwa.

Ngoja nikuandikie nyimbo hizi kama una bundle nenda YouTube kazitafute utazame video na uhakikishe una music system nzuri au spika nzuri za masikioni.


Tafuta hizi video:


1. Thriller
2. Earth Song
3. Bad (long version)
4. Smooth Criminal
5. Beat it (lomg version)
6. Black or White ( tafuta long version ya huu wimbo pale yule chui mweusi/Black Panther anatoka nakushuka kule chini utamu wa ile video ndio upo kule)
7.You rock my world (Long version)
8. Ghosts (long version)
9. Blood on the dance floor



Tafuta video za live concert za Michael Jackson uone Matusi ya uwezo wake hakuna mtu anamfikia hadi leo hii kwa rekodi shenzi wewe.

Nenda katazame hizo kazi halafu ndio uje kuandika utumbo wako hapa.

Umenikera sana dogo, ungekuwa mbele yangu kwanza ningekuchapa kofi tatu za haraka halafu ningekufukuza.
 
Amenikera sana huyu dogo hadi nimeshindwa kula. Hawa watoto wa miaka 2000 wanadharau sana hawa.
 
Ili upate toba ya kweli, sikiliza huku unasoma lyrics za hizi nyimbo;

Earth song- Uharibifu wa Mazingira, Madhara ya vita, Ubaguzi wa rangi/utumwa.

Gone too soon- Waliotengwa kwa kuugua UKIMWI.

Black or white - Anakemea ubaguzi wa rangi

Another Part of Me - Umoja

Man in the Mirror - Kujitambua (Self-awareness)

The Lost Children- Anaongelea watoto wa mitaani


Alafu ule hizi ngoma:-

This Girl is Mine
Jam
Leave me alone,
Off the Wall,
Pretty Young Thing(PYT)
Rock With You
Speechless
You Rock My World
Who Is It
Butterfly

NB: Ukimaliza uje uombe radhi hapa
 
Plus:

Dirty Diana... Hasahasa album nzima "Thriller" na "Bad".

Hizo album mauzo yake hayajawahi kufikiwa hadi leo.. hasa Thriller ngoma zote kwenye album ni nyundo... enzi hizo unasikiliza side A unaenda side B unarudi side A mwendo kugeuza kanda... Masaa mawili ya hits.
 
Alafu kama watu walikuhadithia kuhusu yeye na kwanini yuko kama alivyokuwa sikiliza huu wimbo wake 'Childhood'

Na malizia kwa kuangalia documentary yakuitwa 'The Killing of Michael Jackson'
 
Una miaka mingapi?
 
Mzee, acha kabisa! Sasa kijana wetu huyu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…