Ni nani aliyemtuma Prof. Mruma na ni lini?

Ni nani aliyemtuma Prof. Mruma na ni lini?

ba60d06e23f4a85fce56fbcb665afaa1.jpg


Natafakari hapa nimekosa jibu.

Hivi!!!! Aliyemtuma Prof. Mruma Wizarani kuchunguza wizi wa madini yetu ni nani? Na ni lini alitumwa?

Nachoelewa kwenye secta/ Wizara ya madini Tanzania, Mruma hajaingia leo wala jana. Amekuwepo kitambo sana. Sasa inakuaje leo Magufuli ajitamba na kumkingia kifua kuwa alimtuma yeye?

Basi tusema alimtuma kipindi ni waziri. Sasa waziri wa Ujenzi au wa masamaki unahusikanaje na madini?

Dah. Sidhani kama tutafika kwa usanii wa level hii.




[emoji124]‍♂️naenda zimbobo.
Mwelezeni huyo skimmer akatafute wa kuwadanganya haraka!! anataka tu kumsevu tunajua! Hilo ndiyo utawala wa magusheria!! Hata kama alikuwa askari kanzu asingemtaja hadharani. Kwani wako wangapi wanaliojichomeka sekta mbalimbali?
 
Mkuu Alen Kilewela, mtu kuwa shushushu sio lazima awe ni mwajiriwa wa TISS, Mtanzania yoyote aliyeajiriwa popote anaweza kuwa an informer wa jicho la serikali kuhusu kile kinachoendelea ndani ya taasisi hiyo.

Hiyo inawezekana kabisa, he was part and part and parcel ya yote yaliyofanyika, lakini kitendo cha kutoa tip ya kinachoendelea anakua amejiokoa.

Kwenye ile kesi ya uhaini ya mwaka 1984, ilipotajwa mwanzo ilikuwa na washitakiwa 43. Ilipoanza rasmi washitakiwa walibaki 26. Waliokuwa washitakiwa na wahusika wa mpango huo lakini waliamua kutoa ushirikiano na kugeuka ni mashahidi wa serikali kwa kuwasaliti wenzao.

Kitendo cha rais Magufuli kumtaja Mruma kuwa ni snitch ni kitu kibaya sana!.
P.
Mh rais ilibidi atamke vile ili kuweka mambo sawa, ikumbukwe Mruma alishatajwa kwenye ripoti,. Asingetajwa, sidhani kama mh rais angemuongelea.
Mbona wa kwenye makinikia ya dhahabu hatujatajiwa?
 
Akili yako ya kitoto sana. Yan mkosaji anasamahewa pale anapotoaushirikiano!

Hii inaweza kuwa ni sahii kwa upande wa CCM maana ndyo tabia zenu. Mtu akijipendekeza kwa mwenyekit makosa yake mnamfutia akiwa upinzani ndipo mnaasnza kumraftia makosa.

[emoji124]‍♂️naenda zimbobo.
Mjinga ni mtu asiyejua, akishajulishwa na kuelewa, ujinga wake humtoka, hivyo mwanzo nilikuona mjinga kuhusu mashushushu, nikajitolea kukuelimisha tena kwa mifano.

Mjinga anaendeleza ujinga hata baada ya kuelimishwa, huyo sasa sio mjinga tena, huyo sasa ni ...s

Hata kama wewe ni Tiss au ni informer na ulielezwa kuna sifa za kuwa informer ambazo unazijua, na umebaini Mruma hana sifa hizo, naomba kukujulisha kuwa umedanganywa. Anybody can be an informer hadi mkeo!
 
Itakuwa mruma alipandikizwa pale mwadui na utawala wa jk au mkapa,
sasa kwa mda wote ule alikuwa anakusanya data za kutosha kuwajua wezi wetu,
na hata huo mkataba aliosaini wa kutuingiza hasara ya matrilioni ilibidi asaini ilki kuweza kupata data kamili za namna wizi unavyofanyika ili vizazi vyetu vijavyo vije kujifunza na kuepuka hizo mbinu ovu,

mimi kinachonichanganya kuhusu huyu mruma,

mbona ana pua imechongoka?
 
Hiyo yote ni ndugu Yohana kujaribu kuficha makosa yake ya kumteua mtu anayenuka kuchunguza uozo mwingine! Its pure bullsh¡t!
 
Walibadili lini makompyuta yao yote??, na walifyonzaje data zao zote???

Wangetueleza wazi siye wananchi tunaochelewa kuelewa....ingefaa sana
 
Mleta hoja usiuumize na kuuchosha sana ubongo wako kuhusu huyu prof. Ukiisoma ripoti yake ya makinikia, ripori ya bunge na kulinganisha na sifa alizopewa jana utauona weupe wake.
Inawezekanaje kutia sahihi mkataba uliowezesha mali ya matrilioni ya shilingi kutoroshwa na nchi kupata hasara na leo usifiwe kwa kazi nzuri? Usisahau ripoti yake ya makinikia iliangukia pua na kuibua msamiati wa uzalendo uliosambaa kwa kasi.
Sisi wanasayansi tunaamini kuwa tafiti hupingwa kwa tafiti. Na tafiti ya makinikia imepingwa na ripoti ya bunge na ambayo ni valid kwa sasa.
Hivyo kitendo cha prof kuhudumu eneo la almasi kwa zaidi ya miongo miwili na ripoti ya bunge kuelezea kasoro na hasara walisosababisha waliokuwa hapo siioni sababu ya yeye kuendelea kuhudumu kwenye utumishi wa umma.
Kwa busara yake angeondoka kama kina simbachawene ili kuiondoa sintofahamu hii.
Labda mimi sielewi, hivi agent hutumwa kuharibu zaidi kile kilichoharibika au kukiokoa kisiharibike zaidi? Naogopa marisasi 22- 28!
 
Lazima kwanza kuwe na "mission" na "Target" na hapo ni lazima tuambiwe wakati Mruma alipoacha kusoma mapendekezo toka kwa wasaidizi wake alikuwa kwenye hiyo "mission" na "target" ya kutokusoma hayo mapendekezo ilikuwa nini?
Mkuu Allen Kilewella, naendelea kusisitiza, anybody can be an informer. An informer ni jicho tuu la serikali kwenye taasisi husika, hivyo anaweza kuwa kuanzia mfagiaji, messenger, mpika chai, Secretary, dereva, etc.

Wanaopewa missions na targets ni ma agents. Not everyone can be an agent.
 
Mkuu Allen Kilewella, naendelea kusisitiza, anybody can be an informer.
Nakubaliana na wewe kabisa kwamba mtu yeyote anaweza kuwa "informer", lakini hoja yangu hapa ni kwamba wakati Mruma anakosea alikuwa ametumwa kukosea? Kutokusoma kwake mapendekezo toka kwa waliokuwa wasaidizi wake ilikuwa ni sehemu ya huo u-informer wake?

Hata kumtumia mtu kutoa habari ni lazima kuwe na "mission" na "target"
 
Nataman sana kucomment hapa....ila jana nimekutana na watu wasiojulikana basi nikaona isiwe taabu....nikajifanya na mimi ni mtu nisiyejulikana nikaendelea na safari zangu.....bottom line....this was the most expensive mission....kwa jinsi ilivocost taifa pesa nyingi in the process ya kudukua na kukusanya ushahidi kwa miongo miwili.

Nawaza tu sina maana yoyote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom