Ripoti ya makinikia ya Almasi na biashara ya Tanzanite yawasilishwa. Prof. Mruma, Maswi na Muhongo washutumiwa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Leo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anapokea taarifa za kamati mbili zilizoundwa na Bunge kuhusu makinikia ya Almasi na biashara ya Tanzanite.

-Ripoti hizo zitapokelewa na spika kisha yeye atamkabidhi Waziri Mkuu.

-----------

Anaewasilisha ripoti hii ni mbunge wa Ilala, Musa Azan Zungu na anaongelea kamati iliyoyabaini ikiwemo kutowajika kwa mamlaka zinazohusika na almasi na Tanzanite ikiwemo NEMC na wizara ya nishati na madini.

Kamati ilibaini kutolipwa kwa income tax ikiwa kinyume na kifungu cha kodi kinacholazimisha kampuni za madini kulipa kodi. Kampuni ya Williamson haijalipa income tax kutoka 2007 mpaka 2017 kwa kisingizio cha kupata hasara.

Mapato stahiki nchi inatakiwa kupata ni kodi kwani mrahaba ni kiasi kidogo ambacho huwa ni fidia. Kuna mkanganyiko wa takwimu kwenye mauzo ya almasi. Kuna takwimu zinazokinzana ambapo nishati na madini na wakala wa madini(TIMA) umebaini kutofautiana kwa takwimu kutoka taasisi hizo mbili za serikali.
  • Kamati imebaini kwenye vyumba ambavyo Almasi huwa inahifadhiwa, kuna milango ya dharura ambayo hutumiwa vibaya.
  • Serikali inapata hasara kubwa kutokana na usafishaji wa Almasi nje ya nchi ambao hudaiwa kuwa inapungua thamani.
  • Kamati imeona kuna haja usafishaji wa mwisho wa madini ya Almasi ufanyike hapa nchini kwani haihitaji uwekezaji mkubwa.
  • Kutokana na kukosa mapato stahiki, kuna haja ya Serikali kupitia misamaha yote ya kodi ya madini ya Almasi hapa nchini.
  • Thamani ya Madini ya Almasi yanayouzwa nje ya nchi ni kubwa zaidi ukilinganisha na kodi inayolipwa hapa nchini.
  • Kwa maoni ya kamati kwa uamuzi wa serikali kutoinunua Petra kwa dola milioni 10 umesababisha hasara kwa sababu kwa sababu mgodi umezalisha almasi zenye thamani ya dola milioni 343. De Beers waliuza hisa bila kufata utaratibu, kamati ikiongozwa na waziri wa wakati huo, Ngonyani walitoa ushauri usinunuliwe.
  • Viongozi wa serikali waliopendekeza mgodi usinunuliwe ndio waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bodi.
Kamati ilipowahoji wajumbe wa bodi, Professa Jairo na Prof Mruma chini ya kiapo, Prof Mruma aliiambia kamati alishindwa kufuatilia madeni(Akiwa mwenyekiti wa audit commitee ya mgodi) kwa sababu hakuwa na muda wa kusoma na aliawaamini waliompelekea taarifa hizo baada ya kamati kumuhoji madeni yaliyobambikwa kwa serikali yamekuwa ni mengi mno.

Kamati ilimuhoji mheshimiwa Maswi ambaye alikuwa Katibu Mkuu na ni mmoja aliyetia saini mkataba ambao Kamati inaona una utata, alijibu hata yeye aliona kilichofanyika ni upuuzi mtupu na alienda mara moja Tanzanite one na alichukia na kutorudi tena ilhali akiwa ndie msimamizi wa Wizara.
  • Kamati imebaini kuna zawadi ilitolewa kwa kiongozi mmoja mkubwa, zawadi hio ya almasi kwa sasa inakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 200.
  • Makinikia yaliyobakiwa yanakadiriwa kuwa na thamani inayokadiriwa kuwa trilioni 2.3. Kamati inahoji mbona taarifa haikutolewa na yalichimbwa na marehemu Wilamson miaka ya 50? Wataalam wahakikishe gharama za makinikia hayo hazijumuishwi kwenye gharama za mgodi.
  • Inasikitisha kuona watumishi wa serikali hawajui kinachoendelea kwenye makampuni ambayo walipaswa kuyasimamia.
  • Zungu amempongeza Rais Magufuli kwa kuliamsha dude na wao wanaendelea nalo.
Waliofata kuongea baada ya kuwasilishwa ripoti zote mbili ni mwenyekiti wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe kisha spika wa bunge, Job Ndungai na kumaliziwa na waziri mkuu, Kassim Majaliwa.

-------

Waziri mkuu amesema yapo makampuni kumi ambayo yameonyesha nia ya kujenga mtambo wa kuchenjua mchanga wa makinikia. Amezishukuru kamati ya bunge na kusema serikali ina nia ya dhati na haitafanya mchezo kuona rasilimali husika zinalinufaisha taifa.

Majaliwa kasema hata maamuzi watakayoyafanya yatakuwa yenye tija kwa Tanzania. Taarifa alizopokea, ushauri na udhaifu uliotolewa ni maeneo ambayo wakati wote wamekuwa wakiyapigia kelele.

Kassim Majaliwa: Pamoja na mamlaka niliyonayo ya kuchukua hatua, naheshimu sheria na kesho asubuhi nitampelekea mheshiwa Rais na kesho nakuomba mheshimiwa spika twende wote, acha nikawasiliane na kiongozi mkuu wa nchi, baada ya hapo mtapata mrejesho.

Leo waziri mkuu, Kassim Majaliwa anapokea taarifa za kamati mbili zilizoundwa na Bunge kuhusu makinikia ya Almasi na biashara ya Tanzanite.

-Ripoti hizo zitapokelewa na spika kisha yeye atamkabidhi waziri mkuu.

hizi siasa sasa ivi raia hawashoboki ripoti ikija inakuja kwa mbwembwe watu wakitoa fact kuwa ripoti ni ya uongo mnajificha hamrudi na feedback , izo ripoti bora ziwe kimya kimya tu
 
Leo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anapokea taarifa za kamati mbili zilizoundwa na Bunge kuhusu makinikia ya Almasi na biashara ya Tanzanite.

-Ripoti hizo zitapokelewa na spika kisha yeye atamkabidhi Waziri Mkuu.

-----------

Anaewasilisha ripoti hii ni mbunge wa Ilala, Musa Azan Zungu na anaongelea kamati iliyoyabaini ikiwemo kutowajika kwa mamlaka zinazohusika na almasi na Tanzanite ikiwemo NEMC na wizara ya nishati na madini.

Kamati ilibaini kutolipwa kwa income tax ikiwa kinyume na kifungu cha kodi kinacholazimisha kampuni za madini kulipa kodi. Kampuni ya Williamson haijalipa income tax kutoka 2007 mpaka 2017 kwa kisingizio cha kupata hasara.

Mapato stahiki nchi inatakiwa kupata ni kodi kwani mrahaba ni kiasi kidogo ambacho huwa ni fidia. Kuna mkanganyiko wa takwimu kwenye mauzo ya almasi. Kuna takwimu zinazokinzana ambapo nishati na madini na wakala wa madini(TIMA) umebaini kutofautiana kwa takwimu kutoka taasisi hizo mbili za serikali.

SARAKASO ZA CCM
 
Back
Top Bottom