Kama Prof. Mruma ni Mjumbe wa Bodi ya Mgodi wa Mwadui,je alikuwa anajichunguza? Kwa nini asiwe kwenye chain?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
Taarifa zinaonyesha prof Mruma aliwahi au ni mjumbe wa mgodi huu wa mwadui ulioitia hasara serikali

Mjumbe wa Bodi anawajibika kuhakikisha mgodi unafata taratibu zote na bila shaka prof Mruma aliingia kupitia uteuzi wa serikali ili akalinde maslahi ya nchi

Jambo la kushangaza,huyu prof aliyetakiwa ayalinde maslahi ya nchi katika mgodi,ndiye kachaguliwa kuchunguza suala la wizi wa mapato ambalo alitakiwa alizuie hukohuko mgodi ni

Kwa hiyo prof huyu ni "judge in his own cause" maana ilitakiwa mtu independent ,mtu huru aihoji Bodi pamoja na Mruma,cha ajabu,anayetakiwa kuhojiwa,ndiye anajichunguza yeye mwenyewe

Nina imani maamuzi ya kupeleka almasi nje hufanywa na Bodi na Mruma aliwahi/huwa anahudhuria vikao vya Bodi hiyo ambapo wataalamu huwasilisha mbele ya Bodi mchakato mzima wa uchimbaji na thamani ya Madini,na baadae Bodi hupitisha na kusaini kukubali yaliyoelelezwa

Sasa najiuliza,minutes za vikao alivyohudhuria na kusaini bwana Mruma vipo? Aliprotest kama kulikuwa na irregularities? Aliprotest kwa nani?

Nadhani prof Mruma ana maswali mengi ya kutujibu,mengi sana,badala ya karata tatu nani kaona

Bahati mbaya media ya Tanzania ni kama Toto la ndege,"taarifa zao zote ni za fulani kasema"

Hawana muda wa kuchimba kutoka kwa chanzo vyao has a wajumbe wa zamani wa Bodi ili waelezee mchakato wa kufikia maamuzi,thamani ya Almasi na mambo kama hayo,hata ikibidi bila kutaha majina

Waandishi wa habari wamegeuza vichwa vya watanzania kuwa "dustbin" zao kuwalisha mambo ambayo hayajachakatwa,ikiwamo hata kuwasiliana na uongozi wa mgodi

Nadhani majibu yanahitajika.....prof Mruma ulikuwa hapo mwadui na hasara ikatokea mbele ya macho yako,binafsi nadhani una la kujibu pale ambapo minutes za Bodi zenye saini yako zikianza kutolewa kama ushahidi,
 
Hii nchi kumpata ambaye siyo mwizi ni mara chache sana..... Kama haibi huku ataiba kule!!!!
 
Japokuwa Profesa Mruma ni mwizi wa kawaida sana, lakini bado ni mbumbumbu wa ovyo kawaida.
Karani mzuri katika kuifirisi nchi yetu.
Magu anajaribu kumlinda sasa ili kuipa uhalali ile ripoti ya kutungwa ya makinikia ambayo Mruma aliitunga.

Lakini ni suala la muda tu, ipo Siku Magu atamtumbua kwa sababu nyingine nyingine, kama alivyomtumia Profesa Muhongo na mwisho wa siku bado walikosana.

Uhusiano wa Profesa Mruma na Magu ni uhusiano wa kiunafiki, kuunga unga na kulindana tu, na uhusiano wa namna hii, haunaga muda mrefu.
 
time will speak
..........................
 
Hii nchi ili uwe mzalendo ni lazima uongee uongo

Ukiongea ukweli unafuatwa na watu wasiojulikana

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Taarifa zinaonyesha prof Mruma aliwahi au ni mjumbe wa mgodi huu wa mwadui ulioitia hasara serikali

Mjumbe wa Bodi anawajibika kuhakikisha mgodi unafata taratibu zote na bila shaka prof Mruma aliingia kupitia uteuzi wa serikali ili akalinde maslahi ya nchi

Jambo la kushangaza,huyu prof aliyetakiwa ayalinde maslahi ya nchi katika mgodi,ndiye kachaguliwa kuchunguza suala la wizi wa mapato ambalo alitakiwa alizuie hukohuko mgodi ni

Kwa hiyo prof huyu ni "judge in his own cause" maana ilitakiwa mtu independent ,mtu huru aihoji Bodi pamoja na Mruma,cha ajabu,anayetakiwa kuhojiwa,ndiye anajichunguza yeye mwenyewe

Nina imani maamuzi ya kupeleka almasi nje hufanywa na Bodi na Mruma aliwahi/huwa anahudhuria vikao vya Bodi hiyo ambapo wataalamu huwasilisha mbele ya Bodi mchakato mzima wa uchimbaji na thamani ya Madini,na baadae Bodi hupitisha na kusaini kukubali yaliyoelelezwa

Sasa najiuliza,minutes za vikao alivyohudhuria na kusaini bwana Mruma vipo? Aliprotest kama kulikuwa na irregularities? Aliprotest kwa nani?

Nadhani prof Mruma ana maswali mengi ya kutujibu,mengi sana,badala ya karata tatu nani kaona

Bahati mbaya media ya Tanzania ni kama Toto la ndege,"taarifa zao zote ni za fulani kasema"

Hawana muda wa kuchimba kutoka kwa chanzo vyao has a wajumbe wa zamani wa Bodi ili waelezee mchakato wa kufikia maamuzi,thamani ya Almasi na mambo kama hayo,hata ikibidi bila kutaha majina

Waandishi wa habari wamegeuza vichwa vya watanzania kuwa "dustbin" zao kuwalisha mambo ambayo hayajachakatwa,ikiwamo hata kuwasiliana na uongozi wa mgodi

Nadhani majibu yanahitajika.....prof Mruma ulikuwa hapo mwadui na hasara ikatokea mbele ya macho yako,binafsi nadhani una la kujibu pale ambapo minutes za Bodi zenye saini yako zikianza kutolewa kama ushahidi,
Mheshimiwa Bashe: unaona hizi chuki? Ni hawa walibambwa kwa huo wizi wanatoa hoha za chuki kama hizi - hawampendi Mruma kwa vile aliwaumbua, wangependa awe discredited. Kama wanamchukia Prof Mruma, je Rais aliyemtuma? Si wangetaka wamnyonge? Hilo wazo lako la kufuta immunity utakuwa umemhukumu kifo huyo Mnyantuzu mwenziyo. Hivi ulishawahi kumsikia mtu anamwita Nyerere eti ni Rais uchwara? Labda ulikuwa hujazaliwa, ulishawahi kumsikia mtu akimtukana Mkapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua JPM ametuona waTZ kama watoto wadogo tunaobembelezewa pipi!!! Eti baada ya kuona Prof Mruma amehusika kwenye wizi wa mwadui ikiwa ni siku chache tu tangu amsifie huyu Prof na kumpa Uteuzi akatwambia eti aliwekwa bodi ya Mwadui kama Snitcher tu ili agundue kilichokuwa kinafanyika!!!!! Uongo mtupu!!!!
Ingekuwa ni kweli ni Snitcher angelishazuia Wizi huu siku nyingi!! Prof Mruma must be responsible!!!! Awajibishwe!!!
"Aahh Bastola ya nini tena jamani!!!!"
 
Inawezekana kweli Le Prof ni Muajiriwa wa Kitengo cha Watu wasiojulikana lakin upande wa Migodini
 
Back
Top Bottom