JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Sheria ya #UlinziWaData ambayo bado haipo nchini Tanzania ina umuhimu mkubwa kwasababu itasaidia kulinda data za mteja kama zifuatazo;
Majina ya Watu(Wateja kama ni kwenye Kampuni ya biashara), Anuani za Posta na Makazi za Wananchi ambao na Wateja wa Makampuni ya biashara
Barua pepe za watu, hii inajumuisha mawasiliano yote yanayaofanyika kwa njia ya barua pepe na kufanikishwa chini ya uwezeshaji wa mtoa huduma
MTEJA ANA HAKI YA KULINDIWA DATA ZAKE ZA KIBENKI NA AFYA
Sheria ya ulinzi wa data Tanzania inahitajika ili kulinda haki ya kila Mtanzania ya kulindiwa taarifa zake, iliyoidhinishwa katika ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa za Kibenki na miamala yote inayofanyika kupitia Taasisi za Fedha. Sheria ya ulinzi wa data itazitaka Kampuni husika kuhakikisha taarifa za wateja wao zinatunzwa
Taarifa za afya za Watu, taarifa hizi hukusanywa na Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma ya afya pamoja na mashirika yanayotoa Bima za Afya