Dhuluma na wizi unaofanywa na kampuni zinazokopesha bodaboda (pikipiki)

Mzee wa old school

JF-Expert Member
May 16, 2021
585
934
Habari wana jamvi.

Kuna baadhi ya KAMPUNI za kukopesha BODABODA (mkihitaji sana nitaitaja) kuna tabia ya DHULUMA, utapeli au UWIZI naweza sema inafanya kwa vijana wa tanzania. Kila kijana anaye kopa PIKIPIKI kwenye hizo KAMPUNI pale anapo maliza deni, watu 9 kati ya kumi ambao nimekutana nao ndani ya mwezi wanalia PIKIPIKI zao zimeibiwa. Na pia wakati mwingine hat wale waliokaribia kumaliza madeni mathalani mwezi 1 au miwili wanakumbwa na adha ya PIKIPIKI kuibiwa.

PIKIPIKI mkopaji anapochukua inakuwa na GPS, ambayo imewekwa na KAMPUNI. Lakini mteja akitala kujua namna GPRS ilivyo wekwa au mteja aweke mwenyewe, KAMPUNI inakataa inasema mteja anaweza kimbia na chombo, ilihali mteja anawadhamini na pia kaweka rehani baadhi ya mali na pia kuna barua ya serikali ya mtaa..

Kinacho nishangaza said, PIKIPIKI ikipotea ama kuibiwa, masaa 2 mengi ukienda kuitrack hazionekani, na pia ukiwafuata KAMPUNI wanakwambia wewe sio mteja wetu tushamalizana ma wewe.... Ukienda polisi napo hakuna msaada zaidi muwakilishi wa KAMPUNI akipewa wito wa polisi anapiga simu kituoni yanaishia kwenye simu tu na mteja akijitahidi kufuatilia sana.. kauli anazopewa polisi ni sawa sawa na majeruhi aliye gongwa na gari na akasahau kusoma pret namba ya gari iliyo mgonga.

MASWALI YA KUJIULIZA.
* GPS wanaweka KAMPUNI hata mteja hajui, PIKIPIKI inapo ibiwa tu! Dakika chache GPS haisomi.

* Ukitoa taarifa ushirikiano haupati kutoka kwenye KAMPUNI.

* Kwanini wateja wakimaliza mkopo au wanaokaribia kumaliza, asilimia kubwa huibiwa.

* Kwanini polisi hawachukulii seriouse sana malalamiko ya KAMPUNI hiyo ilihali yanatokea mara kwa mara...

Ifike wakati basi hata watu wawe na hofu ya Mungu... Na

pia serikali iwe inafuatilia mienendo ya KAMPUNI inazozisajili na ikitokea ulakini na ikathibitisha inazifungia tu. Maana zinazidi kuongeza umasikini kwa vijana wa Tanzania.

Kwenu ninyi vijana wa Tanzania. Hebu mjitambue.. mkiona sehemu kuna shida, achaneni napo ili washindwe kuendesha biashara wafunge.. hiyo itakuwa fundisho hata kwa KAMPUNI mengine watakuwa waaminifu katika huduma zao. Maana itakuwa katika ikili zao kuwa ukiwa mdhulumati tanzania hufanyi biashara.

Wenu Mzee wa old school, ambaye kwa akili zangu timamu niliyeamua kutumia elimu yangu na maarifa aliyonipa Mungu kusaidia uma wa Watanzania kujitambua.

Cc GENTAMYCINE
Robert Heriel Mtibeli na Watanzania wengine mliopo jamvini na msiokuwepo
 
Hao jamaa skuizi wamekuwa kausha damu aisee Yani masharti kibao kama waganga wa kienyeji na hizo GPS skuizi wanazitoa tu ikiibiwa kule inapoenda wanachezea mfumo wake na GPS inakuwa haifanyi kazi Tena ni sawa na hizi simu za mikopo tu nirahisi sana kuzitoa mifumo yao
 
Habari wana jamvi... Kuna baadhi ya KAMPUNI za kukopesha BODABODA (mkihitaji sana nitaitaja).. kuna tabia ya DHULUMA, utapeli au UWIZI naweza sema inafanya kwa vijana wa tanzania... Kila kijana anaye kopa PIKIPIKI kwenye hizo KAMPUNI pale anapo maliza deni, watu 9 kati ya kumi ambao nimekutana nao ndani ya mwezi wanalia PIKIPIKI zao zimeibiwa.... Na pia wakati mwingine hat wale waliokaribia kumaliza madeni mathalani mwezi 1 au miwili wanakumbwa na adha ya PIKIPIKI kuibiwa.....
Aiseeeh
 
Hao jamaa skuizi wamekuwa kausha damu aisee Yani masharti kibao kama waganga wa kienyeji na hizo GPS skuizi wanazitoa tu ikiibiwa kule inapoenda wanachezea mfumo wake na GPS inakuwa haifanyi kazi Tena ni sawa na hizi simu za mikopo tu nirahisi sana kuzitoa mifumo yao
eeh hebu nimegee hapo kwa simu za mkopo na mpango nao..wapuuz matapeli mbwa.
 
Back
Top Bottom