Ni miaka 60 sasa tangu mchezaji wa mwisho kuhama moja kwa moja kutoka Man Utd kwenda Liverpool

Andre-Pierre

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
328
1,209
Phil Chisnall anabakia katika vitabu vya kumbukumbu kama mchezaji wa mwisho kuhama direct toka Man Utd kwenda Liverpool baada ya hapo haijawahi kutokea tena. Alifanya uhamisho huo mwaka 1964.

Man Utd & Liverpool ni wapinzani kweli katika mpira na uhasama wao ulifanya mechi zao ziwe zinachezwa mchana kweupe waingereza wakiita “lunch time kick off”

Uhasama wao umeendelea kwa kutouziana wachezaji kwa moja kwa moja (direct). Mchezaji akitaka kuchezea upande wa pili wa mpinzani atalazimika kuchezea timu tofauti kati ya hizo kwanza ndo ahamie upande wa pili.
Mfano; Michael Owen alihama Liverpool akaenda Real Madrid kisha Newcastle Utd afu ndo akaenda Man Utd. Hii imemfanya Owen aonekane msaliti.

Uhasama wao umefanya mtoto akizaliwa jijini Liverpool anafundishwa kutokuipenda Man Utd hivyohivyo mtoto akizaliwa jijini Manchester anaambiwa maadui zetu ni Liverpool.

Katika miaka hii 60 ya kutouziana wachezaji, sioni kama rekodi itavunjwa kwa siku za karibuni, sioni kabisa, unaweza ukashangaa miaka 100 inatimia.
 
Nakumbuka kuna mchezaji wa man u alitaka kwenda liver mzee Ferguson akamwambia unajisumbua bure huko huwezi kwenda ukitokea huku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom