Makala: Usajili wa Coutinho ni taa ya kijani kwa nyota wengine wa EPL

PITCOL

Senior Member
Aug 8, 2017
128
66
Football Events7910:_______Makala NO-81:_______Jan 2018:____{1/1}:

USAJILI WA COUTINHO NI TAA YA KIJANI KWA NYOTA WENGINE WA EPL


Ni vigumu sana kushindana na moyo hasa unapopenda kitu. Muda mwingine unaweza usiwe kabisa na ndoto ya kitu flani lakini ghafla kile kitu kinapoonesha kukubali nawe unakwenda huko. Ghafla mapenzi ya kile kitu yanakuja na sasa wewe mwenyewe unaweka ahadi ya lazima kile kitu kuwa nacho au kukipata na kuwa sehemu ya maisha yako kwa njia yoyote hile.Hapo ndipo pengine mapenzi yana nguvu kuzidi unachokijua.

Usajili wa kiungo mshambuliaji Philippe Coutinho kutoka kwa majogoo wa jiji (Liverpool) kwenda kwa wakatalunya (FC Barcelona) ni ishara tosha kuwa wachezaji wengi wakubwa wanandoto au wanapenda kuchezea vilabu viwili vikubwa vya nchini Hispania, FC Barcelona na Real Madrid. Coutinho alikuja Liverpool Jan 2013 kutokea Inter Milan kwa ada kiduchu ya £8.3m na sina huakika kama alikuwa na ndoto za kujiunga na miamba hao wa wakatalunya. Achilia kwamba yeye mwenyewe kusema kuwa kwenda Barca ilikuwa ndoto yake.

Ni vigumu kuamini kuwa Liverpool waliamua kumuuza Coutinho katikati ya msimu wakati wakijua fika kuwa msimu bado haujaeleweka. Lakini unaweza pia usiwalaumu sana Liver kwani miezi 6 iliyopita walijitahidi sana kumzuhia na akabaki japo tayari mchezaji mwenyewe alikuwa ameomba kuuzwa kwenda Barca.Ukizingatia pia dili la sasa lilikuwa ni £142m linalomfanya kuwa mchezaji ghali namba 2 kwa sasa duniani na pia pengine kujituma kwa mchezaji kungeshuka hivyo wao wakaamua kumuuza pale ambapo akili yake ilipokuwa.

Nyota wengi wanaocheza ligi ya England wamekuwa ni wahanga wengi wa kunyakuliwa na hawa miamba miwili ya Hispania yani Barca na Real Madrid.Timu za England kwa upande wao imekuwa ni vigumu kuchukua wale nyota wa timu hizo hata pale wanapo toa donge nono.Hii nip engine na timu hizo kuwa tayari zimejitengeneza kama wakubwa na pengine wenye kila kitu kuzidi vilabu vingine barani ulaya na dunia kwa ujumla.

Kama ni suala la pesa basi wachezaji kama Lionel Messi,Sergio Ramos,Sergio Busquet,wangekuwa tayari wako England.Luis Suarez,Ronaldo pamoja na Gareth Bale tayari wangekuwa wamerudi England. Lakini mwisho wa siku wao wanaona pengine kuviacha vilabu hivyo hasa wakati bado wanawahitaji ni kama kurudi hatua moja nyuma.Hii inaamua wao
kuendelea kubaki katika timu hizo yani mpaka pale ambapo wamechuja au wameshindwa kufanya kilicho waleta.

Wachezaji wengi wanaokwenda ligi ya England wakitoka ligi ya Hispania (La Liga) hasa vilabu vya Barca na Real Madrid hawatakiwi tena na vilabu hivyo. Mfano wachezezaji kama Alexis Sanchez,Mesut Ozil,Yaya Toure,Angel Di Maria na Alvaro Morata walikuwa bado wana viwango lakini walikuwa hawatakiwi tena. Ukweli ni kwamba vilabu vya England kwao imekuwa ni ngumu kuwachukua wachezaji muhimu na wakali kutoka vilabu hivyo viwili.

Wachezaji wakali wa EPL kutoka La Liga wengi wao wamekuwa wakitoka vilabu kama Valencia,Sevilla,Villarreal Atletico Madrid kwani hawa wana njaa na bado wanazidiwa sana na ile top 4,5,6 ya England. Mfano David Silva,Nicolas Otamendi,David De Gea,Juan Mata,Eric Bailly, Fernando Torres wote hawa wametoka vilabu tofauti na Barca & Real Madrid wakiwa ni nyota kwao na kwenda kuwasha moto England.

Mchezaji wa kikosi cha kwanza wa Real Madrid au FC Barcelona kutajwa kutakiwa na vilabu kama Man U, Liverpool, Chelsea, Arsenal na kwasasa Man City wamekuwa wakiona ni kitu cha kawaida kabisa kulinganisha na upande wa pili. Mchezaji yeyote wa kikosi cha kwanza wa timu hizo za England anaposikia jina lake kutakiwa na eidha Barca au Madrid basi wengi wao wanaona ni kupiga hatua kubwa sana kisoka.Hii ni hatari zaidi hasa wale wachezaji wa timu za kawaida kusikia majina yao yanatajwa na hao miamba wa Hispania.

Wachezaji kama Luis Suaez ameondoka England akiwa ni mfungaji bora wa EPL goli 31 mwaka 2014. Cristiano Ronaldo aliondoka England kwenda Hispania akiwa ni mchezaji bora wa dunia (July 2009).Luca Modric(2012), Javier Mascherano(2010) aliondoka England akiwa kiungo bora mkabaji, Xabi Alonso (2009), Gareth Bale (2013), Alex Song (Aug 2012), Cesc Fabregas (2011) aliondoka England akiwa ni kiungo bora kabisa na nahodha wa Arsenal na sasa Philippe Coutinho, hao ni baadhi tu ya wachezaji bora nyota ambao ndani ya mika hii 10 wamehama England na kwenda Hispania wakiwa bado wanatakiwa na timu zao.

Hii ni safari ambayo hatujui mwisho wake ni lini kwani baadhi tu ya nyota wa EPL wameendelea kuachwa tu kucheza katika ligi hiyo yenye wafuatiliaji wengi duniami.Wachezarji kama Eden Hazard, Mo Salah, Harry Kane, Kevin De Bruyne na wengine wameendelea kuachwa tu hapo England kwa sababu wakubwa bado hawajatia nia yao ya kwelikweli kama kwa wengine. Ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa Coutinho angeondoka Liverpool katikati ya msimu lakini tayari kashaondoka Liver. Hii ni ishara tosha kuwa wachezaji wa EPL wanapoona treni ya kwenda Barca au Madrid inawasubiri basi hawana budi kupanda treni hiyo bila kujua kama kuna siti hau hakuna.

Mwisho wa siku ni kwamba nyota hao wanao kipiga katika EPL kabla ya mwaka kugeuka basi kuna mwingine pia atamfuata Philippe Coutinho hasa akienda upande wa pili wamambo. Wachezaji wengi bora wa dunia wamekuwa wakipita La Liga pengine hii ndio imekuwa chachu kubwa kwa wao kuipa mkono wa kwa heri EPL na kutimkia zao La Liga.Hivyo klabu kama Chelsea, Man City, Tottenham na Liverpool tena wajitayarishe kwani kabla ya mwaka kugeuka yatawakuta ya Coutinho.

5a62351488b73186a3000001.jpg

.
. .
.
Makala kama hizi pia unaweza kuziona katika page ya facebook Football Events7910 .
Mawasiliano: +255 657 00 58 77 or +255 763 619 770 or +255 625 76 13 88
Email: ernestmazengo@gmail.com
Prepared By
Mr Mazengo {Football Pundit /Analyst}
 
Asante sana Brother kwa upembuzi yakinifu
Kuna sababu moja kubwa sana ambayo imejificha kuhusu lundo la wachezaji kupenda kuchezea ligi ya Hispania.
Hali ya hewa.
Uingereza inatawaliwa sana na hali ya mvua nyingi na baridi kali. Hii huwashinda sana wachezaji wa Amerika ya kusini na kutundanganya eti ndoto yangu ni kucheza Barca.
Wake pia ni tatizo.Uingereza hawawezi vaa vimini wakatuonyesha mapaja yao, ni jeans na mikoti kwa kwenda mbele.
Pia ligi ya Uingereza ina hitaji intensive physique ambayo wakati mwingine ni kero.Huna mpira lakini unanigwa shingo.Spain watu wanacheza kwa kukaba space sio man to man iliyopo Uingereza.
 
Kuna mambo kadhaa ya kuangalia hapa.
1. Wachezaji wote wanaotoka latin America ndoto yao kubwa ni kucheza spain, ikifatiwa na ureno na italia. Kinachowashawishi ni pamoja na lugha.
2. Mchezaji yeyote ndoto yake ni kuvaa jezi za barca na madrid. Ukifanikiwa kuvaa jezi za club mbili hizi itakuwa ni moja ya njia ya kufikia malengo maana hata ukiachwa lazima utaangukia kqenye vilabu vikubwa kule epl.
3. Madrid, barcelona na Bayern huwa wanaacha wachezaji. Ukiachwa na vilabu hivi ujue haupo kwenye mipango yao.
4. Wachezaji wengi wanaotoka laliga kwenda epl ndio wanaorun priemir league kwa sasa.
5. Hakuna mchezaji yeyote anayeweza kukataa ofa ya madrid na barca achilia mbali Atletico madrid.
 
Wamchukue na David De Gea kama wanaweza.
Kabla ya msimu kuanza de gea alikua tayari anataka kwenda madrid, Man u ndio mlioweka ngumu!..Kutakiwa Real Madrid au Barcelona si mchezo lazima udate!..
Leo hii taarifa zinasema Salah amemwambia agent wake afanye mchakato aende madrid.
 
Back
Top Bottom