Ni lini Tume za Uchunguzi zitakuja na suluhu ya matatizo yanayoikabili Tanzania yetu?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Rais wa awamu tatu Benjamin William Mkapa alipoingia madarakani aliunda tume iliyoongozwa na Jaji Warioba, kuchunguza rushwa na udhibiti wake.

Kila mmoja aliunga mkono dhamira ya dhati ya Ben. Kilichotokea baada ya taarifa za matokeo ya tume hiyo, alihojiwa kwanini amekwenda nje ya hadidu za rejea. Waliotufikisha hapo na hapa waliishia kulindwa kwa heshima zote na kuendelea kula cake ya Taifa mpaka leo.

Matokeo ya taarifa ile ni uanzishwaji dubwasha kubwa la kuzuia rushwa, likiwa limeshindwa kabla halijaanza kazi na mpaka kesho limebaki kuwa eneo la kuwachapia dagaa huku makambale yakiendelea kufurahia Kodi za wajinga.

Si serikali tu hata tume teule za bunge nazo zilikuja na maudhui yanayo fanana kwa taadhira,lakini utekelezaji wa maazimio ya tume hizo, mpaka kesho yataendelea kuiumiza nchi. Mathalani sakata la Richmond kuhusu umeme, pamoja na mvua nyingi na mabwawa kukaa bado umeme wetu ni maamuzi ya wanufaika wachache ndani ya deal Hilo.

Kubwa nalotaka kusemea hii tume ya hivi karibuni ya haki jinai ambayo Rais amepokea taarifa zake Nini impact yake kwa Taifa ikiwa zimewekwa kwenye mashubaka ya Ikulu kama yalivyo makabrasha mengine!

Kwanini serikali haijitathimini kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu unao sababishwa na ukosefu wa haki jinai.

Mhusika mkubwa kama mtuhumiwa ni Jeshi la Polisi ambalo mbali ukosefu wa weredi limejigeuza kuwa Jeshi la kisasi kwa raia wasio na hatia.

Wadau wa utetezi wa haki za binadamu wamependekeza ulazima wa kulifanyia Jeshi reform ili lienda na wakati na liondokane na mfumo wa kikoloni uliolenga kuwatweza watu utu wao kwa malengo yenye maslahi na matakwa ya malkia.

Ni wakati sasa kwa wananchi kuinyooshea serikali kidole kutokana na matumizi mabovu ya fedha za umma kutumika vibaya.

Ajabu hata taarifa ya CAG haizungumzi ubadhilifu wa fedha za umma kupitia tume mbalimbali zinazoundwa bila kuwa na tija kwa Taifa.

Inaaminika wizi wowote ni connection, hata za haya matumizi mabovu ya fedha za umma nayo ni connection ndiyo maana taarifa hizo zinabaki kuwa story tale.

Tuamke kwa maslahi ya umma tuache kuwa washangiliaji wa tume hizi huku tukihalalisha wizi wa fedha zetu wenyewe.
 
Ata wachunzwaje hamna kitu wanaweza kufanywa uchunguzi ukifanyika unàkuta mhusika ni kijana/chawa wa mheshimiwa.

Makonda alikuwa anafanya ufisadi lakini ni kijana wa magu. magu akiletewa ripoti inabidi awe mopole.

Makamba hapo tanesco alifanya ujinga lakini hawezi kuwajibishwa kwasababu kujuana. Tanzania kuendelea ni kazi sana rushwa imetamalaki sana. kwanzia juu mpka chini.
 
Rais wa awamu tatu Benjamin William Mkapa alipoingia madarakani aliunda tume iliyoongozwa na Jaji Warioba, kuchunguza rushwa na udhibiti wake.

Kila mmoja aliunga mkono dhamira ya dhati ya Ben. Kilichotokea baada ya taarifa za matokeo ya tume hiyo, alihojiwa kwanini amekwenda nje ya hadidu za rejea. Waliotufikisha hapo na hapa waliishia kulindwa kwa heshima zote na kuendelea kula cake ya Taifa mpaka leo.
Methali ya FUNUKA KOMBE MWANAHARAMU APITE inakubalika na pia ni applicable in Tanzania only.

Tume zikishateuliwa wanasisitizwa kuhusu huu msemo wa wahenga. Tena wanaambiwa wazi kuwa wamepewa favor kuteuliwa.
 
Lyatonga Mrema alitenguliwa kwa kutoa Siri za Baraza la Mawaziri akiwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu.

Maanake alitoa hadharani Siri ya wizi unaofanywa na kubarikiwa na Baraza la Mawaziri.

Mfumo huo bado unaendelea japo hakuna waziri mwenye gut kama aliyekuwa nayo Mrema,wote wamejikita kulinda ugali wao na wizi wao ndani ya mamlaka yao.
 
Methali ya FUNUKA KOMBE MWANAHARAMU APITE inakubalika na pia ni applicable in Tanzania only.

Tume zikishateuliwa wanasisitizwa kuhusu huu msemo wa wahenga. Tena wanaambiwa wazi kuwa wamepewa favor kuteuliwa.
Tena favor si kwa Taifa ni favor ya mteuzi
 
Ni ngumu hizo tume kuwa na nguvu kwenye mazingira ambayo walengwa ni watu walioko kwenye nafasi zao kwa kujuana. Unakuta rais mwenyewe ambaye ndio namba Moja wa maamuzi anaingia madarakani kwa chaguzi za kihuni, na wanaofanikisha yeye kuingia madarakani ndio hao hao wanakutwa kwenye hizo ripoti za uchafu.
 
Mtihani huu mwenye kusahihisha ni wananchi,hatari wenye nchi wanaogopa mamlaka yao waliyoyatumia kuiweka serikali,bila katiba Bora ya wananchi hata Jeshi la malaika likishuka litakuwa CCM
 
Back
Top Bottom