Ni lazima nafasi nyeti zichukuliwe na "wastaafu"?

Binafsi sijaona udini kwenye uteuzi huu. Naona bwana mkubwa ame-balance vizuri.

Hujaona udini kwa sababu kachaguliwa muislamu mmoja na wengine wote ni wakritso kwako hiyo ndio "ame-balance vizuri" kinyume chake ni udini, it goes without saying wakizidi wakristo balance nzuri lakini wakizidi waislamu udini!

Cha kufurahisha ni mkikosa hoja ya udini mnakimbilia "urafiki" wakiteuliwa wakrsto wengi mnadai "maswahiba" wake anawaweka kwa sababu maalum.

He cant wi,n either way he is in wrong, hapa ndipo mlipomfikisha wadini nyie.
 
Patrick Rutabanzibwa ni mmoja wa Makatibu Wakuu ambao ni bold hakuna mfano. Nakumbuka kipindi cha Mkapa, alikosana na waziri wake wizara fulani, waziri akamshitaki kwa rais kuwa lazima ama waziri aachie ngazi, ama Ruta apigwe chini. Ben alimuhamisha tuu hiyo wizara.Huyu jamaa ni mtu wa principles, mawaziri ni political post, sasa wanapotaka kuleta siasa kwenye utendaji, ukiwatilia ngumu, wanakupigia kelele.Jamaa hajikombi wala kujipendekeza kwa wanasiasa na labda ndio maana ameshindwana na Lau hapo mambo ya ndani.
 
Hakuomba kazi ya kuwa katibu wa kudumu wa Mambo ya ndani kabla yake kuna makatibu watatu wameondolewa.ukiona kaondolewa kachemsha.

Kuna issue ya vitambulisho alitofautiana na waziri wake, Masha. Inawezekana hawaivi.
 
Hongera Bi. Salome Sijaona kwa kustaafu, ....

Hongera ya nini? kwani amejitolea kustaafu? si kwa mujibu wa sheria? hivi huyu si ndiyo yuleyule aliyeimarisha makundi ya rushwa na ufisadi mwingine pale ardhi mpaka Magufuli akachukiwa kwa kuwabana wala rushwa za viwanja na waliofanya double/tripple allocation?
 
Hongera Bi. Salome Sijaona kwa kustaafu, sasa naona kazi ipo huyu Bw. Rutabanzibwa atauza ardhi yetu, tuwe macho.

Amshinde anayeondoka? Yaani huyu mama namshauri asijiingize katika siasa maana watamuanika na akakosa vyote alivyojikusanyia.

Ni ushauri wenye nia njema kwake na kwa watanzania kwa kile alichowabakizia.

Omarilyas
 
Hongera walioula.

Tunataka ari mpya ya kweli sio ya kisiasa

Leka

Sasa kama umemuona "ameula" iweje utegemee vingine tofauti na ulaji na siasa longolongo?

Kwa mitizamo kama hii sio bure wanajiamualia kujikusanyia tu na kuacha kuwatumikia wananchi kama ambavyo wanavyotakiwa.

omarilyas
 
..kuna kipindi watumishi wa wizara ya nishati walikuwa wanaanikana na kulumbana waziwazi ktk magazeti. kuna anayekumbuka walikuwa ni kina nani, na walikuwa wakilumbana kwa masuala gani?

..nahisi kama David Jairo alikuwa miongoni mwa hao waliokuwa wakilumbana and displaying their dirty laundry in the newspapers. kama nimekosea naomba mnisamehe.

..David Jairo wametoka mbali sana na Raisi Kikwete. Jairo alikuwa na JK wizara ya nishati, baadaye JK akamvuta Foreign na siku zote wamekuwa watu wa karibu sana.

..kuna jamaa anaitwa Mtawa nilitarajia ndiyo anaweza kuchukua nafasi ya Jairo. huyo naye ni mtu wa karibu sana kwa JK.

..sasa JK ana mtu wake Nishati na Madini kwa hiyo if anything goes hawezi kukwepa lawama.

NB:

..baada ya Mwanyika, na Mwakapugi kustaafu, Kamati ya Mwakyembe watabaki kulia na Dr.Hosea na Bashir Mrindoko.

..Mrindoko akiwa acting PS wa Nishati ndiye aliyesaini barua ya kusitisha MOU kati ya serikali na Richmond kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta. uamuzi huo ulifikiwa baada ya Richmond kushindwa ku-raise funds kwa ajili ya mradi huo.

..kamati ya Mwakyembe inamlaumu Mrindoko[Kamishna wa Nishati] kwa kutomshauri vizuri Mwakapugi[Katibu Mkuu] kuhusu undani wa kampuni ya Richmond.
 
Patrick Rutabanzibwa ni mmoja wa Makatibu Wakuu ambao ni bold hakuna mfano. Nakumbuka kipindi cha Mkapa, alikosana na waziri wake wizara fulani, waziri akamshitaki kwa rais kuwa lazima ama waziri aachie ngazi, ama Ruta apigwe chini. Ben alimuhamisha tuu hiyo wizara.Huyu jamaa ni mtu wa principles, mawaziri ni political post, sasa wanapotaka kuleta siasa kwenye utendaji, ukiwatilia ngumu, wanakupigia kelele.Jamaa hajikombi wala kujipendekeza kwa wanasiasa na labda ndio maana ameshindwana na Lau hapo mambo ya ndani.
Isije kuwa Ruta ndiye kaleta usiku ktk deal la Vitambulisho!
 
Patrick Rutabanzibwa ni mmoja wa Makatibu Wakuu ambao ni bold hakuna mfano. Nakumbuka kipindi cha Mkapa, alikosana na waziri wake wizara fulani, waziri akamshitaki kwa rais kuwa lazima ama waziri aachie ngazi, ama Ruta apigwe chini. Ben alimuhamisha tuu hiyo wizara.Huyu jamaa ni mtu wa principles, mawaziri ni political post, sasa wanapotaka kuleta siasa kwenye utendaji, ukiwatilia ngumu, wanakupigia kelele.Jamaa hajikombi wala kujipendekeza kwa wanasiasa na labda ndio maana ameshindwana na Lau hapo mambo ya ndani.

kweli nchi inaendeshwa kishkaji...umenikumbusha kitu...!!

waziri masha ameshamlalamikia huyu jamaa kwa rais kuwa hawaheshimu yeye waala naibu wake.....na katika siku za karibuni habari za uhakika walikuwa kama paka na panya.....nadhani jk amechukia kwa nini jamaa hamuheshimu rafiki yake....kaamua kumpeleka dampo ya mahasimu wake wizara ya ardhi akakae pale na waziri magufuli!!

pia natoa pongezi kwa salome sijaona ...kwani ni kati ya makatibu wakuu waadilifu.., ardhi kuna kashfa sana lakini sijapata kumsikia na tatizo pale......na amekaa miaka mingi sana pale....

nafikiri huyu ni yule binti wa Lawi Sijaona!!!.

kudos salome!!
 
Lakini hii ya Ruta na Magufuli wizara moja naona imekaa poa sana, hasa wakatio huu mgumu wa viwanja na mazingira yetu..
 
Mkandara,Philemon Mikael,

..Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu wakati wizara ya Nishati na Madini wakati tunaingia mkataba na Net Group.

..pia nadhani mikataba yote mibovu ya madini, except ule wa Buzwagi, imesainiwa wakati Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini.

..zaidi ile MOU ya kujenga bomba la mafuta Dar--Mwanza kati ya serikali na Richmond ilisainiwa na Rutabanzibwa kwa niaba ya serikali ya Tanzania.

..sasa nini kinachowapa imani kwamba Rutabanzibwa atafanya maajabu huko wizara ya ardhi?
 
Jokakuu,
Nakubaliana nawe kwa kiasi lakini kumbuka pia ni Ruta pia aliyepinga mikataba yote kimaandishi hata nukuu za upinzani wake zimechapishwa na zipo hadi leo hiii.. zinaweza kabisa tumika kortini kama ushahidi. nakumbuka kuna wakati FMES alizzitumia hapa JF ktk sakata la IPTL..
 
Mwakapugi kastaafu? january haijafika bado! hiyo ni janja ya nyani ya kuuzima moto wa richmond scandal unaotarajiwa kulipuka kipindi kijacho cha bunge! Pia JK kashauriwa kufanya hivyo kama kujiosha na hii scandal na hata kama Mwakapugi atapelekwa mahakamani kama mgonja tayari atakuwa ni mstaafu hayuko tena kazini! so watanzani tuwe macho kwa kila move ya kutupiga changa la macho!
 
Mkandara,Philemon Mikael,

..Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu wakati wizara ya Nishati na Madini wakati tunaingia mkataba na Net Group.

..pia nadhani mikataba yote mibovu ya madini, except ule wa Buzwagi, imesainiwa wakati Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini.

..zaidi ile MOU ya kujenga bomba la mafuta Dar--Mwanza kati ya serikali na Richmond ilisainiwa na Rutabanzibwa kwa niaba ya serikali ya Tanzania.

..sasa nini kinachowapa imani kwamba Rutabanzibwa atafanya maajabu huko wizara ya ardhi?
jokaKuu,
Kumbuka kwamba Net Group ilikuwa shinikizo ya Mkapa. Rutabanzibwa asingefua dafu mbele ya rais mbabe!
 
Lakini hii ya Ruta na Magufuli wizara moja naona imekaa poa sana, hasa wakatio huu mgumu wa viwanja na mazingira yetu..

Ardhi ni Chiligati siyo Magufuli. Katika Vitambulisho Ruta na Masha walikuwa upande mmoja dhidi ya Membe na Luhanjo
 
Back
Top Bottom