Ni lazima nafasi nyeti zichukuliwe na "wastaafu"? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lazima nafasi nyeti zichukuliwe na "wastaafu"?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Bill, Oct 19, 2009.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko katika safu ya maofisa waandamizi wa Serikali kwa kuteua Makatibu Wakuu wa Wizara wanne wapya, kuhamisha wengine wawili, na kuteua Katibu wa Rais mpya.

  Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Oktoba 19, 2009, Ikulu, mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Philemon Luhanjo, imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amefanya mabadiliko hayo kufuatia kustaafu kwa baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara.

  Aidha, taarifa inasema kuwa mabadiliko hayo yanaanza leo, Oktoba 19, 2009.

  Taarifa hiyo imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana David Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Jairo alikuwa Katibu wa Rais.

  Bwana Jairo anachukua nafasi ya Bwana Arthur Mwakapungi ambaye amestaafu.

  Katika taarifa yake, Bwana Luhanjo amesema kuwa pia Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sazi Salula kuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Salula alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Taarifa hiyo pia imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Mbarak M. Abdulwakil aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Bwana Abdulwakil anachukua nafasi ya Bwana Patrick Rutabanzibwa ambaye anahamishiwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kama Katibu Mkuu. Ndugu Rutabanzibwa anachukua nafasi iliyoachwa na Bi. Salome Sijaona ambaye amestaafu.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mhe. Rais Kikwete pia amemteua Bwana Christopher N. Sayi kuwa Katibu Mkuu wa Wizata ya Maji na Umwagiliaji.

  Kabla ya uteuzi wake, Bwana Sayi alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo hiyo, na anachukua nafasi ya Bwana Wilson Mukama ambaye ameanza likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.

  Bwana Luhanjo amesema katika taarifa yake kuwa vile vile Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sethi Kamuhanda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

  Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kamuhanda alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Anachukua nafasi Dkt. Florence Turuka ambaye anahamishiwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kama Katibu Mkuu. Bw. Turuka anachukua nafasi ya Dkt. Naomi Katunzi, ambaye anamaliza mkataba wake wa utumishi wa Serikali mwezi ujao, Novemba, 2009.

  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi pia inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mbena alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, na anachukua nafasi ya Bwana Jairo.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  19 Oktoba, 2009  NB: Naomba kuuliza, hivi Arthur Mwakapungi amefikia umri wa kustaafu au ni kwa manufaa ya umma na shinikizo la bunge?
   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ++
  N
  Yaani huyu badala ya kumuondoa na mambo ya Meremeta na vitambulisho anampeleka kwenye viwanja vyetu???? Haa tutasikia bosi wake Masha naye kahamishwa!!!!????
   
 3. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwakapugi ameachiwa mpaka kastaafu.....Sijui naye atafanyiwa kama aliyofanyiwa Mgonja?
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  kuna tofauti kati ya "Florence" Vs "Frolence" .......huyu bwana kule Habari , Utamaduni na Michezo ilikuwa ni kumpotezea muda wake huyu jamaa...........haya sasa wana-SUA.....Prof Msolla na Turuka we want results  Huyu anaitwa Athur Mwakapugi na sio "Mwakapungi", kweli hata mimi nashangaa kusikia eti amefikia umri wa kustaafu..........then kuna watu wengi tu wanahitaji kustaafu.........au ndio yale mambo ya vyeti feki (i.e. vyeti vya kuzaliwa in this case)
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hta mimi nimebaki na mshangao! Arthur keshafikia kustaafu!He looks so young and energetic!
   
 6. e

  echonza Senior Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nawapongeza walioguswa na uteuzi mpya na waliopandishwa kutoka Unaibu kuwa Makatibu Wakuu. Nawaombea kwa Mungu awape nguvu ya kuwatumikia watanzania. Hata hivyo, nimeshangazwa sana kusikia kwamba Patrick Rutabwanzibwa kuhamishiwa Wizara nyingine wakati tu ana muda mfupi pale mambo ya ndani akitokea Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Kama kweli hawa watu ni muhimu katika kuweka misingi ya utendaji ndani ya Sekta husika, sijaona kwa nini Mtaalamu kama Ruta kutolewa pale alipokuwa tu ameanza kuweka misingi ya namna ya utendaji ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Utampima vipi utendaji wake mtu kama yule? Tatizo nashindwa kuelewa ama Rais anashauriwa vibaya na wasaidizi wake ama ni maamuzi yake yasiyozingatia wataalamu wanasema nini.

  Hata mwajiri akiwa anatafuta mtu wa kumwajiri na siku ya usaili akajitokeza mtu aliyehama makampuni zaidi ya manne ndani ya miaka miwili hakika hatapewa kazi kwa misingi ya kutokuwa makini na utendaji wake. Kwa nini asitulie? Sasa hili la Rais kumhamisha Katibu Mkuu ndani ya Miaka miwili mara mbili ni suala la ajabu na la kushangaza kabisa. Mimi naliona halina tija ndani yake. Patrick Rutabanzibwa liacha misingi ya utendaji wa uwajibikaji pale maji na ninavyomfahamu hata huko mambo ya ndani atakuwa amefikia hatua fulani kufanya mabadiliko ili watanzania tujifunze kufanya kazi kwa tija. Lakini hajamaliza muda kapelekwa kwingine tena, duh hiyo lazima mimi niipe tafsiri ya kutozingatia taratibu katika kufanya mabadiliko ndani ya Serikali.
   
 7. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jairo kaula...
   
 8. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko katika safu ya maofisa waandamizi wa Serikali kwa kuteua Makatibu Wakuu wa Wizara wanne wapya, kuhamisha wengine wawili, na kuteua Katibu wa Rais mpya.

  Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Oktoba 19, 2009, Ikulu, mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Philemon Luhanjo, imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amefanya mabadiliko hayo kufuatia kustaafu kwa baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara.

  Aidha, taarifa inasema kuwa mabadiliko hayo yanaanza leo, Oktoba 19, 2009.

  Taarifa hiyo imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana David Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Jairo alikuwa Katibu wa Rais.

  Bwana Jairo anachukua nafasi ya Bwana Arthur Mwakapungi ambaye amestaafu.

  Katika taarifa yake, Bwana Luhanjo amesema kuwa pia Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sazi Salula kuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Salula alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Taarifa hiyo pia imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Mbarak M. Abdulwakil aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Bwana Abdulwakil anachukua nafasi ya Bwana Patrick Rutabanzibwa ambaye anahamishiwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kama Katibu Mkuu. Ndugu Rutabanzibwa anachukua nafasi iliyoachwa na Bi. Salome Sijaona ambaye amestaafu.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mhe. Rais Kikwete pia amemteua Bwana Christopher N. Sayi kuwa Katibu Mkuu wa Wizata ya Maji na Umwagiliaji.

  Kabla ya uteuzi wake, Bwana Sayi alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo hiyo, na anachukua nafasi ya Bwana Wilson Mukama ambaye ameanza likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.

  Bwana Luhanjo amesema katika taarifa yake kuwa vile vile Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sethi Kamuhanda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

  Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kamuhanda alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Anachukua nafasi Dkt. Florence Turuka ambaye anahamishiwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kama Katibu Mkuu. Bw. Turuka anachukua nafasi ya Dkt. Naomi Katunzi, ambaye anamaliza mkataba wake wa utumishi wa Serikali mwezi ujao, Novemba, 2009.

  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi pia inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mbena alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, na anachukua nafasi ya Bwana Jairo.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  19 Oktoba, 2009
   
 9. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  David Jairo kupelekwa Nishati na Madini mi ndio naona move of the day. Jamaa alikuwepo wizara ile enzi za IPTL na JK akiwa waziri...Baadae akapotea, alipokuja kuibuka ni katibu wa rais, JK alipochukua nchi, now anamrudisha kulekule Nishati na Madini.

  Inawezekana amepelekwa kwa kazi maalum, maana huyu jamaa ni very daring na on the other side ni msaidizi mwaminifu wa JK. Sikilizieni maamuzi bold sasa from Wizara ya Nishati na Madini...Mzee Mwakapugi walikua wanampelekesha tu mzee wa watu, hana makuu, alichokua anakitaka ni kustaafu salama na kakipata.
   
 10. K

  Kyaruzi Member

  #10
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 23, 2007
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuomba kazi ya kuwa katibu wa kudumu wa Mambo ya ndani kabla yake kuna makatibu watatu wameondolewa.ukiona kaondolewa kachemsha.
   
 11. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  PS Rutabanzibwa amehamishwa Mambo ya ndani kwa sababu ya kutofautiana na waziri wake.Inawezekana Rais amepata ushauri kutoka kwa Waziri ya kumbadilisha kituo cha kazi PS Patrick.
   
 12. E

  Eddie JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hah hah... JK anawabeba waislamu, teuzi zake zote udini mtupu anajaza waislamu tu tena hawana sifa.

  Wapo wapi wapondaji? au ndio mambo ya status quo?
   
 13. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JK anawapendelea wakristo ...hata akijipendekeza jamaa hawanaga shukruni ni kama nguruwe..akiingia shambani atakula kila kitu peke yake ..JK mnafiki tu...
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  ...

  AZIMIO NAMBA 7:
  "Wajumbe wote wa Kamati ya Serikali ya Majadiliano (Government Negotiation Team – GNT) ambao ni Maofisa Waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya Umma kwa kulitia hasara Taifa kutokana na kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya Taifa".

  HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
  Katika kushughulikia suala hili, (yaani katika mchakato mzima wa Zabuni pamoja na majadiliano ya Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND), kulikuwa na Kamati za aina tatu.

  Kwanza, ni Kamati iliyokuwa inaundwa na Mwanasheria Mkuu wa SerikaliMheshimiwa Johnson Mwanyika (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati naMadini Bw. Arthur Mwakapugi pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi Bw. Gray Mgonja. Kamati hii ilikuwa na jukumu la kutoa ushauri kwaWaziri wa Nishati na Madini na Serikali kwa ujumla.

  ....

  AZIMIO NAMBA 14:
  "Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), na Katibu Mkuu, Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni.

  Aidha, Kamishna wa Nishati, Ndugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara mwaka 2004 kwenye Mradi wa bomba la mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua Kampuni hiyo kusitisha Mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura haujaanza."


  HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
  a) Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki alijiuzulu mwezi Februari 2008 kwa kuwajibika kutokana na suala hili. Hata hivyo, kwa lengo la Serikali kujiridhisha zaidi kuhusu ushiriki na ushauri wake katika suala hili, Vyombo vya Dola vinaendelea kuendesha uchunguzi wa kina. Lengo ni kutaka kujua kama kuna rushwa yoyote inayomhusisha Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), ambayo ilijitokeza katika mchakato huu, ili hatimaye uamuzi stahiki dhidi yake uweze kuchukuliwa.

  b) Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. ArthurMwakapugi ambaye alikuwa miongoni mwa Wajumbe watatu wa Kamatiiliyoundwa na Makatibu Wakuu wa Fedha na Uchumi, Nishati na Madinipamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, naye amepelekewa barua yakutakiwa ajieleze katika maeneo ambayo Kamati Teule ya Bunge ilibainikuwa hakuyazingatia kwa maslahi ya Taifa. Hatua hii imechukuliwa kwakuzingatia Sheria na Kanuni za Nidhamu katika Utumishi wa Umma na

  Misingi ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (
  Natural Justice), kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

  Bwana Mwakapugi amekwishawasilisha maelezo yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ndiye Mamlaka yake ya Nidhamu katika muda uliotakiwa.

  Chanzo:

  TAARIFA YA WAZIRI MKUU, MHE. MIZENGO P. PINDA,
  (MB.), KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BUNGE YA MKATABA BAINA YA TANESCO NA
  RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY

   
 15. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kambeba nani hapa? au unamcheka kwa kuwajaza nyinyi watupu?Kamuhanda ana uzoefu gani?
   
 16. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hongera Bi. Salome Sijaona kwa kustaafu, sasa naona kazi ipo huyu Bw. Rutabanzibwa atauza ardhi yetu, tuwe macho.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  Mtuhumiwa katika kashfa ya Richmond astaafu kazi serikalini

  Na Boniface Meena
  Mwananchi
  10/19/2009


  MMOJA wa watuhumiwa wa kashfa ya mitambo ya kufua umeme ya Richmond Development (LLC), ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi amestaafu wadhifa wake huo na nafasi yake imechukuliwa na David Kitundu Jairo, aliyekuwa Katibu wa Rais Jakaya Kikwete.

  Mwakapugi amestaafu wakati serikali ikisubiriwa kutoa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Kampuni ya Richmond kwenye Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

  Mkutano wa 17 wa Bunge unatarajiwa kutawaliwa na mzimu wa Richmond, ambayo ilipewa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura mwaka 2006 kwa njia ambazo zilionekana kukiuka taratibu na kusababisha Bunge liunde kamati teule iliyotoa taarifa ambayo iliwahusisha baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu ya nne.

  Kufuatia kuibuka kwa kashfa hiyo, aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, alilazimika kujiuzulu wadhifa wake huo baada ya kuhusishwa katika sakata hilo.

  Katika mkutano wa 16 wa Bunge uliomalizika mwishoni mwa Agosti mwaka huu mjini Dodoma, serikali ilijaribu kuwasafisha maafisa wake waandamizi; mpango ambao ungewasafisha pia mawaziri waliojiuzulu, lakini Bunge likagoma na kuiagiza serikali kutekeleza maazimio yake kwa kuwawajibisha maafisa hao.

  Mwakapugi ni mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakichunguzwa kuhusu kashfa ya Richmond na wengine ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini(Takukuru), Dk Edward Hoseah na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

  Tayari Mwanyika amechukua likizo na anatarajiwa kustaafu mwezi ujao. Kwa upande wa Dk Hoseah na maafisa wengine wa serikali bado haijulikani ni hatua gani za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao kama Bunge lilivyoagiza katika maazimio yake.

  Kustaafu kwa Mwakapugi kumetokea mapema, kwani awali Ofisa Uhusiano wa Wizara ya Nishati na Madini, Aloyce Tesha aliliambia gazeti hili kuwa, Mwakapugi yuko likizo na anatarajiwa kustaafu mwezi Januari mwakani atakapotimiza rasmi miaka 60.

  "Yuko likizo, kwa kuwa alikuwa akihitajika sana ofisini, hivyo likizo zake alikuwa nazo na ndiyo amezichukua sasa hivi, anatarajiwa kustaafu mwezi Januari mwakani kisheria," alisema Tesha.

  Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo imeeleza kuwa Rais Kikwete amefanya mabadiliko katika safu ya maofisa waandamizi wa serikali kwa kuteua makatibu wakuu wa wizara wanne wapya, kuhamisha wengine wawili na kuteua katibu mpya wa rais.

  Katika taarifa hiyo, Luhanjo, alieleza kuwa Rais Kikwete amefanya mabadiliko hayo kufuatia kustaafu kwa baadhi ya makatibu wakuu wa wizara akiwemo Mwakapugi.

  Tayri Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, ambao walijiuzulu uwaziri kutokana na taarifa ya kashfa hiyo, walishatoa maelezo yao bungeni na nje ya Bunge huku Karamagi akisema kama kuna ushahidi apelekwe mahakamani.

  Tangu kusainiwa kwa mkataba wa Richmond Juni 23, 2006 na Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu, wabunge wamegawanyika kutokana na baadhi kuunga mkono maazimio na wengine kupinga.

  Mgawanyiko huo umesababisha kundi moja kujiita kuwa ni vinara wa mapambano dhidi ya ufisadi na jingine likipinga vita hiyo kwa madai kuwa inaichafua serikali ya CCM na chama chake.

  Mbali na Ikulu kuridhia Mwakapugi kustaafu, taarifa yake iliyotolewa na Luhanjo imeeleza kuwa mabadiliko hayo yameanza jana Oktoba 19, 2009.
   
 18. K

  Keil JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama ni operation safisha Richmond, basi ngoja tuone watasema nini kwa Dr. Hosseah, sijui nae watasema anastaafu ama mkataba umeisha? Maana Mwanyika wameishasema kwamba anastaafu mwezi ujao.
   
 19. K

  Keil JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwawado, yaonekana una inside info, huyu Bwana Rutabanzibwa ametofautiana na Waziri wake kwenye issue gani? Maana Wizara ya Mambo ya Ndani ina kasheshe nyingi.
   
 20. 911

  911 Platinum Member

  #20
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Siku chache zilizopita GT alianzisha thread kuhusu David Jairo.Hopefully alikuwa anajua kuhusu huu uteuzi kabla haujawa public.Lakini namna alivyoileta sasa...
   
Loading...