Ni lazima nafasi nyeti zichukuliwe na "wastaafu"?

David Jairo kupelekwa Nishati na Madini mi ndio naona move of the day. Jamaa alikuwepo wizara ile enzi za IPTL na JK akiwa waziri...Baadae akapotea, alipokuja kuibuka ni katibu wa rais, JK alipochukua nchi, now anamrudisha kulekule Nishati na Madini.

Inawezekana amepelekwa kwa kazi maalum, maana huyu jamaa ni very daring na on the other side ni msaidizi mwaminifu wa JK. Sikilizieni maamuzi bold sasa from Wizara ya Nishati na Madini...Mzee Mwakapugi walikua wanampelekesha tu mzee wa watu, hana makuu, alichokua anakitaka ni kustaafu salama na kakipata.
Kama ndivyo basi kila la kheri maana kama kuna wizara ambayo walioko hawajui wanafanya nini ni hii ya nishati na madini. Tatizo la umeme halina majibu miaka nenda miaka rudi, tatizo la madini nalo halina majibu. Sasa jamaa wanakazi gani wizarani kama hakuna kitu kinaenda mpaka mwisho kwa mafanikio?
 
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi pia inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mbena alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, na anachukua nafasi ya Bwana Jairo.
Kwa wanaomfahamu hebu watueleze, Mbena si yule aliyekuwa Hazina kitengo cha fedha za nje? ambaye alishiriki katika kuwachotea mafisadi fedha za CIS?
 
Mimi Nampongeza Mh. Rais JK kwa kufanya uteuzi huu ambao ni kati ya Majukumu yake.

Pia nawapongeza wote walioteuliwa.

Kwa Moyo wa dhati ninampongeza Mhandisi Christopha N. Sai kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
 
Mwakapugi, Sijaona na Mukama wanastaafu, sawa kabisa lakini bado JK na serikali yake watupie macho mashirika machache ya umma yaliyosalia. Kuna huyu Mnene/Mkuu/Dingi wa Benki ya Posta yeye mbona haondoki.??????? Alistaafu mwaka 1997 halafu akaendelea kufanya kazi kwa mkataba wa miaka mitatu mitatu, huu sasa ni mwaka wake wa 12 kwa mkataba. Hivi hakuna WaTZ wengine wenye sifa ila yeye tu ilhali ana umri wa karibu miaka 70.

Wakuu nalileta jamvini suala hili maana hata uwezo wake wa kufikiri umedumaa. Anaogopa kompyuta kama nini maana hajawahi kujifunza na anaona aibu kuwaambia vijana wamfundishe. Hivi kweli karne hii mkubwa wa taasisi kama benki hajui matumizi ya mtandao na anaendelea tu kupeta kazini, jamani jamani, atafia kazini huyo msaidieni aondoke maana kazi yake ni kusinzia tu mezani akiachia kazi afanyiwe na kibaraka wake mmoja mwanasheria ambaye hafai kabisa kuongoza ila kajaa majungu tu kwa kila anayemwona tishio. Kazi yao matambiko tu kule mlingotini ndiyo maana hata bodi ya wakurugenzi haimwondoi mdingi yule ila kumpa mkataba mpya kila baada ya miaka mitatu. WANAJAMVI MPO??? Kazi kwenu lifanyieni kazi.
 
David Jairo kupelekwa Nishati na Madini....

Inawezekana amepelekwa kwa kazi maalum, maana huyu jamaa ni very daring na on the other side ni msaidizi mwaminifu wa JK...
Kwa kuwa IPTL bado ni moto unaowaka chini kwa chini....
Na kwa kuwa wakati IPTL inaanza Mukulu alikuwa Wizarani....
Na kwa kuwa jamaa ni msaidizi mwamnifu wa Mukulu....
Na kwa kuwa jamaa ni very daring....,
basi kuna uwezekano kweli amepelekwa kwa kazi maalum
 
Nimecheeeeka. Nikupe Jimbo?
 
Kwa kuwa IPTL bado ni moto unaowaka chini kwa chini....
Na kwa kuwa wakati IPTL inaanza Mukulu alikuwa Wizarani....
Na kwa kuwa jamaa ni msaidizi mwamnifu wa Mukulu....
Na kwa kuwa jamaa ni very daring....,
basi kuna uwezekano kweli amepelekwa kwa kazi maalum
Ndo uzuri wa JF...shoka huwa linatupwa shinani moja kwa moja. Labda daring yake ni kuyakabili yatakayojiri maana huo moto wa chini kwa chini ndo ile sauti ya madai ya haki itendeke bila mwekezaji kujeruhiwa peke yake
 
TEUZI za RAIS ni kama kuteuliwa na Mwenyezi Mungu. Hazipingiki, hazihojiki, wala hazijadiliki. Halafu tunadai tuna KATIBA, tuna BUNGE na tuna UTAWALA BORA sio BORA UTAWALA.
 
++
N
Yaani huyu badala ya kumuondoa na mambo ya Meremeta na vitambulisho anampeleka kwenye viwanja vyetu???? Haa tutasikia bosi wake Masha naye kahamishwa!!!!????

Huenda anakula na wakubwa katika kutuibia kwake
 
Nashangaa Mh. Rais kila akifanya mabadiliko mimi hanikumbuki au kuna mkono wa mtu
 
Sasa wewe Kyaruzi, kama kachemsha si apumzishwe? Hoja yangu haikuwa na nia ya kumtetea Ruta kubaki pale alipokuwa kabla, bali ilihoji juu ya maamuzi ya Mhe. Rais. Maana kama maji na umwagiliaji alishindwa au alichemsha na baadaye mambo ya ndani achemshe tena, sasa wa nini huyo? Wataalamu wameisha Tanzania yote hii? Unajua tuwe macho yanapotokea mambo ya namna hiyo.
 
Sina uhakika ana umri gani kwa sasa. Lakini inasemekana alitakiwa asitaafu mwezi Januari mwaka ujao. Hivyo, Rais anafahamu juu ya maamuzi yake yalisababishwa na nini. Ama ni kwa manufaa ya umma au kwa shinikizo la Bunge, hakika yeye anafahamu. Kimsingi tusubiri taarifa ya utekelezaji ya maagizo ya Bunge kuhusu watuhumiwa wa sakata la Richmond Development Ltd.
 
jairo kaula...

Huyu alikuwa katibu wa rais, ina maana ni mtu wa karibu sana na JK. Kwahiyo hatuelewi mipango iliyopo pengine ya kuendelea kutuibia madini yetu kupitia rafiki zao akina Sinclair na kupitia mikataba feki ya uzalishaji wa umeme kwa makampuni mbalimbali.
 
David Jairo kupelekwa Nishati na Madini mi ndio naona move of the day. Jamaa alikuwepo wizara ile enzi za IPTL na JK akiwa waziri...Baadae akapotea, alipokuja kuibuka ni katibu wa rais, JK alipochukua nchi, now anamrudisha kulekule Nishati na Madini.

Inawezekana amepelekwa kwa kazi maalum, maana huyu jamaa ni very daring na on the other side ni msaidizi mwaminifu wa JK. Sikilizieni maamuzi bold sasa from Wizara ya Nishati na Madini...Mzee Mwakapugi walikua wanampelekesha tu mzee wa watu, hana makuu, alichokua anakitaka ni kustaafu salama na kakipata.

Aisee! Kumbe! Mhhhhhhh! May GOD forbid all kinds of wizi wa rasilimali zetu through this guy.
 
Hah hah... JK anawabeba waislamu, teuzi zake zote udini mtupu anajaza waislamu tu tena hawana sifa.

Wapo wapi wapondaji? au ndio mambo ya status quo?

Binafsi sijaona udini kwenye uteuzi huu. Naona bwana mkubwa ame-balance vizuri.
 
Una maana gani Mkuu? DINI na KABILA navyo ni vigezo kwenye TEUZI hizi?! TUMEKWISHA!

Mkuu angalia vizuri kwenye hiyo post yangu No. 37 hapo juu. Nilikuwa na-respond kwenye post ya mkuu Eddie hii hapa chini.

Hah hah... JK anawabeba waislamu, teuzi zake zote udini mtupu anajaza waislamu tu tena hawana sifa.

Wapo wapi wapondaji? au ndio mambo ya status quo?

Sikuwa na maana ya kuwa kabila au dini ni kigezo cha kuteuliwa kwenye cheo fulani. Hope umenielewa.
 
Mkuu angalia vizuri kwenye hiyo post yangu No. 37 hapo juu. Nilikuwa na-respond kwenye post ya mkuu Eddie hii hapa chini.

Sikuwa na maana ya kuwa kabila au dini ni kigezo cha kuteuliwa kwenye cheo fulani. Hope umenielewa.
Nimekuelewa. Vigezo hivi vipo sana ingawa havisemwi hadharani. CCM wanavitumia sana hasa baada ya Mwalimu kuondoka madarakani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom