Ni lakijinga lakini nilichemsha pia

MUREFU

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,224
1,225
waungwana leo nimeingia kwenye daladala nikawa nimesimama mara akaingia mzee na mwanafunzi wasekondali kama watatu kutoka kituo kinachofuata. yule mzee akawauliza wale wanafunzi ilikuwa hivi :-
Mzee: Hamjambo watoto?
Wanafunzi: Hatujambo shikamoo!
Mzee: Marahabaa! mnasoma wapi?
Wanafunzi: Shule ****** secondali
Mzee: Mpo kidato cha ngapi?
Wanafunzi: Kidato cha pili
Mzee: Safi sana hebu niambieni hivi sasa Tanzania ninamikoa mingapi?
Wanafunzi: Hatujui babu
Mzee: Hamjui? wanafunzi wa kidato cha pili hamjui?
Wanafunzi: Sio sisi tuu hata gali zima hili hawajui maana kila siku nchi yetu mikoa ninaongezeka
Mzee: Ndio inatangazwa kila siku lakin inapaswa kujua mikoa na wilaya zake. umesema gali zima hawajui?
Wanafunzi: Ndio wangekuwa wanajua wangeshajibu.
(Kweli gali zima lilikuwa kimya nikiwemo kama kawaida kondakta hawakosi kuropoka au kuongea)
Konda: Nyinyi wanafunzi mnajua nini kama sio Fasebuku tuu mikoa ipo 120 Kama makabila yapo 26 kazi yenu facebuku tuu ndio maana hamjui.
KIUKWELI WOTE TULIBAKI KIMYA ZAID NA KUTOKANA ILIKUWA HASUBUHI HAKUNA ALIEKUWA ANAZUNGUMZA. SWALI LANGU NI HILI MAANA NA MIMI NILISHINDWA HEBU NITAJIENI KUNAMIKOA MINGAPI KWA SASA NA WILAYA NGAPI TANZANIA?
 

NEGLIGIBLE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
356
225
Hivi tatizo la kushindwa kutofautisha "l" na "r" ni la kurithi?
Sekondali-sekondari
gali-gari
hasubuhi-asubuhi
 

wa home

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
233
225
jibuni sio mnakuja kurekebisha watuuu, umu hamjui wengine ni wahehe? Leteni jibu mkishindwa nitarudi kujibu.
 

Wakumwitu

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
372
195
Kaka "r" na "l" siyo tatizo la mshikaji hapo juu pekee. Inategemea umekulia wapi, na kabira lako pia. Ninakiri kuwa, pamoja na kusoma kwangu kote, tatizo limegoma kunitoka. Kwa kiingereza naweza andika vizuri, ila nikachesha kutamka. Kiswahili Kwa kweli nahitaji ushauri wa daktari.
 

Von Mo

JF-Expert Member
May 7, 2012
1,823
2,000
[h=3]SERIKALI YA TANZANIA YATANGAZA RASMI MIKOA NA WILAYA MIPYA[/h] SERIKALI YA TANZANIA YATANGAZA RASMI MIKOA MIPYA MINNE NA WILAYA 19

SERIKALI ya Tanzania imetoa matangazo rasmi ya Serikali (Government Notices)
kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya minne na wilaya mpya 19 ambayo
yamechapishwa tangu Machi 2, mwaka huu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema matangazo hayo ambayo yalisainiwa na

Rais Jakaya Kikwete tangu Machi mosi, 2012, yanabainisha mikoa mipya
kuwa ni Geita, Katavi, Njombe na Simiyu. Mikoa hii imechapishwa katika
Tangazo la Serikali Na. 72.

Wilaya 19 ambazo zimeanzishwa na kuchapishwa katika Tangazo la

Serikali Na.73 ni Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi na
Itilima. Wilaya nyingine ni Kakonko, Kalambo, Kaliua, Kyerwa, Mbogwe,
Mkalama na Mlele. Nyingine ni Momba, Nyang'hwale, Nyasa, Uvinza na
Wanging'ombe.

Kwa mujibu wa matangazo hayo makao makuu ya mikoa hiyo mipya minne

yatakuwa kama ifuatavyo: Geita (Geita), Simiyu (Bariadi) Njombe
(Njombe) na Katavi (Mpanda).

Mikoa hiyo itakuwa na wilaya zifuatazo; Geita utakuwa na wilaya tano

za Bukombe, Chato, Geita, Mbongwe na Nyang'hwale. Mkoa wa Katavi
utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda. Mkoa wa Njombe utakuwa na
wilaya nne za Makete, Njombe, Ludewa na Wanging'ombe wakati mkoa wa
Simiyu utakuwa na wilaya tano za Bariadi, Busega, Maswa, Meatu na
Itilima.

Makao makuu ya wilaya mpya zilizoanzishwa ni kama ifuatavyo: Buhigwe

(Buhigwe); Busega (Nyashimo); Butiama (Butiama); Chemba (Chemba);
Gairo (Gairo); Ikungi (Ikungi) Itilima (Lagangabilili); Kakonko
(Kakonko); Kalambo (Matai) na Kaliua (Kaliua).

Nyingine ni Kyerwa (Rubwera); Mbogwe (Mbogwe); Mkalama (Nduguti);

Mlele (Inyonga); Momba (Chitete); Nyang'hwale (Kharumwa); Nyasa
(Mbamba Bay); Uvinza (Lugufu) na Igwachanya (Wanging'ombe).

Julai 2010, kabla Rais Kikwete hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge,

Serikali ilitoa uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya mpya 21.
Hata hivyo, baada ya kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa
maelezo ya mipaka hiyo vizuri (boundary descriptions),wilaya
zilipunguzwa na kubakia 19.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, MACHI 8, 2012.
MIKOA YA TANZANIA BARA.
Na. Mkoa
1 Arusha
2 Dar Es Salaam
3 Dodoma
4 Iringa
5 Kagera
6 Kigoma
7 Kilimanjaro
8 Lindi
9 Manyara
10 Mara
11 Mbeya
12 Morogoro
13 Mtwara
14 Mwanza
15 Pwani
16 Rukwa
17 Ruvuma
18 Shinyanga
19 Singida
20 Tabora
21 Tanga

MIKOA MIPYA ITAKAYOANZISHWA
(i) Mkoa wa Njombe ambao unatokana na kumega na kuunganisha
Wilaya za Njombe, Ludewa na Makete kutoka Mkoa wa Iringa.
Mkoa huu utakuwa na Wilaya mpya ya Wanging'ombe ambayo
inatokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Njombe.

(ii) Mkoa wa Geita ambao unatokana na kumega na kuunganisha
Wilaya za Geita kutoka Mkoa wa Mwanza, Bukombe kutoka Mkoa
wa Shinyanga na Chato kutoka Mkoa wa Kagera. Mkoa huu
utakuwa na Wilaya mpya ya Nyang'hwale ambayo inatokana na
kugawanywa kwa Wilaya ya Geita.

(iii) Mkoa wa Simiyu ambao unatokana na kumega na kuunganisha
Wilaya za Bariadi kutoka Mkoa wa Shinyanga, Maswa kutoka Mkoa
wa Shinyanga, Meatu kutoka Mkoa wa Shinyanga na Wilaya mpya
ya Busega kutoka Mkoa wa Mwanza. Mkoa huu utakuwa na Wilaya
nyingine mpya ya Itilima ambayo inatokana na kugawanywa kwa
Wilaya ya Bariadi.

(iv) Mkoa wa Katavi ambao unatokana na kumega na kuunganisha
Wilaya za Mpanda kutoka Mkoa wa Rukwa pamoja na Wilaya
mpya ya Mlele ambayo inatokana na kugawanywa kwa Wilaya ya
Mpanda.
MADHUMUNI YA KUANZISHWA MIKOA MIPYA
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza kuwa, kwa ajili ya
utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Mheshimiwa Rais anaweza kuigawa
Nchi katika Mikoa au Wilaya. Hivyo, madhumuni ya kuanzishwa kwa Mikoa hiyo
ni kuboresha utendaji wa Serikali Kuu kwa kupunguza ukubwa wa maeneo ya
Mikoa mama ili Wananchi wapate huduma za kiutawala ngazi ya Mikoa kwa
Karibu

Jumla ya Mikoa ya Tanzania Bara itakuwa 25 ambayo ni Arusha, Dar Es
Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara,
Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga,
Singida, Tabora, Tanga, Njombe, Geita, Simiyu na Katavi

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom