Ni kweli kuku ana sumu kali kuliko nyoka?

Ni kweli kuku ana sumu kali kuliko nyoka?

Hivi ulikuwa unamaanisha nini hapa?

Ni wapi sijaeleweka?mleta mada kasema usiku ukiwa unaenda kwa kuku useme ili ajue ni mtu asije kukudonoa kwa sum

Nimejaribu kuuliza,ninavyojua mim sum ya nyoka imehifadhiwa kwenye mishipa maalum kwenye mwili wa nyoka ambapo nyoka akibugudhiwa huirelease kupitia mishipa maalum na meno maalum aliyonayo kwenda kwenye mwili wa adui yake.

Kisha nikauliza hiyo sum ya kuku iko wapi au inakua imehifadhiwa wapi kwenye mwili wa kuku,na inatolewaje kwenda kwenye mwili wa adui ili imdhuru?

Nilikua namaanisha hivyo ingawa maneno yalikua machache ila hiyo ndio dhana yake.
 
kwa hiyo mkuu unabisha ukiwa na uhakika au unabisha kwa kuwa hujui sumu ya nyoka inakaa sehemu gani mwilini mwake?

Nan amesema hajui sum ya nyoka inakaa sehem gan?una uhakika ulichouliza ndicho unachokimaanisha?
 
Ni kweli mie huwa namwimbia taarabu anakuwa mpole kama Aisha Mashauzi halafu ndo namgusa!
 
Hata mate ya binadamu ni sumu kwa nyoka. Indocid (yes, ile dawa ya kutuliza maumivu kwa binadamu) ni sumu kali kwa panya!

Panya gani wanaokufa kwa indocid?mie nilitega unga wa indocid kwenye chakula nillikuta panya tena mmoja aliyekuwa ananisumbua amekula chakula chote nikadhani angekufa!Kesho yake alikuja hadi kwenye net usiku!bonge la panya ila nilimnasa kwa gundi nikamuua.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Panya gani wanaokufa kwa indocid?mie nilitega unga wa indocid kwenye chakula nillikuta panya tena mmoja aliyekuwa ananisumbua amekula chakula chote nikadhani angekufa!Kesho yake alikuja hadi kwenye net usiku!bonge la panya ila nilimnasa kwa gundi nikamuua.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Kumbe unatumia net?
 
Ni kweli ila sio muda wote inakua ni wakati wa usiku wa manane pindi kuku akiwa kalala fofofo huwa sumu inajikusanya kwenye kucha na mdomoni ili kujilinda na adui yeyote, na si vyema wakati huo kumshika kwa ghafla inabidi umshitue kwanza ndipo umkamate

wezi wakuku wanayajua haya unayoyasema..basi tungekuwa tushazika wengi na kuku wasingeibiwa nyumbani kwetu
 
Elimu na iwe msingi wa kujitambua, kuchambua na kujenga hoja kwa mantiki sahihi.
Ninachoona mimi ni kilekile,, tunaishi kwa Gossip!! we kama kuku ana sumu zaidi ya nyoka ungeweza kula kichwa chake? just by simple reasoning, inawezekana? eti ugune ajue we ni binadamu, kwani binadamu hawezi kumdhuru?
Akili ndogo isiachwe itawale akili kubwa, elimu sio kujua kusoma ama kutengeneza magari etc, iwe njia ya kupanua uwezo wako wa kufikiri na kujenga hoja.
mk1


Mkuu usibishe kwa gossip, otherwise jiweke neutral ili ujue zaidi.

Kuna mdau kasema kuwa kuku hupasua kichwa cha nyoka ndipo anamuua, si kweli. Niliishawahi kushuhudia kuku akimdonoa nyoka kama mara nne na nyoka akalegea na kufa kabisa.

Lakini nyoka huyo huyo unaweza tumia nguvu nyingi kama mara nne hivi ndo anakufa. Niliuliza wazee waliokuwepo walinipa jibu hilo kuwa kuku ana sumu kali sana ambayo anapomdonoa nyoka huiachia, na ndo ambayo humuua.
 
Nasubir giza liingie nimvizie kuku wangu bandani anidonoe nione kama ntakufa, incase nikifa basi mtoa mada itabidi awe responsible, vyombo vya usalama are we together?
 
Nasubir giza liingie nimvizie kuku wangu bandani anidonoe nione kama ntakufa, incase nikifa basi mtoa mada itabidi awe responsible, vyombo vya usalama are we together?

mkuu mbona ukutupa majibu tena alikufa eneo la tukio!?
 
Kwa hiyo akishasikia ni binadam ndio hakudonoi?sijui ni kwa nini uongo na uzushi huenea kwa kasi na haraka kuliko ukweli.

Hakuna kitu kama hiyo mkuu,huo ni uongo na uzushi mkubwa,nyoka kitaalam ana mishipa baadhi ya sum sio mwili wote,je kuku hiyo sumu inakaa wapi?.

Wale mnaopinga eleweni kwamba mambo mengi hayajafanyiwa utafiti duniani. Ni kweli kuku ana sumu, jongoo ana sumu pia, Chura ana sumu, dudumizi ana sumu. Kuku ana sumu kali sana hasa akiwa na vifaranga ama ameatamia mayai. Sumu yake hiyo ni ya kujikinga. Hebu kwa wale wanaobisha, hamjawahi kuona kuku akimla nyoka, tena wakati mwingine akiwamzimamzima! Babu zetu wenye akili kuliko sisi , walilijua hili na ndiyo sababu wanakwambia ukipita sehemu kuku kaatamia ama ana vifaranga usiku, ama uwe na taa au zungumza ajue huyo ni mtu na hana madhara, vinginevyo akikudonyoa ni vigumu kupona.
 
Panya gani wanaokufa
kwa indocid?mie nilitega unga wa indocid kwenye chakula nillikuta panya
tena mmoja aliyekuwa ananisumbua amekula chakula chote nikadhani
angekufa!Kesho yake alikuja hadi kwenye net usiku!bonge la panya ila
nilimnasa kwa gundi nikamuua.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Indocid Expired!
 
Kweli elimu ni janga la kitaifa. Yaani hata JF sasa tunabishana kuhusu kuku kuwa ama kutokuwa na sumu! Huyu huyu ndege tunayemfuga kupata nyama na mayai?? Kwa kifupi, kuku HANA sumu yoyote ila mdomo wake ni mgumu ni misuli yake ya shingo ina nguvu na ndio maana anaweza kuuwa wadudu wengi wakiwemo nyoka na nge. sio sumu, ni ugumu tu wa mdomo wake na nguvu za misuli ya shingo yake. kwa binadamu sana sana utapata kidonda tu kutokana na uchafu mwingi ulio kwnye ncha ya mdomo wake. dah! haya mapokeo haya...!
 
Kwa hiyo akishasikia ni binadam ndio hakudonoi?sijui ni kwa nini uongo na uzushi huenea kwa kasi na haraka kuliko ukweli.

Hakuna kitu kama hiyo mkuu,huo ni uongo na uzushi mkubwa,nyoka kitaalam ana mishipa baadhi ya sum sio mwili wote,je kuku hiyo sumu inakaa wapi?.

Mkuu kama hujui uliza ufafanuliwe lkn sio kukanusha halafu wkt umesha kataa, unauliza tena swali. Huu si uungwana.

Mimi naamini kuku ana sumu kali na anapopambana na kitu kinachoweza kudhuru uhai wake. Nimeshuhudia kuku akipambana na nyoka, hali kadhalika nyoka na chura. Anayewahi mwenzie ndiye humwua mwenzake kwa sumu. Kuku akishadonoa nyoka, palepale nyoka hulegea na kuishiwa nguvu. Kama umekulia mjini, waachie wa shamba wakueleze.

Kuku akimwona nyoka, huwa hakimbii anamkabili japokuwa nyoka huwa mwelevu na mwepesi kuliko kuku.

Chura yeye yuko tofauti, akifanikiwa kumn'gata nyoka haachii hadi nyoka afe ndo anaachia
 
wezi wakuku wanayajua haya unayoyasema..basi tungekuwa tushazika wengi na kuku wasingeibiwa nyumbani kwetu
mkuu wezi nao ni binadamu hivyo huweza kuwasha tochi ili kuweka wazi ubinadamu wao,kwa maana hiyo kuku lazima atulie!
japo sisemi kwamba kuku anasumu ni mpaka wataalamu watakapokuja kuthibitisha hili!
 
Back
Top Bottom