Ni kweli kuku ana sumu kali kuliko nyoka?

Ni kweli kuku ana sumu kali kuliko nyoka?

Nimetatizwa sana na hii kitu nimewahi kusikia mara kadhaa huko nyuma watu wakisema kuwa kuku hasa yule anaetaga au mwenye vifaranga huwa ana sumu kali kuliko hata ya nyoka.

Wakasema kuwa kama ukiwa unataka kumkamata usiku hasa kwenye giza ni lazima uongee ili ajue kuwa huyo anaekuja ni binadamu la sivyo ukipenyeza mkono wako kimyakimya akikudonoa dawa huwa hakuna lazima unabadilishwe jina kuwa marehemu.

tafadhali mwenye ufahamu juu ya kitu nitoeni gizani hizi ni habari za ukweli au ni mambo ya binadamu wa kwanza alikuwaga sokwe

Natanguliza shukrani wakuu

Hoja kama hizi huwa zanipa wakati mgumu sana kupinga kuwa watanzania wana upeo mfinyu sana wa akili.
 
wale mnaopinga eleweni kwamba mambo mengi hayajafanyiwa utafiti duniani. Ni kweli kuku ana sumu, jongoo ana sumu pia, chura ana sumu, dudumizi ana sumu. Kuku ana sumu kali sana hasa akiwa na vifaranga ama ameatamia mayai. Sumu yake hiyo ni ya kujikinga. Hebu kwa wale wanaobisha, hamjawahi kuona kuku akimla nyoka, tena wakati mwingine akiwamzimamzima! Babu zetu wenye akili kuliko sisi , walilijua hili na ndiyo sababu wanakwambia ukipita sehemu kuku kaatamia ama ana vifaranga usiku, ama uwe na taa au zungumza ajue huyo ni mtu na hana madhara, vinginevyo akikudonyoa ni vigumu kupona.
huu ndio nakwambia ni uongo,nimefuga kuku sana toka nikiwa mdogo,nimedonolewa sana na kuku wanaoatamia au wenye vifaranga.kama ndio hivyo ningekua nishakufa mkuu,nimedonolewa sana na kuku.
 
Mkuu kama hujui uliza ufafanuliwe lkn sio kukanusha halafu wkt umesha kataa, unauliza tena swali. Huu si uungwana.

Mimi naamini kuku ana sumu kali na anapopambana na kitu kinachoweza kudhuru uhai wake. Nimeshuhudia kuku akipambana na nyoka, hali kadhalika nyoka na chura. Anayewahi mwenzie ndiye humwua mwenzake kwa sumu. Kuku akishadonoa nyoka, palepale nyoka hulegea na kuishiwa nguvu. Kama umekulia mjini, waachie wa shamba wakueleze.

Kuku akimwona nyoka, huwa hakimbii anamkabili japokuwa nyoka huwa mwelevu na mwepesi kuliko kuku.

Chura yeye yuko tofauti, akifanikiwa kumn'gata nyoka haachii hadi nyoka afe ndo anaachia

mkuu nimekuelewa,ni kweli mkua kuku hula na kuua wadudu au wanyama wenye sumu kama nyoka,sijakataa,ila kuhusu kuku kuweza kumdhuru binadam kwa sum yake hilo ndio jambo ambalo sikubaliani nalo,nimedonolewa sana na kuku,ningekua nishakufa
 
huu ndio nakwambia ni uongo,nimefuga kuku sana toka nikiwa mdogo,nimedonolewa sana na kuku wanaoatamia au wenye vifaranga.kama ndio hivyo ningekua nishakufa mkuu,nimedonolewa sana na kuku.

mkuu inategemea ni wakati gani...usiku au mchana
 
Hoja kama hizi huwa zanipa wakati mgumu sana kupinga kuwa watanzania wana upeo mfinyu sana wa akili.

mkuu watu wenye akili wanapinga hoja kwa hoja sio hoja kwa kejeli na dharau....waugwana hawaishi namna hiyo
 
Haha! duh, kuna vitu vingine yani hata kwa akili ya kawaida tu kuku sumu? tena kali kuliko nyoka? haha!
em ngoja nicheke kwanza ntarudi kuedit post...
 
Back
Top Bottom