Ni kweli kuku ana sumu kali kuliko nyoka?

Ni kweli kuku ana sumu kali kuliko nyoka?

mzaramo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2006
Posts
6,371
Reaction score
5,194
Nimetatizwa sana na hii kitu nimewahi kusikia mara kadhaa huko nyuma watu wakisema kuwa kuku hasa yule anaetaga au mwenye vifaranga huwa ana sumu kali kuliko hata ya nyoka.

Wakasema kuwa kama ukiwa unataka kumkamata usiku hasa kwenye giza ni lazima uongee ili ajue kuwa huyo anaekuja ni binadamu la sivyo ukipenyeza mkono wako kimyakimya akikudonoa dawa huwa hakuna lazima unabadilishwe jina kuwa marehemu.

tafadhali mwenye ufahamu juu ya kitu nitoeni gizani hizi ni habari za ukweli au ni mambo ya binadamu wa kwanza alikuwaga sokwe

Natanguliza shukrani wakuu
 
Na mimi utanisaidia hapa, kwa watakaochangia hoja, niliwahi sikia hivyo pia
 
Kwa hiyo akishasikia ni binadam ndio hakudonoi?sijui ni kwa nini uongo na uzushi huenea kwa kasi na haraka kuliko ukweli.

Hakuna kitu kama hiyo mkuu,huo ni uongo na uzushi mkubwa,nyoka kitaalam ana mishipa baadhi ya sum sio mwili wote,je kuku hiyo sumu inakaa wapi?.
 
ngoja wataalamu waje nami pia nahitaji kujifunza kitu hapa.
 
Ni kweli ila sio muda wote inakua ni wakati wa usiku wa manane pindi kuku akiwa kalala fofofo huwa sumu inajikusanya kwenye kucha na mdomoni ili kujilinda na adui yeyote, na si vyema wakati huo kumshika kwa ghafla inabidi umshitue kwanza ndipo umkamate
 
wangekua walishakufa wengi siamini haya mambo ya fiction story
 
Ni kweli ila sio muda wote inakua ni wakati wa usiku wa manane pindi kuku akiwa kalala fofofo huwa sumu inajikusanya kwenye kucha na mdomoni ili kujilinda na adui yeyote, na si vyema wakati huo kumshika kwa ghafla inabidi umshitue kwanza ndipo umkamate

Usiku wa manane hapana. Kuku hata mchana akimdonoa nyoka lazima afe ndugu yangu. Na kawaida anaemuwahi mwenzie lazima afe. Kwa binadamu hapo cna hakika kama inamdhuru au la
 
Ni kweli ila sio muda wote inakua ni wakati wa usiku wa manane pindi kuku akiwa kalala fofofo huwa sumu inajikusanya kwenye kucha na mdomoni ili kujilinda na adui yeyote, na si vyema wakati huo kumshika kwa ghafla inabidi umshitue kwanza ndipo umkamate

Asante mkubwa, kiukweli hata mie nlisikia hivyohivyo
 
Ni kweli hiyo ndiyo defensive mechanism yake haswa wakati wa usiku kwani haoni gizani ili adui akimnyemelea bas amuwahi
 
Back
Top Bottom