Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 7,035
- 15,332
Kiongozi! Zanzibar ni Nchi(Kisiwa/Mji) uliyondani ya Sayari Dunia.Macho yanauwezo wa kuona mbali sana, ndio maana tunaweza kuona sayari kama mars & mwezi & nyota.
Zanzibar hatuwez kuona sababu ya duara la dunia....
Zanzibar n karibu kuliko mars
Mars ni Sayari, Mwezi ni Satellite ya asili na Nyota ni magimba makubwa katika anga yanayong'aa na kutoa mwanga. Sayari huwa zinang'aa na hii hutokana na Sayari huwa zina akisi mwanga kutoka kwenye Jua, halikadhalika na mwezi vivyo hivyo. Mars, mwezi na nyota zina maumbile makubwa.
Zanzibar haing'ai wala haina nuru yoyote inayoifanya ing'ae, na laiti kama ingelikuwa na nuru kama ya nyota basi nuru yake tungeishudia kwa macho ndani ya hii Tz pasipo kuhadithiwa.
Tofautisha muono wa kuona kwa tambarare na muono wa kuona juu. Nukta yako ni kwamba kama lenzi ya macho ina ukomo mbona mwezi tunauona(???)Lakini umbali wa kutoka Dunia-mwezi ni km 384,400.
Tu assume kutoka Kigamboni mpaka Zanzibar ni tambarare tupu, hakuna miinuko wala milima wala bahari. Wewe umesimama km 0 kutoka Kigamboni, ila ulipo simama wewe hapo Kigamboni-Zanzibar ni umbali wa km 384,400. Kwa hayo macho ya kawaida ambayo unasema unauona mwezi kwa hizo km, kwa huo mfano Zanzibar kwa km hizo hizo utaiona?


