Ni kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo yapo taratibu sana?

Mkuu,Nimezaliwa na Kukulia Wilayani Kinondoni,Nimekaa Wilayani Kigamboni,Temeke na Ilala.Ila shughuli zangu zimenifanya nizunguke takribani kila kona ya Dar,,

Kigamboni kuanzia Feli kwenda Cheka,Kimbiji kutafuta Pemba mnazi
Kutoka Kibada kwenda Mwasonga nishafika

Ilala kuanzia Upanga,mChafukoge mpaka Kitunda,kuanzia ukonga mpaka Nzasa, Msongola kurudi Viwege na Magohe..Buguruni mpaka Tabata mpaka Kinyerezi na Kifuru

Temeke kuanzia Chang'ombe mpaka Tuangoma,kwenda Chamazi kwenda Mbande

Ubungo :Sinza kwenda Goba,Kwenda Msumi na Kiluvya,kuja Msigati...

Yan,Dar kimsingi Luna maeneo mengi bado huduma hazifika mkuu...
Wilaya ya Ilala ina maeneo kibao Umeme ni wa REA,maji machafu ya Visima.

Wilaya ya Ubungo maeneo mengi barabara ni mbovu,matope mwanzo mwisho.
Ndio hakuna sehem iliyoendelea kote, lakini sehemu zile zilizokua hazina maendeleo sasahv panaendelea sana na kujengeka sana, kigamboni Iko vile vile, kama kimbiji nilipita mwaka 2016, mpaka Leo pako vilevile, wakati sehemu nyingne zimeshakua mjini kabisa, ukweli ni kwba Kwa dar wilaya maendeleo yake yakio slow sana ni kigamboni, kama pametengwa hivi
 
Kwa Mujibu wa Wikipedia, Wilaya ya Kigamboni imeanzishwa November, 2015. Hivyo ni Moja ya Wilaya za Karibuni kuanzishwa.

Nadhani changamoto kubwa ni uchache wa mtandao wa barabara za lami.

Japo kwasasa nimeona Kuna upanuzi wa barabara kipande cha Kibugumo hadi maeneo ya Hospitali ya Wilaya.

Ukiwa mtu wa kupenda Utulivu, Kigamboni ni pahali pazuri sana kuishi, na maeneo mengi ya ardhi yamepimwa.

Binafsi naishi hapo, na Kwa vile hupenda upepo wa bahari basi Kila weekend napita pita kwenye beach kupunga upepo wa bahari 🤗.

Chini hapa ni Moja ya beach nilitembelea huko Jana, Iko hapo Maweni - Mji Mwema.

IMG_20240303_162348_486.jpg

Kigamboni ni pazuri, atakaye na aje 🙏
 
View attachment 2924236

Kigamboni ni pazuri, atakaye na aje 🙏
Zaidi ya huko maweni hujatoka ukaona barabara za matope na mashamba ya mpunga? Mapori?
 
Zaidi ya huko maweni hujatoka ukaona barabara za matope na mashamba ya mpunga? Mapori?
Maendeleo ni Process Mkuu

Hayo maeneo ni mengi huku, nimejenga jirani na Chuo cha Afya Kigamboni.

Sehemu niliyojenga, pana viwanja vingi vya watu viko wazi hivyo ilinigharimu sana kuufikisha Umeme site kwangu

Nafahamu hiyo kadhia ya barabara, japo najipa Imani kwamba huenda kufikia 2030 hali ikabadirika.
 
Ni asilimia ngapi panaboreshwa ndani ya wilaya nzima? Sehemu kubwa ni mapori na barabara mbovu sehemu nzuri ni chache ukilinganisha na wilaya nyingne, angalia hata barabara za lami za kigamboni ni ngapi, halafu angalia temeke, ilala, ubungo na kino utapata jibu kua kigamboni ndio wilaya iliyo ya mwisho kimaendeleo Kwa mkoa huu wa dar
Nakuuliza swali moja tu la msingi kaka.
UNAWEZA NIAMBIA IMECHUKUA MIAKA MINGAPI ILALA NA TEMEKE KUWA PALE ILIPOKUA??
Pia miji haiendelezwi kiduwanzi tu pasi na kutizama pull factors za kupaendeleza.
 
😃😃Kama mbutu pale ikifika usiku ni kama Upo mbeya giza lake
Maendeleo ni Process Mkuu

Hayo maeneo ni mengi huku, nimejenga jirani na Chuo cha Afya Kigamboni.

Sehemu niliyojenga, pana viwanja vingi vya watu viko wazi hivyo ilinigharimu sana kuufikisha Umeme site kwangu

Nafahamu hiyo kadhia ya barabara, japo najipa Imani kwamba huenda kufikia 2030 hali ikabadirika.
Yani 2030 wakati Kuna sehemu viwanja bei chee nguzo ipo hapo nnje, na ukitoka kilomita 2 tuu daladsla za kariakoo hizo hapo, magari ya mkoa pia unapata
 
Kigamboni ni kubwa sana, wewe unataja huko mwanzo mwanzo, Toka dege nenda kimbiji Hadi Pemba mnazi, tokea kibada pita mwasonga nenda kimbiji au tundwi songani, mkamba, Shariff, sacos, ngoma mapinduzi ni mapori tu unaweza ukasema sio dar Kuna nyumba Hadi za tope
Sasa wewe unategemea pajengeke kwa mara moja????
Kuna pull factors zipi za kupafanya pajengeke kwa haraka hivyo??
 
Nakuuliza swali moja tu la msingi kaka.
UNAWEZA NIAMBIA IMECHUKUA MIAKA MINGAPI ILALA NA TEMEKE KUWA PALE ILIPOKUA??
Pia miji haiendelezwi kiduwanzi tu pasi na kutizama pull factors za kupaendeleza.
Umekubali lakini kigamboni ndio wilaya ya mwisho kimaendeleo Kwa dar?
 
Pole sana kaka 😃

Sie tulishawai vamiwa.. kipind fulani mtaa mzima na majambazi ikabidib tuajiri wamasai wa ulinzi shirikishi
Pale ni balaa sana ila skuizi Kuna afadhali mie nakumbuka ilikuwa saa 11 asubuhi naenda zangu kariakoo nikiwa na begi langu nimebeba PC mkononi Nina simu kabla ya kumpigia simu boda boda akawa apokei simu nikaona sio kesi ngoja nitembee ile nafika njiani nikakabwa na jamaa kaniambia ukitikisika nakuuua nikawaambia sio kesi chukueni begi na PC na nilikuwa na elfu 50 mfukoni nikawaambia nayo chukueni wazee roho yangu niachieni wakanibakisha sina kitu haooo wakasepa na mapanga Yao walikuwa majamaa wawili walikuwa na silaha za mapanga wakakimbilia porini Toka siku ile nili Lia kama mtoto nilipotezea data zangu nyingi sana 😭😭😭😭😭
 
Yani 2030 wakati Kuna sehemu viwanja bei chee nguzo ipo hapo nnje, na ukitoka kilomita 2 tuu daladsla za kariakoo hizo hapo, magari ya mkoa pia unapata
Hata hivyo huku sio Kwa Kila mtu, wengine waache waishi huko huko Sinza/Makongo Juu n.k

Imagine gharama za kuvuka ukiwa na gari kwenda Mjini Kwa Mwezi tu unatumia 90,000 daraja la Kigamboni ama 120,000 ukivuka Ferry
 
Back
Top Bottom