Barabara ya Kibada - Mwasonga mbioni kuwekewa Lami, Bashungwa akagua athari za mvua

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,862
12,099
WhatsApp Image 2024-04-29 at 19.09.43_a0d01296.jpg

WhatsApp Image 2024-04-29 at 19.09.03_2ecc02d9.jpg
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa Serikali tayari imeshampata Mkandarasi na kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji yenye urefu wa kilometa 41 kwa kiwango cha lami.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuongezwa kwa ujenzi wa kilometa 10 katika barabara hiyo ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji kwa kuinganisha na kipande kilichobakia cha Kimbiji hadi Cheka kwa kiwango cha lami.

Bashungwa amezungumza hayo Aprili 29, 2024 Wilayani Kigamboni Mkoani Dar es Salaam katika ziara yake ya kikazi ya kukagua athari za miundombinu ya barabara na madaraja zilizotokana na mvua za El-Nino na kujionea hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Wakala wa Barabara (TANROADS).

“Nilivyokuja Kigamboni kukagua barabara hii ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji tulikuwa hatujasaini mkataba, nitumia nafasi hii kuwataarifu kuwa tayari tumesaini mkataba na sasa Mkandarasi anaendelea kuleta mitambo eneo la kazi ili mvua itakapokatika aweze kuanza kuijenga barabara hii kwa kiwango cha lami na haitakuwa kilometa 41 tena bali 51 kwani tunaiunganisha na kipande kilichobakia cha Cheka hadi Kimbiji”, amesema Bashungwa.
WhatsApp Image 2024-04-29 at 19.09.02_16433253.jpg

WhatsApp Image 2024-04-29 at 19.09.02_6fb0c13b.jpg
Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa Serikali iko kazini na imejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TANROADS na TARURA kurekebisha maeneo yote yaliyopata athari ili ziendelee kupitika na kutokwamisha shughuli za wananchi na viwanda katika uzalishaji.

Halikadhalika, Bashungwa amemuelekeza Mkandarasi Estim kuendelea kuleta vifaa na mitambo yote katika eneo la mradi wa barabara ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji wakati akisubiria malipo ya awali na kiangazi kianze ili ujenzi uweze kuanza mara moja.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameeleza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam hauna mafuriko ila wananchi wameziba njia za maji kwa kujenga nyumba kwenye mikondo ya maji na kusistiza kuwa Mkoa huo unahitaji kufumuliwa upya kwa na kujenga mifereji imara ya maji ya mvua ili kuzuia maji kutoingia kwenye makazi ya wananchi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile ameeleza kuwa barabara ya Kibada - Mwasonga hadi Cheka ni barabara muhimu sana kwa wananchi wa Kigamboni kwani inapitisha magari zaidi ya elfu moja ya ujazo mbalimbali makubwa na madogo na pia ni barabara inayoelekea kwenye viwanda vikubwa zaidi ya 10 na kuna eneo kubwa la uwekezaji hivyo ujenzi wa barabara hiyo utaleta tija na chachu ya kimaendeleo kwa wanakigamboni.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. John Mkumbo ameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji (km 41) utatekelezwa na Mkandarasi wa Kampuni ya Estim na tayari ameshakabidhiwa eneo la ujenzi tangu Aprili 10, 2024.
 
Mh bashungwa njoo barabara ya Mbezi stand ya Magufuli kupitia mpiji magoe mpaka Bunju B, Barabara makabe mpaka mpiji, na Barabara ya kibamba mpaka chama mpiji, zote ziunganishwe na kujengwa kiwango cha lami
 
Estim wako kwenye wakati mzuri sana, kule Zanzibar walikuwa na miradi 21, hadi ikabidi wanunue meli yao kwa ajili ya kubebea mchanga wa ujenzi.

Naona na hii ya Kibada - Mwasonga kapewa yeye. Ila kwa barabara hii ajipange, maana ina maeneo mengi korofi sana kipindi cha msimu wa mvua.

Ova
 
Mh bashungwa njoo barabara ya Mbezi stand ya Magufuli kupitia mpiji magoe mpaka Bunju B, Barabara makabe mpaka mpiji, na Barabara ya kibamba mpaka chama mpiji, zote ziunganishwe na kujengwa kiwango cha lami
Yue mkandarasi aliyejenga makabe msakuzi mhuni kweli kweli.....
Wakazi wa huko nawaonega huruma jinsi magari yao yanavyopigika na mashimo na maandaki huko

Ova
 
Yue mkandarasi aliyejenga makabe msakuzi mhuni kweli kweli.....
Wakazi wa huko nawaonega huruma jinsi magari yao yanavyopigika na mashimo na maandaki huko

Ova
Juz Muungano day nlienda mpiji magoe kupitia hii njia ya makabe, kwakweli hali ni mbaya sana

Kule watu wanaishi kwa tabu sana
 
Juz Muungano day nlienda mpiji magoe kupitia hii njia ya makabe, kwakweli hali ni mbaya sana

Kule watu wanaishi kwa tabu sana
Mimi nawashangaa watu wa kule
Wanashindwa hata kupiga kelele
Unakuta mtu anapita na vanguard yake namba E linapiga mashimo tu

Ova
 
Mh bashungwa njoo barabara ya Mbezi stand ya Magufuli kupitia mpiji magoe mpaka Bunju B, Barabara makabe mpaka mpiji, na Barabara ya kibamba mpaka chama mpiji, zote ziunganishwe na kujengwa kiwango cha lami
Barabara ya mbezi mpiji magohe inajengwa kwa kiwango Cha changalawe , Kwa Sasa serikali inajenga kipande Cha kibamba mpiji kwa awamu kiwango Cha lami. Sababu kubwa ni kwamba kipande Cha mbezi mpiji magohe kinahitaji fidia kubwa kwa wananchi kwenye utekelzji wa Barabara ya lami poa inahitajika ujenzi wa Madara makubwa manne hivyo bajeti yake ni kubwa. Ujenzi wa kibamba mpiji ukiisha serikali itafikria ujenzi wa njia Hy kwa kutafuta fedha kwa wahsan
 
Back
Top Bottom