Ni kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo yapo taratibu sana?

Dada amehamia kwake mwaka mpya ndio ilikua uzinduzi ""Cheka"" huko mbele mbele sanaa sababu ya umbali nilipata uvivu wa kwenda japo nilipewa mwaliko..

Yaan kule ukiwa hauna usafir wako binafsi ni shida yaan..
Nilienda mwaka juzi mwishoni wakiwa wanachimba msingi Hadi Leo sijawai kwenda maana ni kilometers Mingi sanaa + Mapori
Ni uhakika sister angu na mumewe wanachoma mafuta mengi go & returns zao kigamboni to posta
Posts ni karibu sana
 
Nimekaa sana Kigamboni na nimetembea sehem nyingi, sehemu kubwa ya Kigamboni ni mapori tuu, miundombinu mibovu sana, barabara za lami ni chache mno, hakujajengeka sijui kwanini watu hawajengi Kwa Kasi.

Ukitoka Mji Mwemba mpaka Pemba mnazi Kuna sehemu lami inaishia, Kimbiji ya miaka 10 iliopita na ya Leo hakuna tofauti, huko Buyuni Sasa kama mkoani, njoo Mwasonga hapo kati ni mapori tu na barabara mbovu, ukitokea kiwanda cha Nyati cement kupitia mwasonga-kibada barabara ni mbovu balaa, mvua zikinyesha hapapitiki, kuna sehemu kuna mashamba ya mpunga kunajaa maji balaa hakuna nyumba ni nyasi tuu na mapori unaweza ukasema sio Dar.

Nashangaa sana juzi nmetoka Chanika nikataka kupotea, kumbe Chanika kumekuwa mjini kabisa, nashangaa sana kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo hamna au kwakuwa wilaya mpya ndio maana inakua ya mwisho Kwa maendeleo Kwa hizi wilaya 5 za Dar??
Ushirikina mwingi na ukosefu wa maji safi na salama
 
Ukitaka ukae sehemu ambayo inakuwa haraka. Nenda sehemu ambapo watu wa kipato cha kati na maskini wanajenga.

Kigamboni viwanja vingi na maeneo vinamilikiwa na watu matajiri ambao hawana shida ya nyumba za kuishi.

Unakuta mtu ana nyumba Mbezi beach ila amenunua kiwanja Kigamboni.

Huyo mtu hawezi kujenga leo wala kesho.

Hao ndio wanachelewesha mji kukua.

Tofauti na maeneo kama Chanika maana wanaonunua viwanja ni watu wenye shida ya nyumba za kuishi. Hivyo wanajenga fasta mji unajaa
Fact
 
Kwanza mtazamo wa maendeleo kwa mtu. Inatofautiana mtu mmoja na mtu mwingine.

Kwa wale wanaoamini maendeleo ni watu kuwa wengi, mji kuchangamka, makelelele, vuruguvurugu, mara gari linapita, mara pikipiki zinakimbia, watu mara wana sherehe, vigoodoro wadada wanatikisa matako yao, mara huku bar, mara huku disko, mara singeli. Mtu ambaye kiufupi anaamini maendeleo ni amshaamsha, lazima atataka amshaamsha. Kuna wengine wanaaamini maendeleo ni huduma bora na utulivu pamoja na ukimya. Mara nyingi ni watu wenye pesa zao na wanapenda Sehemu ya kutulia na kurelax.


Sasa kwa uzoefu wangu ni kuwa bei ya viwanja ndio inaamua aina ya eneo, spidi ya kukua na kupangika. Maeneo ambayo bado watu wanauziana kwa kupima miguu na kiwanja ni bei nafuu lazima hilo eneo litakuwa na wateja wengi na kutachangamka ndani ya muda mfupi sana, ukilinganisha eneo ambalo kiwanja kimepimwa kitaalam na serikali, kwanza bei ni kwa square meters tena unaona square meter moja inacheza kuanzia 8000(porini) mpaka 30,000-50,000(sehemu iliyo na huduma) 55,000-85,000(sehemu iliyochangamka sana na yenye huduma zote na majirani wapo)

Maana yake kiwanja cha miguu 20x20 ambacho mtu anapata kwa 800,000 mpaka 1,600,000 ambayo ni bei hiyo watanzania wengi wa kawaida wanaimudu ndio kitanununulia haraka na kuendelea kwa haraka.

Ila 20x20 ikishakutana na wataalam wa ardhi waje waigeuze kuwa square meters zinakuwa 400sqm. Ambayo kwa bei ya kibosi itaanzia 4,000,000-8,000,000. Na sehemu yenye huduma itakuwa 12,000,000- 20,000,000. Sasa hizo bei za juu ndio bei za huko kigamboni. Sehemu iko porini mno ila bei milioni 20, na sasa Matajiri wao wanachukua maeneo makubwa tu kuanzia 10,000sqm mpaka 50,000sqm wengine mpaka 100,000sqm. Halafu wanakaa nayo wanatulia tena kwa bei ambazo ni highly overpriced mpaka 200m-500m. Maana yake huko kuja kuendelea bado sana. Mpaka hao Matajiri waanze kuja kuendeleza sio leo. Hawana njaa wala shida ya nyumba. Sanasana hao Matajiri wanatumia hizo hati ilikukopea hela benki ili kukuza biashara zao. Sanasana NMB na CRDB n.k.





Muda umefika serikali ikubali kupima ardhi na kuuza kwa bei nafuu kwa ajili ya wananchi wa kawaida bei ya square meters 1 iwe chini ya 2000. Masuala ya kuuza bei ya kiwanja bei juu kuanzia 10,000@sqm mpaka 50,000sqm hayasaidii wananchi.
Mkuu hizi bei za viwanja za 800,000 mpaka 1,600,000 ni za Dar?? Au unaongelea mkoa mwingine??
 
Kigamboni imekaa kushoto na Airport, maji ya Bomba maeneo mengi hakuna, mvua zikinyesha njia zahuko hazipitiki, ni mbali kwenda Magufuli Mbezi, pia usafiri wakwenda mjini ni majanga tupu Kuna Mda ferries Huwa Zina haribika na haziendi Kwa mpangilio ikifika kuanzia saa6 za usiku usafiri wahuko ni tabu tupu, kiufupi kigamboni pamejitenga watu wanapakwepa
Mkuu,
-Bunju B,Mbweni na Ununio na Silversand zipo mbali na Airport ,Bandari na Magufuli,,,

-Mbweni na Ununio, usafiri ni shida hata saa 7 mchana, na ikifika saa 2 usiku ndiyo usahau...

Kuhusu Njia kutopitika kipindi cha mvua, hiyo ni Sifa ya Dar nzima,,,Msimbazi, Kariakoo,Kawe hadi Kariakoo

Kuanzia Pugu kwenda Mvuti, huduma ya maji ni mbovu kuliko....

Watu hawajengi kisa hawana hela ya kujenga huko.
 
Kigamboni imekaa kushoto na Airport, maji ya Bomba maeneo mengi hakuna, mvua zikinyesha njia zahuko hazipitiki, ni mbali kwenda Magufuli Mbezi, pia usafiri wakwenda mjini ni majanga tupu Kuna Mda ferries Huwa Zina haribika na haziendi Kwa mpangilio ikifika kuanzia saa6 za usiku usafiri wahuko ni tabu tupu, kiufupi kigamboni pamejitenga watu wanapakwepa
Itakua kweli watu wanapakwepa, haiwezekani sehemu za wilaya ya ilala , kinondoni na temeke zilizokua nyumakabisa saiv pameendelea sana kigamboni pako vzilevile
 
Back
Top Bottom