Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Zipo tuhuma nzito Sana zinazomkabili aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga, kuhusiana na kile kinachoitwa "plea bargaining" mtindo uliobuniwa wakati wa utawala wa awamu ya 5, ambapo watuhumiwa "waliobambikiwa" makosa, wakati wa utawala wa awamu ya 5, "walilazinishwa" kukiri makosa na hivyo kukamuliwa mabilioni ya pesa, ambapo inadaiwa kuwa mabilioni hayo hayakufikishwa kwenye hazina ya Taifa hili na badala yake ziliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake!
Hizi ni tuhuma nzito Sana kumkabili mtumishi wa Umma, tena mwenye hadhi ya ujaji, Biswalo Mganga, ambapo anadaiwa kuwa Kati ya shilingi bilioni 51, alizokusanya kwa njia hiyo ya "plea bargainining" mabilioni mengi, hakuyafikisha hazina, kwa mujibu wa taarifa ya CAG, Charles Kicheere, na badala yake, mabilioni hayo yanasemekana, yaliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake.
Watuhumiwa hao waliobambikiziwa Kesi, Ili hatimaye walazimishwe kukiri makosa hayo wanayotuhumiwa nayo na baadaye "wakamuliwe" mabilioni hayo ya pesa, wametoa wito kwa Rais wetu, aweze kuunda Tume ya Majaji, kuchunguza tuhuma hizi nzito, wakati huo huo akimsimamisha Kazi ya ujaji, aliyomteua mapema mwaka jana.
Ni utaratibu wa kawaida sana, unaotumika Katika nchi za Jumuiya ya Madola, ambayo nchi yetu ipo, ambapo tunalazimika kufuata.
Swali kubwa ninalojiuliza, ni kwanini hadi hivi sasa, Rais Samia, anashikwa na "kigugumizi" kuunda Tume hiyo ya Majaji, ambayo itatafuta ukweli wa kujua kama tuhuma hizo ni za kweli au la?
Ni vyema Rais Samia, akatambua kuwa kushikwa kwake na "kigugumizi" cha kuunda Tume hiyo ya Majaji,, kutatoa tafsiri kwa wananchi wengi kuwa, yeye Rais ana mpango wa kumwewekea kinga dhidi ya tuhuma anazokabiliwa nazo huyo aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga.
Vile vile itatoa tafsiri kuwa kuna baadhi ya watu hapa nchini, hususani viongozi waandamizi wa Serikali hii ya CCM, wanapewa kinga ya "impunity" ya kutoshtakiwa, hata kama wamefanya makosa makubwa ya jinai, jambo ambalo halitendi haki kwa wananchi, kwa kuwa Katiba yetu inaeleza wazi kuwa wananchi wote, wapo sawa mbele ya sheria.