UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 3,101
- 14,248
Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane!
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka Kwa Wananchi ya kwamba,Vyombo vyetu vilivyopewa dhamana ya kuwatetea wananchi Kwa Mujibu wa Katiba Sheria havifanyi hivyo,badala yake vinaendelea kulinda maslahi ya wanasiasa walioko Madarakani huku wananchi wakiendelea kuumizwa,kuteswa na kunyanyaswa!
1.POLISI
Hii ni Idara ya Usalama wa mambo ya ndani ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi Kwa muda mrefu sana tangu tumepata Uhuru hadi Leo,Ajabu ni kwamba,Viongozi wakubwa wa Idara hii ya Usalama pamoja na kulalamikiwa na Wananchi,imekuwa ikijifungamanisha na Vyama vya sisasa,hasa Chama tawala Tanzania tangu tupate Uhuru (CCM)
Kwa Mujibu wa Sheria hii Idara inapaswa kuwalinda Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mali walizo nazo!
Ajabu ni kwamba,wao ndiyo wamekuwa wakilalamikiwa Kwa Kuuwa Raia na kugandamiza Haki za Raia wa Tanzania pasipo sababu za Msingi!
Je,ni sababu zipi zinawafanya wao Kuwa na upande wa kisiasa wakati Sheria na Katiba imewakataza?
Ni kitu gani kifanyike Ili kuzia Hali hii?,Ni lini Unadhani Watanzania wataanza Kuwa na Imani na Idara ya hii ya Usalama?
Halafu pia nadhani Hawa watu wanapata Kiburi Kwa kuitwa "Jeshi la Polisi",Hawa watu wahapaswi kuitwa "Jeshi" wanapaswa kuitwa "Idara"
2.MAHAKAMA
Kwa Mujibu wa Katiba na Sheria,Mahakama ndicho chombo Cha juu Cha Nchi ambacho kinapaswa kusimamia Haki ndani ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Ajabu ni kwamba,hata Mahakama nazo zimeshakosa kuaminiwa na wananchi kwasababu ya kujiingiza kwenye mambo ya siasa!
Nchi nyingine zote zenye Demokrasia,Mahakama ndo huwa chombo Cha juu Cha Haki ambacho wananchi hukikimbilia,Mahakama huponya nafsi za wananchi wake,Mahakama huponya mioyo ilipondeka ya wananchi wake,Mahakama huwa upande wa wananchi mara zote dhidi ya Serikali katili,Mafisadi na wauaji!
Hapa kwetu Tanzania hili ni tofauti kabisa,Mahakama ndizo huwa mstari wa mbele kuona watu(wasiokuwa na chochote) wanakosa Haki zao Kwa kukandamizwa!
Kibaya zaidi kila Mtanzania anaelewa kabisa bila ya Kuwa na chochote Huwezi kupata Haki hata kama Haki Iko upande wako!
Tumeshuhudia wanasiasa hasa wa Upinzani (CHADEMA) wakiwalalamikia Majaji kadhaa ambao inaonekana kabisa ni wafuasi na wanachama wa Chama Tawala lakini hakuna hatua zozote za kinidhamu zinazochukuliwa dhidi Yao!
Je,Kwa mantiki hiyo kutakuwa na Haki?
Je,Nini kifanyike kuondoa Hali hii?
Je,Hayo Maridhiano ambayo Serikali ya Rais Samia imepanga kuyafanya itaondoa mambo haya?,Au hakuna lolote litakalofanyika?
3.IDARA YA USALAMA/JESHI
Idara ya Usalama pamoja na Jeshi ni Idara nyeti ambazo hazipaswi kabisa kujifungamanisha na upande wowote wa Siasa,lakini hapa Kwetu Tanzania imekuwa tofauti kwasababu ya Maslahi binafsi ya wanasiasa!
Juzi wakati Raisi Samia anaapa Kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisikika akisema ya kwamba,Kuna watu wameingia nchini Tanzania Ili kufanya Vurugu,Lakini hadi Leo hatuambiwi na kuelezwa hao watu baada ya Uchaguzi wamechukuliwa hatua gani,Badala yake tunaona maelfu ya Watanzania wenzetu wakifunguliwa mashitaka ya Uhaini & Ugaidi dhidi ya Serikali!
Je,Ilikuwa ni Taarifa ya uongo kuhusu wananchi wa nchi Jirani kuingia nchini na kufanya Vurugu?,Je,Ilikuwa na dhamira gani kudanganya umma?
Je,Hatuoni kama ndivyo,Jeshi la Wananchi wanaopaswa kulinda mipaka ya nchi na Idara ya uhamiaji (Jeshi) wameshindwa kabisa kulinda mipaka ya nchi na Uhamiaji haramu?
Je,kama ndivyo,Hatuoni tukiwa na Uhasama wowote ule kutoka nchi Jirani itakuwa rahisi kupenyeza vikundi vya Kigaidi?
Maswali ni Mengi lakini Je,Je,Je,Je,Je,Je, haziwezi kuisha!
Je,Kama ndivyo Tunapaswa kufanya Nini kama Taifa?
4.AJIRA
Ajira nyingi kwenye nchi hii zinazolewa kisiasa,ni lazima uwe na Koneksheni ndipo upate nafasi nzuri au upate kazi serikalini(Hili liko wazi na Wala si SIRI)
Watanzania wanasoma,wanapata Uzoefu na hakuna wa kuwaajiri,wanaajiriwa watu ambao hawana Ujuzi wowote ule!
Ishu hapa ni lazima uwe na Koneksheni,eidha kutoka CCM au Serikalini?
Je,Hali hii itaendelea hadi lini?