Watu wengi wanashauri uende sehemu fulani pesa ipo ila hawasemi mshahara ni shilingi ngapi, extra duty allowance ni kiasi gani, hawazungumzii safari, per diems, honorariums, bonuses, special tasks etc na hii inakua ngumu kulinganisha.
Watu wanaofanya kazi kwenye taasisi husika wakwambie:-
Mshahara ni shilingi ngapi, posho ya nyumba na usafiri, per diem ni sh ngapi na safari ni nyingi kiasi gani. Mfano, mkisafiri nje ya kituo cha kazi hua ni kwa siku ngapi na per diem ni kiasi gani. Pia overtime allowance ni sh ngapi na hua inalipwa mapema kiasi gani?
Kwa mtazamo wangu, kama mshahara unazidi 3 M, Housing and Transport Allowance inafika 700k, per diem ni 150k na safari za nje ya kituo hua ni 2 weeks angalau 6 times a year na overtime inafika 40k per day na wanalipa fasta tu baada ya kuclaim, hiyo sehemu ni nzuri kwenda.
Kama kuna taasisi yoyote hapo juu ina hizo benefits, basi nenda. Kama hakuna, nenda zako TCRA ukale maisha.