Ni hatari, Waziri jangili huyu hapa

Ni hatari, Waziri jangili huyu hapa

Zitto sio mbunge wa Kanda ya Ziwa yupo wazi aliisemea hela ya uswis mbunge wa kanda ya ziwa aliyekuwa anamuunga mkono Zitto,tumuache Zitto apumue
Ni nani sasa? Hii nchi kuna kanda za Maziwa mangapi?
 
Haya ni mauwongo makubwa kabisa imagine waziri anakutwa na pembe za ndovu, hii itakuwa balaa ya mwaka. Na huyo waziri sijui atakuwa wa namna gani!! Maana kuna makosa hata mwehu hawezi fanya ndio hili.

Jamaa waache kumsingizia Waziri wetu.

Lazaro Nyarando aliwahi kukutwa na meno ya tembo,akarushia watu risasi huko huko singida.
 
Hawa jamaa mwaka 2005 ndo walitumika kuchafua wagombea wengine. Walisema Salim na genge lake walimuua Karume na wakasema Sumaye ana mabilioni mengi aliyokwiba... Baada ya baba Riz kuingia mjengoni mmoja wa waandishi wao akawa mwandishi wa ikulu... Walipoona gazeti lao haliuziki tena wakamuuzia Rostam ndo wakaenda kuanzisha Raia Mwema. Kazi naona imeanza tena...
kuna tofauti kati ya rai na raia mwema hata kama yote ni magazeti
 
wizara nyeti ni ya fedha na anayetoka singida kwenye hiyo wizara ni serial killer mwigulu nchemba,..
 
Haya ni mauwongo makubwa kabisa imagine waziri anakutwa na pembe za ndovu, hii itakuwa balaa ya mwaka. Na huyo waziri sijui atakuwa wa namna gani!! Maana kuna makosa hata mwehu hawezi fanya ndio hili.

Jamaa waache kumsingizia Waziri wetu.
siku atakayomlala mkeo na wewe kulala sero ndio utayajua magamba vizuri!
 
Lakini kuna mtu aliwahi kamatwa na pembe za ndovu kwenye gari na kulikuwa na majibishano makali kati yake na officer wa TRA. Huyo mtu sasa hivi ni waziri na ni waziri wa wizara nyeti.
 
Anatembelea Singida,analala katika Hoteli ****,amekabidhiwa wizara nyeti hivi karibuni (Presumably ya senti senti na chenji kidogo).
Huyu atakuwa naniiii aah naniiii.Loh jina limenitoka tena.

You are intelligent! very intelligent. this must be a certain chamber in the ministry of finance!! yes an arrogant minister.
 
Yule huwa hamung'unyi hata kidogo. Akiweka hadharani habari basi anaweka kila kitu bila kubakisha hata kiduchu hata msomaji unaposoma habari hiyo unaielewa A to Z. Nakumbuka kwa mfano ushahidi aliouweka kwenye gazeti la ----------- kuhusiana kutekwa kwa Dr Ulimboka habari ambayo ilisababisha gazeti lake kufungiwa ushahidi ule ulikuwa umejitosheleza.
Yaani mpaka Ikulu walishindwa kujibu ikawalazimu wafungie gazeti.!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kwani nyarandu si alikuwa waziri toka zamani? maana habari inasema aneteuliwa baada ya mabadiliko ya juzi juzi hapa
Nyalandu alikuwa naibu waziri. Ameteuliwa juzi kuwa waziri kamili baada ya Kagasheki kujiuzulu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Haya yatakuwa yale yale majungu kwa Katibu Mkuu wa CCM. mbona majina yamehifadhiwa , majina yamehifadhiwa, majina yamehifadhiwa , kwa nini?
Raia Mwema imeshawapikia. Sasa mnataka iwatafunie na kuwamezea vile vile?
 
Mkuu Jasusi nimefurahi kukuona, siku hizi unaonekana hapa kwa nadra sana. Tunakosa hekima na busara zako katika jukwaa hili. Natumai umzima kabisa wa afya....Walikuwa hawana cha kujibu maana details zilizowekwa zilikuwa ni za hali ya juu Mkuu. Kubenea mwache aende zake.

Yaani mpaka Ikulu walishindwa kujibu ikawalazimu wafungie gazeti.!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Jasusi nimefurahi kukuona, siku hizi unaonekana hapa kwa nadra sana. Tunakosa hekima na busara zako katika jukwaa hili. Natumai umzima kabisa wa afya....Walikuwa hawana cha kujibu maana details zilizowekwa zilikuwa ni za hali ya juu Mkuu. Kubenea mwache aende zake.
BAK
Na mimi nimefurahi kukuona. Nilikuwa na majukumu narudi nyumbani usiku nikiwa hoi bin taabani. Najua nimekosa uhondo mwingi sana hapa JF. Lakini kwa sasa nitakuwepo angalau kwa muda.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mawaziri wote wa ccm mbona wote ni majangiri

CCM = Chama Cha Majangili hivyo ni kawaida yao kufanya uhalifu bila kuhukumiwa kwani wanalindwa na mtandao wao (CCM). Si umeona Kinana ni kibaka badala ya kumkamata na kumnyonga wamemuongezea ulaji na majukumu ya kutembea vijijini kugawa ugali bure katika makongamano ya udanganyifu kwa wananchi.
 
Sawa Mkuu nafurahi kufahamu hivyo.

BAK
Na mimi nimefurahi kukuona. Nilikuwa na majukumu narudi nyumbani usiku nikiwa hoi bin taabani. Najua nimekosa uhondo mwingi sana hapa JF. Lakini kwa sasa nitakuwepo angalau kwa muda.
 
Kwa hali ya Tanzania ilivyo ukiona hivi huu ni mkakati wa makusudi wa kuondoa mijadala muhimu kama masuala ya IPTL n.k taarifa hii imeandikwa kwa lengo la kupotosha umma na kuhamisha attention ya watu kujadili mambo yasikuwa na miguu wala mikono. Intelligensia ya wapi inaweza kufanya yote hayo na matokeo yake ni kwenda kuandika kwenye gazeti so what? Taarifa imeandikwa kwa namna ambayo kila mahali kuna ushaidi, lakini inaacha maswali ya nini kilichofanyika, je walitaifisha meno, bunduki au kuwatia kuzuizini wote waliokamatwa? labda mwandishi wa habari hii atupatie kwa muhutasari lengo na madhuni ya kuandika taarifa hii yenye mapungufu makubwa nini hasa?
 
Jina lake Waziri jangili na bado Mkuu wa nchi ambaye alishinikizwa na Wabunge wa chama chake kubadili baraza la Mawaziri jina lake halikumshtua na akaamua kumteua katika baraza jipya la Mawaziri na kumkabidhi Wizara nyeti!

Yawezekani ni ule usemi wa mwana mpe mchawi akulelee
 
Lakini kuna mtu aliwahi kamatwa na pembe za ndovu kwenye gari na kulikuwa na majibishano makali kati yake na officer wa TRA. Huyo mtu sasa hivi ni waziri na ni waziri wa wizara nyeti.

Au unamuongelea waziri aliyeoa former miss Tanzania? Huyu nae alibeba meno ya tembo, aliposimamishwa kwenye gei la ukaguzi wa mazao ya maliasili alivunja geti na kuendelea na safari yake. Nae ni waziri wa wizara yenye ulaji sana, mpaka muda huu.
 
Back
Top Bottom