Ni hatari, Waziri jangili huyu hapa

Ni hatari, Waziri jangili huyu hapa

Nyalandu aje atuweke sawa kwenye hili
 
Haya ni mauwongo makubwa kabisa imagine waziri anakutwa na pembe za ndovu, hii itakuwa balaa ya mwaka. Na huyo waziri sijui atakuwa wa namna gani!! Maana kuna makosa hata mwehu hawezi fanya ndio hili.

Jamaa waache kumsingizia Waziri wetu.

Marehemu Lawrence Gama aliyewahi kuwa mkuu wa usalama wa Taifa na hata mkuu wa mkoa wa Ruvuma alikuwa anahisiwa kuwa alikuwa na mtandao mkubwa sana wa kijangili akiwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma; kwavile kama mkuu wa mkoa yeye ndiye huongoza usalama wa mkoa haikuwa rahisi vyombo vya usalama kuwakamata vijana wake aliokuwa anahusiana nao kufanya uhalifu huo wa ujangili; hivyo wakuu wa usalama mkoani walimtegea alipokuwa nje ya nchi kwa safari za kikazi ndipo walipowakamata vijana waliokuwa kwenye mtandao wake akiwemo Mbunge wa Songea mjini wa wakati huo akiitwa Ali Abdurabi!!! Gama aliporudi alikuta vijana wake wametiwa hatiani na hakuweza kuwasaidia. Incidentally, katika kesi ile prosecutor alikuwa marehemu mke wa John Malecela mwanasheria mama Ezelina Mwaipopo. Viongozi wa magamba hata wakiwa wabunge au mawaziri ni wezi tu!!!
 
Hapana........hii habari ni ya kichunguzi hivyo si vema kuweka majina kabla ya kuridhika nayo. Ila aya hii inaweza kukupa mwanga ni nani huyo waziri


kuna haja gani ya kukimbilia kuandika/publish habari- tena unayoiita investigative report -kama hawana uhakika nayo?

badala ya kutupa mwanga kama unavyofikiri imetupa platform kueneza mjungu,hisia,fitna....
 
Kama siyo jangili, basi wewe lazima utakuwa kwenye kundi linalohusika na ujangili. Habari hiyo, imeandikwa kwa weledi mkubwa ili kutokiuka sheria kandamizi ya habari iliyopo sasa.

Well me call any name, ila ukweli unabaki pale pale tunaendeleza taifa la wasema hovyo, kama unaushahidi wa kutosha kama ilivyoainishwa na umejizatiti kwa kuzunguka mikoa yote why uogope sheria kandamizi? uko wapi ujasiri uliokufanya ukachunguze? hakuna jinsi tunaweza kulitoa taifa letu hapo lilipo kwenye ukandamizi kuwa kuwa waogo siku zote na kukimbilia magazeti. Kipi kilichoogopwa wakati waziri anayesemwa amekanusha?
 
Akina Jenerali Ulimwengu si watu wa Membe?Mbona sasa wanaipiga mabomu kambi yake au tayari wameshindwa kuafikiana mshiko
 
Akina Jenerali Ulimwengu si watu wa Membe?Mbona sasa wanaipiga mabomu kambi yake au tayari wameshindwa kuafikiana mshiko
Sio Nyalandu... amini usiamini, ukiichambua vizuri hiyo habari utamfahamu muhiska na wala huwezi kumdhania!!!

Hapa nakupa highlights...
  • Kama walivyosema Raia Mwema, huyo Waziri ameingia kwenye baraza kwa mara ya kwanza na sio kwamba amepandishwa kutoka unaibu.
  • Ni Waziri kutoka Mkoa wa Mwanza (ile Mwanza Original, manake sifahamu huu mgawanyo wa sasa)
  • Huyo Waziri amewahi kufanya kazi TANAPA
  • Nasema hivi, huwezi kumdhania hata punje!!!
  • Huyo waziri, title yake ni Doctor (I think by professional rather than PhD)
 
Kwani aliekabidhiwa Wizara hii nyeti hivi karibuni hatumjui. Wanajamvi ni kweli Waziri aliekabidhiwa wizara hii hamumjui? Kama mnajua basi huyo ndio Jangili.
 
hii dili profitable sana eeehh...?? huku kwetu tembo wanazama kwenye tope na tunawatoa kwa scavator salama salmin! ingekua huko kwa kina mh wazir report ya kuuwawa kwa tembo ingeongezeka...!
 
Wana-JF bhana... yaani nimewarahisishia kwa 75% lakini hamjamjua tu?! Ewe mheshimiwa kutoka Mkoani Mwanza, nimeshakujua, nipe changu vinginevyo na-drop jina lako hapa hata kama moderators wataondoa angalau watu 10 watafahamu... Najua kv Raia Mwema hawajakutaja, basi hivi sasa utakuwa unahangaika kufanya nao biashara... nikumbuke na mimi vinginevyo namwaga mchele...
 
Taja jina ,hatutaki ubabaishaji wa CCM hapa,au umesahau?
 
Back
Top Bottom