Ni hatari, Waziri jangili huyu hapa

Ni hatari, Waziri jangili huyu hapa

Aiseee!
Hivi kumbe!!!!!
Kwa vyovyote vile huyu waziri ni Mamndeyi. Maana ndiye waziri mwenye kuiongoza wizara nyeti hapa JF, na aliteuliwa uwaziri awamu ya mwisho. Chonde chode baada ya kukutaja usije ukaning'oa kucha meno bila ganzi.
 
Nchi ya wajinga huishi kwa minong'ono na staili fulani ya umbeya,

Mtu unamjua kabisa Nyalandu ama Kinana ni majangili, lakini kwenye kigazeti chako unaandika "jina linahifadhiwa", pumbaaaafu! Kama hutaki kutaja jina kwanini ulete habari hiyo? Yani unatufanya wasomaji tuanze kutabiri?

kwani nyarandu si alikuwa waziri toka zamani? maana habari inasema aneteuliwa baada ya mabadiliko ya juzi juzi hapa
 
Inaudhi sana hii kitu, kama wana ushahidi kiasi hiki kwanini wasianike kila kitu hadharani? Raia Mwema najua baadhi yenu mnapita huku badilikeni katika uandishi wenu ili mkiamua kuandika habari ya ufisadi/ujangili au rushwa basi muweke kila kitu hadharani.

Labda tumkamate huyu mleta taarifa tumpeleke mabwepande
ndo atatoa majina yote ya hawa mawaziri majangili.

 
Gazeti kama gazeti wamefanya yao tayari! !!!!!

Huu sio uchunguzi wa mwandishi hata siku moja, "hii ni kazi" na imefanywa na "WATU" sasa hawa walioandika lazima wamepewa conditions za kuandika, ndio maana ile "sheria" ikirudi mengi yatakuwa yanawezekana sababu hapa ingekuja repoti na kazi ingekuwa saa hizi iko mwishoni lakini mchagua mchele sio mpishi so hata mkilaumu chakula sio kitamu yeye hana la kufanya!!!!

Katiba ina mengi ya kusaidia kuliko idadi ya serikali ila wanaelekeza mjadala huko makusudi ili pingu zibaki wazi waingize mikono na kutoa bila kubanwa!!!!
 
Ukiona Habari imeandikwa kwa "MFUMO HUU"Ujue Wametega MAZINGIRA YA RUSHWA,YALE YALE KAMA YA Zitto.WAITWE WAPOZWE.F**CK
 
Last edited by a moderator:
naona na wanajf tunaendeleza uzembe uleule wa raia mwema, kwa nini wasitajwe hao mawaziri wageni halafu wapigiwe kura.?

1.juma nkamia
2.mwigulu mchemba
3....
4....
Wadau endeleeni kutaja wengine mwisho atafahamika tu
mi simung'unyi ni lazaro nyalandu jamani hamjui hata kuangalia picha....?
 
Ngoja nifuatilie kujua waziri gani ni rafiki wa Kinana katibu mkuu. Nitarudi
 
Mkuu wanafanyia karibu watumishi wote kwenye idara nyeti. Sema ndio ukishaingia kwenye network unakuwa mwingine. Muda mwingine hata kama hafai anaingizwa na wakubwa kwa ajili ya kutumika.
Kuna haja sana ta kuweka madaraka ya raisi au serikali mbali na taasisi za ulinzi.




The king.
Uko sawa, mchele ukiambiwa chagua kazi yako ni kuchagua nabkutenganisha mchele na vinginevyo then mchele unaingizwa jikoni,ikitoka pilau au uji wa mchele kazi sio yako tena!!!!

Katiba ndio dawa ya hii tabu!!!
 
Mimi nashangaa maana hii stori kama imetolewa na usalama wa taif vile, kwamba wameshapeleka ripoti kunakohusika lakini hakuna hatua iliyochukuliwa.

Mleta mada atuambie kama baadae atatujulisha wahusika au ayapeleke polisi ili waifanyie kazi hii taarifa. Kwa hii mada tumeona kuwa ujangili wa meno ya temba bado upo na unafanywa na viongozi walio serikalini. Sasa kinachoshangaza bunge lipo (hata kama ni la CCM) na mahakama ipo sasa kulikoni? Nchi inaangamia kwa wananchi wake kulala usingizi. Tuliowapa madaraka ndio wanaiangamiza nchi sasa tufanyeje? Tujadili wanamtandao!
 
kaka hiyo inatokana na kanuni za kiuandishi,lazima umuhoji kwanza mhusika akikujibu ndo unataja jina,bila kusikiliza upande wake wa stori,utaonekana umevunja maadili ya kiuandishi,na sababu nyingine labda wasije wakaharibu uchunguzi,ila kwa mwenye kung'amua atajua wahusika.

Hawa waandishi wa tz hawasimamii kanuni zao kabisa, I am a victim ya uandishi bila confirmation na jambo lenyewe halikuwa la kweli. Wandishi wengi kuvunja maadili haiwapi shida ndio style yao ya kazi. Hata huyu sintoshangaa hata kidogo kama hatafuatwa na kupoozwa ili asitoe majina ya wahusika. Uandishi wa aina hii unaudhi sana kwa kweli.
 
Ngoja nami niwasiliane na Manyoni tupate jina la Waziri ambaye anaonekana mara nyingi hapo bila kujulikana rasmi ratiba ya kazi zilizompeleka. Nikumjua nitamtaja mpaka hao washirika wake. Kudadeki tumechoka na "jina limehifadhiwa"


Sent from my iPad using JamiiForums
 
km namwona Zitho kabwe....loading....

Hata mimi naona kama kuna Nyalandu na maestro Zitto. Hawa jamaa matajiri na wapo close na mkuu wa nchi ndiyo maana hawachukuliwi hatua! Unafikiri mkuu hajui? Tz ni moja ya nchi yenye the best intelligence system in the world!!
 
Huyu kiumbe hafai kabisa kufichwa fichwa. Inatakiwa atajwe wazi, wananchi wamtambue na ijulikane kama huyo aliyemteua alifanya huo uteuzi kwa makusudi maalum ama alifanya pasipo kujua. Inavyoonekana ni wazi kuwa ujasiri wa kufanya hiyo shughuli umeghubikwa ama una Baraka zote za mamlaka ya juu.

Nakumbuka mwaka jana kama sijakosea kuna lori lilikamatwa na maofisa wa maliasili likiwa na shehena ya mbao kutoka huko huko Singida lakini ilitolewa amri kutoka kwa waziri mmoja kuwa liachiliwe haraka. Yawezekana kabisa kuwa waziri aliyetoa amri ndiye huyo huyo anahusika kwenye biashara ya ujangili.

Watawala wanapokuwa wezi na wahujumu wakuu wa rasilimali za nchi, wananchi wafanye nini ili kulinusuru taifa lao?
 
Inaudhi sana hii kitu, kama wana ushahidi kiasi hiki kwanini wasianike kila kitu hadharani? Raia Mwema najua baadhi yenu mnapita huku badilikeni katika uandishi wenu ili mkiamua kuandika habari ya ufisadi/ujangili au rushwa basi muweke kila kitu hadharani.
Uchunguzi haujakamilika! Magazeti yanaandika ili kumfanya mhusika aelewe kuwa habari zake zinaanza kujulikana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom