Bana likasi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2020
- 6,927
- 6,417
Uchaguzi mwezi October we hofu yako nn,maandalizi yaendelee Kama kawaida vipi Kama ugonjwa ukiisha kabla ya mwezi wa kumi je.Uchaguzi ni Jambo kubwa na muhimu katika nchi ni sawa na familia kupata mtoto mpya.Zipo njia nyingi hata kwa simu itatengenezwa App ya uchaguzi tutapiga.Huu ugonjwa ni mitihani ya Mwenyezi Mungu kutuonyesha sisi wanadamu si lolote si chochote hasa hao watu weupe kuwarudisha kwenye mstari wajue kwamba Mungu yupo thus kwenye machafu umepiga Sana kama wameacha asili na kufikia kuoana jinsia moja bila kuwapa adhabu watarudi vipi kwenye mstari.Bora mengine yahairishwe na sio uchaguzi.Dunia nzima inapita katika kipindi kigumu sana kisiasa, kiuchumi na kijamii. Shughuli zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa zinafanyika kwa ugumu sana. Tumeshuhudia shule zikifungwa, ndege haziingii wala kutoka, utalii ukisimama mabisa, biashara zikidorola, hofu ya ugonjwa na matumaini ya maisha kiuchumi unatawala miongoni mwa Watanzania.
Wakati haya mabadiliko makubwa na hatari yanatokea sisi tunataka kubadilisha baba au kiongozi mkuu wa nchi hii ni hatari sana kwani uchaguzi pekee ni hatari hasa katika uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi. Kwa mfano kama tupo safarini katika basi na gari likianza kuyumba huwa tunajishikilia katika viti au machuma maalumu katika gari sasa itakuwa ujinga kwa watanzania wakati dunia inayumba sisi pia ndani tunajiyumbisha badala ya kujishikilia eti kwa sababu za kisiasa, naomba hekima sasa itumike.
Ninawaasa wanasiasa wenzangu na wadau wote tumuweke Mungu mbele hakuna wakati wa kuwa kitu kimoja kama kipindi hiki cha janga hili la Korona kwani tukivuka salama ni rahisi kurudi katika maisha ya kawaida. Napenda kukiomba chama tawala kubadili misimamo yakekuelekea uchaguzi mkuu 2020 kwani usalama wa taifa zima ni muhimu kuliko uchaguzi wa Raisi. Inamaana gani anachaguliwa Raisi mwingine anaingia madarakani wakati nchi iko ziii hakuna ndege inayoruka, hakuna biashara, hakuna utalii, shule zimefungwa, watu wamefungiwa ndani hii haina maana. na kama kunamtu anataka pia kugombea uraisi kipindi hiki basi huyo anauchu wa madaraka au maslai binafsi au ni maslahi kikundi cha watu wachache. Stabiliti ya nchi kisiasa ni muhimu sana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote.
Naomba Chama Cha Mapinduzi, Chadema, CUF, ACT wazalendo, NCCR Mageuzi na vingine kunahaja ya kukaa pamoja na kuweka sawa jambo hili kwa manufaa mapana ya taifa letu, nashukuru nilipata kuonana na mmoja wa kiongozi wa chama alionyesha kukubaliana na hili naye aliniambia kwa masilai yake binafsi na chama chake halipendezi lakini kwa maslai mapana ya taifa linafaa.
Nimeamua kuwaandikia barua wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi, Chama Cha Democrasia na Maendeleo, Civil United Front, NCCR Mageuzi, ACT wazalendo hili mkubaliane na hekima itumike hasa katika kipindi hiki kigumu cha janga hili la corona duniani, wote kwa umoja wetu tukubaliane kwa maslai mapana ya taifa hili, na ndugu yetu Joni Pombe Magufuli aendelee ili atuvushe katika hiki kipindi cha hatari.
Nawasilisha
Daza Ndaga 0714 733 111