Ni habari lakini hazifunguki - Sakata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni habari lakini hazifunguki - Sakata

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwiba, Nov 22, 2008.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Denti wa Mama JK ajazwa mimba

  Mhe. Mungai alipuliwa

  Sorce Ippmedia 22/11/2008

  Kama kuna mtu ameweza kupata makala hayo na kuyasoma atuwekee ili tujue yaliyojiri katika habari hizo ukienda kwenye ippmedia utaona hazifunguki, very interesting
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Denti wa Mama JK akijazwa mimba nayo ni breaking news? Kwa hiyo ukiwa denti wa mama JK ni marufuku kuzaa? Maana huwezi kuzaa kama hujapata mimba!

  Hizi alasiri news.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Da nilizani wamepita na kuvuluga kwa Mh.laisi kumbe ni mfazili tu,hawa waandishi wanazidi kukosa adabu.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Shame mnafikkiri mnazaa wenyewe!!loh
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Unamaanisha nini unapoandika
  1. Nilizani
  2. Kuvuluga
  3. Laisi
  4. Mfazili
   
 6. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kiswazi hakijakaa fresh
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,178
  Trophy Points: 280
  Mhe. Mungai alipuliwa

  2008-11-22 16:55:39
  Na Emmanuel Lengwa, Jijini

  Wakati vuguvugu la kufichua watu wanaojihusisha na ufisadi nchini limepamba moto, mbunge mmoja wa CCM, amejikuta akilipuliwa kwa kudaiwa kuwa naye ni fisadi mkubwa.

  Mheshimiwa aliyerushiwa kombora hilo la kufungia mwaka, ni Bw. Joseph Mungai ambaye ni mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

  Tuhuma hizo za kifisadi dhidi ya Bw. Mungai zimetolewa na Bw. Renatus Mkinga wakati akichangia mada kwenye kipindi cha Kipimajoto, kilichorushwa `live` na kituo cha luninga cha ITV jana usiku.

  Akizungumza kwa kujiamini, Bw. Mkinga alidai kuwa wakati Bw. Mungai akiwa Waziri wa Elimu na Utamaduni wa serikali ya awamu ya tatu, ulitokea wizi wa fedha zaidi ya shilingi bilioni tatu , mali ya wizara hiyo.

  Akadai punde tu wizi huo ulipotokea, mfanyakazi mmoja wa Wizara hiyo ambaye Bw. Mkinga hakumtaja jina, aligundua na kutoa taarifa kwa Mungai ili hatua zaidi zichukuliwe.

  Bw. Mkinga alizidi kudai kuwa badala ya Waziri Mungai kufuatilia taarifa hizo, alikanusha vikali kuwa hakuna wizi uliotokea na kuchukua hatua kali za kumtimua kazi mfanyakazi huyo aliyebaini upotevu wa fedha.

  Akadai kuwa hata hivyo ukaguzi wa kina ulipofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ikagundulika kuwa fedha hizo zaidi ya shilingi bilioni tatu zilikuwa zimeibwa wizarani hapo.

  Bw. Mkinga alidai kuwa anashangaa kuwa licha ya ukweli huo kubainika, Waziri Mungai hadi sasa bado hajakamatwa na wala mfanyakazi aliyefukuzwa kazi kwa kutoa taarifa hizo za upotevu wa fedha hajarejeshwa kazini.

  ``Naomba nitumie fursa hii kuiomba Serikali imrejeshe kazini kijana huyo, na kumchukulia hatua Mungai, nadhani hata yeye ni fisadi,`` akasema Bw. Mkinga.

  Kipindi hicho ya Kipimajoto kinachorushwa na ITV `live` kila Ijumaa, jana kilikuwa kikijadili mada ya nini kifanyike kupata suluhu ya migomo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

  SOURCE: Alasiri
   
 8. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mi naona nyuzi hii ipelekwe kuleee kwenye Jokes na utani......
   
 9. S

  Sabri-bachani Member

  #9
  Nov 22, 2008
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Khaa. huna mpya. Umerishai!!!!!!!
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135

  Utani ni nini?

  Kama habari hii ni utani, nadhani kila kitu tunachoongea ni utani.
  Kuna masawali mengi ya msingi ya kujiuliza kuhusu tuhuma hizi kuliko kutoa maoni ya kuipeleka habari kwenye utani.

  Labda sielewi, utani kwenye habari hii uko wapi? Naomba nielekezwe.
   
 11. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama utasoma kichwa habari na muandishi mwenyewe alivyoanza ndio utaona, au kama ukii-edit na kuweza kuiweka kwenye hadhi ya kujadilika seriously then itastahili kuwa hapa.....Hebu wewe angalia mwenyewe muanzishaji alivyoandika...
   
 12. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  leo nimeamini kweli wewe ni mwiba.......................
   
 13. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Jokes? Utani? ur serious? Mtu kasema ukweli kafukuzwa kazi. Two Billion zimeliwa na ikathibitishwa hivyo na Mhusika mkuu bado anapeta mtaani, Wanafunzi wetu shida kila kukicha acha hizo bwana Mizengwe
   
 14. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135



  Anayedhani watanzania ni wakimya au hawana ujasiri, na afikiri tena. Hicho kipindi cha Kipimajoto kilikuwa moto sana. Big up kwa mzee Renatus Mkinga. Nakuombea uzima, naamini huko uliko uko salama salmin. Bila shaka huenda tukakusikia tena wakati mwingine - utushushie DATA zaidi.







  .
   
Loading...