Fahari ya Kijana ni Nguvu zake mwenyewe (Mithali 20:29A)
Nimehuzunika sana na yale niliyoyashuhudia Juzi weekend kupitia Kituo Cha TBC ambacho kilirusha tukio la watu waliojiita Vijana wa CCM wa Vyuo Vikuu. Nieleze mapema kuwa hata mimi niliwahi kunasa kwenye mtego huo na tukaishabikia sana CCM kwa kupitia tawi la Abijani( kamwe sijui hata ofisi zao zilipo)
Lakini, enzi zile information ilikua so limited, vijana wa sasa wana kila information kila dakika na kila mahali, wanajua yanayoendelea nchini, wanaujua ukweli wa serikali hii kuwa si sahihi hata kidogo yale yanayotokea. Inflation inaongezeka kila uchao, ubabe wa kitoto wenye kuangamiza kizazi chetu unaongezeka kila uchao.
Tunategemea kuwa Vijana ambao wana nguvu, ambao wanaujua ukweli wa familia zao zinavyoteswa na serikali, waliosoma kwa shida sana, walikosa hadi mkopo na baadhi yao wakapata eti mkopo wa asilimi tano (5%) tulidhani wangesimama na kukataa uonevu huu kwa vitendo lakini matokeo yao vijana hawa wamekua mstari wa mbele kushabikia mambo haya.
Chagueni lililojema Mkaishi
Nawakumbusha Vijana mna safari ndefu, msikubali kupoteza nafasi hii ya kuibadilisha nchi yenu kwa faida ya watoto wenu na watoto wa watoto wenu.