Ni Aibu Vijana Kuishabikia CCM

Ni Aibu Vijana Kuishabikia CCM

Mkuu, hivi kingunge ni mtaalam kweli au vipi ? Maana mpaka leo sijaelewa kwanini masogange aliachiwa aisee !

Mpwa umeshasahau? Ni kweli na yeye ndio muwakilishi wao that means na yeye ni mtaalam
 
Kwanza inabidi upewe pole kwa upeo wako mdogo wa wazua mambo vijana siyo mbugila kwama wewe kiasi kwamba unaweza kuwadanganya kirahisi wakafuata mawazo yako ya kibavicha nchi yetu chini ya ccm imepiga hatua kubwa na kuwa kioo kwa mataifa mengine katiba mpya imeweka baraza la vijana ili vijana wawe na sehemu ya kusemea wakati chagadema kijana haruhusiwi hata kuhoji tu.

Akihoji tu anafukuzwa
 
Duh naona uzi wangu umekuna ajira zenu, mkaamua mtafutane mje hapa, karibuni Sana, nyie wote nawamudu, ndio nimeshamaliza kuongea kuwa NI UJINGA NA AIBU KWA VIJANA KUISHABIKIA CCM:-/ KAMA unaona nimekukera jinyonge

Nina mashaka na elimu yako.....
 
Fahari ya Kijana ni Nguvu zake mwenyewe (Mithali 20:29A)

Nimehuzunika sana na yale niliyoyashuhudia Juzi weekend kupitia Kituo Cha TBC ambacho kilirusha tukio la watu waliojiita Vijana wa CCM wa Vyuo Vikuu. Nieleze mapema kuwa hata mimi niliwahi kunasa kwenye mtego huo na tukaishabikia sana CCM kwa kupitia tawi la Abijani( kamwe sijui hata ofisi zao zilipo)

Lakini, enzi zile information ilikua so limited, vijana wa sasa wana kila information kila dakika na kila mahali, wanajua yanayoendelea nchini, wanaujua ukweli wa serikali hii kuwa si sahihi hata kidogo yale yanayotokea. Inflation inaongezeka kila uchao, ubabe wa kitoto wenye kuangamiza kizazi chetu unaongezeka kila uchao.

Tunategemea kuwa Vijana ambao wana nguvu, ambao wanaujua ukweli wa familia zao zinavyoteswa na serikali, waliosoma kwa shida sana, walikosa hadi mkopo na baadhi yao wakapata eti mkopo wa asilimi tano (5%) tulidhani wangesimama na kukataa uonevu huu kwa vitendo lakini matokeo yao vijana hawa wamekua mstari wa mbele kushabikia mambo haya.

Chagueni lililojema Mkaishi

Nawakumbusha Vijana mna safari ndefu, msikubali kupoteza nafasi hii ya kuibadilisha nchi yenu kwa faida ya watoto wenu na watoto wa watoto wenu.

Pole sana, punguza jazba, umekuja kwa hisia sana bila hoja ya msingi,tufikie mahali tuheshimu maamuzi ya watu mtu, ni uamuzi wa mtu kujiunga na chama chochote, wanasiasa wanapaswa kuuza sera za vyama vyao ili watu wajiunge, sasa ni jukumu la mwananchi kuamua aende wapi ,sasa ukija apa ukaponda vijana walioko chama fulani ili wajiunge uko ulipo bila hoja inayoeleweka utakua na matatizo makubwa
 
Weka mkuu naona unatishia Nyau

Hahahahaaaaa sitishi Nyau Mpwa ila wote tutaonekana vichaa na tutakua tumetoka nje ya mada. Tumalize hii kwanza tufungue nyingine kwenye jukwaa la picha. Unaonaje? Haya jibu hoja yangu
 
Viongozi wa UKAWA ni wazee, hawana mvuto kwa vijana
 
On a serious note na simple common sense.....kwa kijana yeyote anayeshabikia CCM ni lazima atakuwa na akili finyu tu, si bure.
 
Kijana ukiishabikia ccm lazima uwe na magumashimagumashi! Yaani haujielewielewi, haujiaminiamini.
 
Akili ya ccm cjui unaweza fananisha na nn!
 
Kijana fanya mambo yako mwisho wa siku mchague kiongoz mwenye sera za ukwel na mashiko. Ushabiki ni upotezaj muda na chama kitakupeleka wap ila ukipewa mkwanja pokea mwisho wa siku kura ni sir yako
 
mkuu vijana walioko ccm ndo kama akina Sitti Mtemvu (mshindi wa tuzo ya bibi bomba) na akina le mutuz (le mbululaz) tangu mwaka 1969 yupo UVCCM nafkiri miaka yake inahesabiwa kwa kurudi nyuma
 
ukimwona kijana anashabikia ccm ujue ana maslahi ndani ya chama
 
Mara nyingine huwa najiuliza vijana waliopo CCM wana tofauti kubwa sana na wale waliopo CHADEMA.

Vijana wengi waliopo CCM ni wale wenye uwezo wa kifedha au wametoka katika familia za wazazi wenye uwezo.

Wakati waliopo chadema ni vijana wa kawaida sana wanaotoka katika familia za chini na za kawaida mno.

Unaweza kukuta kijana anang'ang'ana kuitetea CCM mpaka meno yanamtoka jasho ukifuatilia historia ya kijana utakuta ndugu yake ni mkuu wa wilaya au waziri au mkuu wa mkoa au ni kiongozi ktk chama hivyo ni sehemu ya walewale wanaolalamikiwa kujilimbikizia mali.

Unategemea mtoto wa sita , membe kinana aiponde ccm haiwezekani.

Ukiwauliza vijana wengi waliopo chadema kwa nini wapo chadema watakuambia sababu kuu ni kwamba mwanzoni waliamini CCM hawaibi rasilimali za umma na sasa wameamini kwamba CCM wanawaibia mali zao hivyo ni afadhali sasa wawape chadema na wao wale kwani CCM wamekula miaka 50. Wanadai japokuwa hawatafaidika na chadema kuwepo madarakani si mbaya kwani hata uwepo wa ccm madarakani hawafaidiki pia.

Kwa hiyo ule msemo anaopenda kuutumia mbunge wa Arusha mjini kwamba mwana ccm huwezi kuwa wewe , huwezi kujiita wewe mwanaccm halafu unatembea bila ndala, huwezi kuwa sehem halafu unatembea kwa miguu, na mwisho huwa anamalizia kwa kusema ccm ina wenyewe , wanatembelea mashangingi na sio wewe unaeganga njaa uraiani.
 
ukimwona kijana anashabikia ccm ujue ana maslahi ndani ya chama

mkuu vijana walioko ccm ndo kama akina Sitti Mtemvu (mshindi wa tuzo ya bibi bomba) na akina le mutuz (le mbululaz) tangu mwaka 1969 yupo UVCCM nafkiri miaka yake inahesabiwa kwa kurudi nyuma

Kijana ukiishabikia ccm lazima uwe na magumashimagumashi! Yaani haujielewielewi, haujiaminiamini.

Akili ya ccm cjui unaweza fananisha na nn!

On a serious note na simple common sense.....kwa kijana yeyote anayeshabikia CCM ni lazima atakuwa na akili finyu tu, si bure.

Hahahahahaaaaa Safi sana natamani Simiyu Yetu na wale wengine wasome hizi comments zenye mashiko
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom