African Believer
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 436
- 425
Ndugu wanajukwaa, kama kichwa cha habari kinavyojieleza mimi kama mdau wa elimu ya Tanzania ningependa kupata ushauri kutoka kwenu kuhusiana na adhabu wanazopewa wanafunzi wanaokutikana na makosa mbalimbali mashuleni.
Hoja yangu imetokana na madhila ambayo yamewapata baadhi ya wanafunzi ambao kwa nyakati tofauti wameangukia kwenye vipigo vikali kutoka kwa wale waliopewa dhamana ya kuwasimamia na kuwafunza (walimu) jambo lililopelekea baadhi yao kupata maumivu makali na hata kuaga dunia.
Kwa sababu ya matokeo ya adhabu za walimu kwa wanafunzi wao, wadau mbalimbali wamekua wakishauri kuwa adhabu ya viboko mashuleni iondolewe. Jambo ambalo kwa mzazi yoyote aliyeona baadhi ya vipande vya video za walimu wakitoa adhabu kali kwa wanafunzi wao watakubaliana na hilo moja kwa moja.
Swali la kujiuliza hapa, je ni kwanini shuleni kuna adhabu? Jibu la moja kwa moja hapa ni kuwa adhabu hutolewa tu pale ambapo mwanafunzi ameenda kinyume na utaratibu ambapo kwa mujibu wa sheria inampasa aadhibiwe.
Kama ni hivyo basi mtoto huadhibiwa kwa sababu amekiuka utaratibu, na adhabu kuu na kongwe ni kuchapwa viboko au kupewa zoezi gumu, na jamii ya sasa haikubaliani na yote hayo. Ni nini basi kifanyike ili kuboresha nidhamu ya wanafunzia watukutu na wasiofuata utaratibu uliowekwa?
Kwa kuwa utukutu na kutokufuata utaratibu vimekuwepo enzi na enzi, na zama zote, hayo yalitafutiwa ufumbuzi wa namna mbalimbali. Ningeomba wanajukwaa kwa ujumla wetu tupate kulijadili hili na kupendekeza njia mpya za kukabiliana na watukutu pasipo kugusa miili yao kwa viboko, makofi, push up ama mateke.
Karibuni wana jukwaa tujadiliane.