GODZILLA
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 5,902
- 10,503
Sijui ni mpaka lini tu hizi adhabu za kinyama zitafutwa mashuleni?
Maana ni kama vile hakuna anayeona madhara yake japo kila siku tunashuhudia watoto na wanafunzi wakiuliwa na walimu mashuleni.
Tulishakuwa na sheria inayotoa mwongozo wa utoaji wa viboko lakini haizingatiwi kabisa, kitu ambacho kinaleta hatari kubwa juu ya usalama wa watoto mashuleni.
Hatuwezi kuwa kila mara tunasubiri mwanafunzi auwawe ndipo tuanze kutoa matamko wakati uwezo wa kudhibiti huu unyama dhidi ya watoto tunao.
Ndani ya miezi saba tu tangu mwaka 2023 uanze imeripotiwa kutokea vifo zaidi ya saba vya watoto mashuleni kutokana na vipigo vya walimu.
Hatuwezi kuendelea na huu uhuni. Ni wazi sheria inayotoa mwongozo wa viboko imeshindwa kufanya kazi, hivyo ifutwe moja kwa moja kwa mustakabali wa watoto wetu.
Natoa rai kwa serikali ione ulazima wa haraka wa kufuta viboko na kumaliza mauaji ya watoto mashuleni.
Naambatanisha uthibitisho.