Ni adhabu ipi iwe mbadala wa viboko kwa wanafunzi watukutu mashuleni?

African Believer

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
436
421
Ndugu wanajukwaa, kama kichwa cha habari kinavyojieleza mimi kama mdau wa elimu ya Tanzania ningependa kupata ushauri kutoka kwenu kuhusiana na adhabu wanazopewa wanafunzi wanaokutikana na makosa mbalimbali mashuleni.

Hoja yangu imetokana na madhila ambayo yamewapata baadhi ya wanafunzi ambao kwa nyakati tofauti wameangukia kwenye vipigo vikali kutoka kwa wale waliopewa dhamana ya kuwasimamia na kuwafunza (walimu) jambo lililopelekea baadhi yao kupata maumivu makali na hata kuaga dunia.

Kwa sababu ya matokeo ya adhabu za walimu kwa wanafunzi wao, wadau mbalimbali wamekua wakishauri kuwa adhabu ya viboko mashuleni iondolewe. Jambo ambalo kwa mzazi yoyote aliyeona baadhi ya vipande vya video za walimu wakitoa adhabu kali kwa wanafunzi wao watakubaliana na hilo moja kwa moja.

Swali la kujiuliza hapa, je ni kwanini shuleni kuna adhabu? Jibu la moja kwa moja hapa ni kuwa adhabu hutolewa tu pale ambapo mwanafunzi ameenda kinyume na utaratibu ambapo kwa mujibu wa sheria inampasa aadhibiwe.

Kama ni hivyo basi mtoto huadhibiwa kwa sababu amekiuka utaratibu, na adhabu kuu na kongwe ni kuchapwa viboko au kupewa zoezi gumu, na jamii ya sasa haikubaliani na yote hayo. Ni nini basi kifanyike ili kuboresha nidhamu ya wanafunzia watukutu na wasiofuata utaratibu uliowekwa?

Kwa kuwa utukutu na kutokufuata utaratibu vimekuwepo enzi na enzi, na zama zote, hayo yalitafutiwa ufumbuzi wa namna mbalimbali. Ningeomba wanajukwaa kwa ujumla wetu tupate kulijadili hili na kupendekeza njia mpya za kukabiliana na watukutu pasipo kugusa miili yao kwa viboko, makofi, push up ama mateke.

Karibuni wana jukwaa tujadiliane.
 
kuchuma mchicha asubuhi hadi jioni au kupanda maboga
ni kwa kijijini tu mjini wasipewe hela ya nauli
 
Shule za dini zinafaulisha na watoto wanakuwa na maadili mema sababu,hawacheki na kima,mtoto akijifanya kaenda kukua hapo shule anarudishwa nyumbani akamfate mzazi wake,aje afokewe badala yake.akirudia tena kosa nao wanamkataa mtoto wako,tena kwa unoko na ada unarudishiwa.

Jaman wazazi/walezi wangu walikuwa wanoko,sijawahi kuchekewa mimi kwenye maslahi mapana ya ustawi wa tabia yangu.nashukulu leo hii mimi si kijana wa ajabu ajabu,ili kuunga mkono juhudi za wazazi wangu namimi nitakuwa mnoko kwa kizazi changu chote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugmatokeukwaa, kama kichwa cha habari kinavyojieleza mimi kama mdau wa elimu ya Tanzania ningependa kupata ushauri kutoka kwenu kuhusiana na adhabu wanazopewa wanafunzi wanaokutikana na makosa mbalimbali mashuleni.

Hoja yangu imetokana na madhila ambayo yamewapata baadhi ya wanafunzi ambao kwa nyakati tofauti wameangukia kwenye vipigo vikali kutoka kwa wale waliopewa dhamana ya kuwasimamia na kuwafunza (walimu) jambo lililopelekea baadhi yao kupata maumivu makali na hata kuaga dunia.

Kwa sababu ya matokeo ya adhabu za walimu kwa wanafunzi wao, wadau mbalimbali wamekua wakishauri kuwa adhabu ya viboko mashuleni iondolewe. Jambo ambalo kwa mzazi yoyote aliyeona baadhi ya vipande vya video za walimu wakitoa adhabu kali kwa wanafunzi wao watakubaliana na hilo moja kwa moja.

Swali la kujiuliza hapa, je ni kwanini shuleni kuna adhabu? Jibu la moja kwa moja hapa ni kuwa adhabu hutolewa tu pale ambapo mwanafunzi ameenda kinyume na utaratibu ambapo kwa mujibu wa sheria inampasa aadhibiwe.

Kama ni hivyo basi mtoto huadhibiwa kwa sababu amekiuka utaratibu, na adhabu kuu na kongwe ni kuchapwa viboko au kupewa zoezi gumu, na jamii ya sasa haikubaliani na yote hayo. Ni nini basi kifanyike ili kuboresha nidhamu ya wanafunzia watukutu na wasiofuata utaratibu uliowekwa?

Kwa kuwa utukutu na kutokufuata utaratibu vimekuwepo enzi na enzi, na zama zote, hayo yalitafutiwa ufumbuzi wa namna mbalimbali. Ningeomba wanajukwaa kwa ujumla wetu tupate kulijadili hili na kupendekeza njia mpya za kukabiliana na watukutu pasipo kugusa miili yao kwa viboko, makofi, push up ama mateke.

Karibuni wana jukwaa tujadiliane.

Minadhan kwanza tubadirike cc wanajamii wenyewe tujifunze kudhibit jazba zetu au wengine waache kujifanya wanamaumivu au uchugu sana pind jambo liclotarajiwa linapovjitokez
Tumewah kuona walimu wakiadhibiwa na kudharirishwa kisa watoto wamepewa dawa kwamzazi km huyo ht mtoto wake akimvua nguo mwenzake cmchap ng'oo lkni kiukweli mtoto wa bongo ataekuwa mtiifu bila yakutumia MBAARTA ( VBC) lbda VITUKUU VYAKIZAZ HIK

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viboko ni adhabu za kitumwa sanaa na unyanyasaji.. Sikuhizi ata ng 'ombe kama unamchapa viboko hovyo hovyo watakuja watu wa haki za wanyama sembuse sisi wanadamu...

Viboko sivipendi coz sijalelewa mazingira ya viboko bali maonyo na sahivi ni kijana mwema na nisiye na tatizo lolote...

Napendekeza watoe adhabu za kujenga na sio kubomoa mfano.. Kupiga deki, kufagia ama kuokota taka taka, kichimba mashimo.... Na hapo kijana akikataa arudishwe kwa wazazi wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na hayo madhari ( vifo) vinavyotokea kutonana na viboka ila kiukwel Shule hasa za serikali yanii kata kata kuna nidhamu mbovu mno miongoni mwa wanafunzi na pindi hata stahiki zinapochukuliwa na utawala dhidi ya wanafunzi watukutu huwezi kuamini wanasiasa hasa madiwani has a WA ccm huwafuata walimu Kwa ukali na kulazimisha kutengua adhabu, Nina ushahidi WA hili!!!
Suluhisho!!! Ili mwalimu usiingie kwenye mgogoro na jamii na kwa kua gvt haina time na nyie!!! Mfano humpewi posho yoyote kama kada nyingine amueni kuweka fimbo chini kama mwanafunzi haingilii interest zako achana nae mradi unalipwa na tarehe ikifika benk kunasomeka unapata wapi muda wa kuhangaika na mtoto wa mtu!!!! Pambania wanao tena peleka private nzuri lipa jata Mil 3 achana hawa akina kanumba watakutia matatizoni
 
Sasa siasa Ukiacha utapungukiwa hoja ama. Eti CCM.
 
Write your reply...

kuwe na utaratibu maalum wa kutoa adhabu sio kila mwalimu kujiamulia tu! aina ya adhabu lwa mfano

mwanafunzi akifanya kosa mara ya kwanza aonywe kwa mdomo then akirudia apewe adhabu hta kukata mti au kufanya usafi akiendelea na ukaidi arudishwe nyumbani, fimbo iwe option ya mwisho kbsa tena sizidi sita
 
Viboko ni adhabu za kitumwa sanaa na unyanyasaji.. Sikuhizi ata ng 'ombe kama unamchapa viboko hovyo hovyo watakuja watu wa haki za wanyama sembuse sisi wanadamu...

Viboko sivipendi coz sijalelewa mazingira ya viboko bali maonyo na sahivi ni kijana mwema na nisiye na tatizo lolote...

Napendekeza watoe adhabu za kujenga na sio kubomoa mfano.. Kupiga deki, kufagia ama kuokota taka taka, kichimba mashimo.... Na hapo kijana akikataa arudishwe kwa wazazi wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu adhabu ya viboko hata mimi huwa nasemaga ni utumwa tu!
Na mwalimu anapokupiga anakuwa anapandisha munkari saikolojikali hasira zake zote za maisha zinahamia kwa mwanafunzi!wakati anapiga fikra zake zinahama kabisa....ndomana utakuta mwanafunzi anapigwa kupitiliza....

Narudia tena kusema,ndomana sisi wengine tulikuwa na historia ya kuwadunda walimu kwa mambo kama hayo yanayofanyika!

Ova

Hiyo nayo ni historia nzuri ya kusimulia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa siasa Ukiacha utapungukiwa hoja ama. Eti CCM.
Pole kama nimekugusa ila chama chenu kina madiwani WA hovyo kuliko unavyofikifia wanafunzi watovu WA nidhamu kisa tu,wazazi ni wapigakura hili nimeli experience nikiwa mwalimu miaka kadhaa iliyopita
 
Minadhan kwanza tubadirike cc wanajamii wenyewe tujifunze kudhibit jazba zetu au wengine waache kujifanya wanamaumivu au uchugu sana pind jambo liclotarajiwa linapovjitokez
Tumewah kuona walimu wakiadhibiwa na kudharirishwa kisa watoto wamepewa dawa kwamzazi km huyo ht mtoto wake akimvua nguo mwenzake cmchap ng'oo lkni kiukweli mtoto wa bongo ataekuwa mtiifu bila yakutumia MBAARTA ( VBC) lbda VITUKUU VYAKIZAZ HIK

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kweli mabadiliko ya jamii nzima ndiyo yataleta ahueni kwa sintofahamu ya ni adhabu gani zitolewe kwa watoto wasiofuata taratibu zilizowekwa.
 
Pamoja na hayo madhari ( vifo) vinavyotokea kutonana na viboka ila kiukwel Shule hasa za serikali yanii kata kata kuna nidhamu mbovu mno miongoni mwa wanafunzi na pindi hata stahiki zinapochukuliwa na utawala dhidi ya wanafunzi watukutu huwezi kuamini wanasiasa hasa madiwani has a WA ccm huwafuata walimu Kwa ukali na kulazimisha kutengua adhabu, Nina ushahidi WA hili!!!
Suluhisho!!! Ili mwalimu usiingie kwenye mgogoro na jamii na kwa kua gvt haina time na nyie!!! Mfano humpewi posho yoyote kama kada nyingine amueni kuweka fimbo chini kama mwanafunzi haingilii interest zako achana nae mradi unalipwa na tarehe ikifika benk kunasomeka unapata wapi muda wa kuhangaika na mtoto wa mtu!!!! Pambania wanao tena peleka private nzuri lipa jata Mil 3 achana hawa akina kanumba watakutia matatizoni
Kwa hilo la nidhamu mbovu hata mimi nimelishuhudia tena kwa kiwango kukunwa.

Swali la kujiuliza, ni kwa nini hili linakua siku hadi siku, na ni hatua gani zichukuliwe ili kukabiliana nalo?

Tukisema tuliache hivyo lilivyo tutajenga jamii mbovu isiyo na maadili na matokeo yake ni kurudisha nyuma maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Mimi nafikiri tunahitaji kuumiza vichwa ili kupata mwaronaini wa hili. Pia nadhani ushirikiano wa kina kati ya wadau yaani; serikali,wazazi, walezi pamoja na walimu unahitajika katika kulitatua hili.
 
Sisi wazazi wa kizazi hiki tumeshindwa kabisa kulea watoto.
Zama hizi za utandawazi watoto wameharibika kabisa kitabia kwa kukosa malezi bora.
Huu ndio mzizi wa matatizo yote haya yanayotokea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waangalie mifano kwenye shule ambazo hazitoi adhabu ya viboko huwa wanafanyaje... tuanzie hapo kwanza!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom