Ni adhabu ipi iwe mbadala wa viboko kwa wanafunzi watukutu mashuleni?

Nakubaliana kabisa na wewe kuhusu utaratibu wa baadhi ya shule za seminari, ambazo hazitoi adhabu ya viboko lakini wakawa na adhabu mbadala lengo likiwa ni lile lile la kumfanya mtoto akue katika maadili mema.

Kwangu mimi pia nimebahatika kusoma seminari lakini pale kwetu viboko vilikuwepo na recta wetu hakuwa na mchezo katika hilo hata kidogo.

Kitu kingine ni lazima uangalie aina ya watoto wanaochaguliwa kusomea kwenye shule za seminari na wale wanaosoma katika shule za kawaida za serikali. Kumbuka lengo kubwa la seminari hasa za Kikatoliki ni kuwaandaa mapadri hivyo humchagua mwanafunzi kwa kufuata vigezo vingi sana, kama vile; historia ya maadili ya familia anakotoka, ushiriki wa wazazi katika ibada, utii wa mtoto katika familia na jamii kwa ujumla, ushiriki wake katika mashirika ya kidini kama vile virafra, mt. Aloice etc. Sasa utaweza kuona utofauti kati ya seminari na shule nyingine za serikali.

Hapo vile vile umesema seminari mnaweza mkaanza 60 mkamaliza 30 sasa wewe unafikiri hao 30 wanaofukuzwa huenda wapi. Hao huenda kuendelea na elimu kwenye shule za serikali/za kawaida. Kumbuka jamii ina jukumu la kuhakikisha kila mtoto anapata elimu inayofaa bila kujali tofauti za kipato, kirangi, kidini, kikabila na kiutimilifu. Suluhisho hapa sio kumfukuza mwanafunzi bali ni kutafuta njia ya kuboresha maadili yake na kumfanya aendelee na elimu ambayo ni haki yake ya msingi.

Tulete mapendekezo ya namna tutakavyotatua tatatizo la ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya wanafunzi pasipo kutajataja seminari ambazo si mfano mzuri wa kulea watoto mchanganyiko.
Bado haikuwahi kusaidia sababu kilichokuwa kinafanyika siyo kuwanyoosha Bali kuwachuja ili kupata wale best waliondani na balance nzur ya nidhamu na academic,vipi wale uliowafukuza ndo umewasaidia au umwrudisha tatizo kwa jamii??umeanza na watoto 60 halafu umemaliza na 30 best unasema umesaidia??tunataka mfumo utakao wasaidia hawa 30 uliowashindwa na mpaka sasa bado sijaona mbadala wa viboko kwa ngozi nyeusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sahihi kabisa!
 
Nashangaa watu wanaongelea maadili, mara nidhamu, sijui malezi.

Ipo hivi, huwezi kukwepa maendeleo ya sayansi na teknolojia. Badala ya kuona watoto wamekosa maadili kuwa na simu shuleni. Tuifanye hiyo kuwa fursa. Tuwafundishe namna ya kutumia simu zao kuwaongezea maarifa.
Kwani naamini lengo kubwa la mtoto kuletwa shuleni ni kupata maarifa ambayo yatakua msaada wake huko mbele kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Alafu suala la adhabu endepo mtoto ataenda kinyume na sheria za shule, ni kuwaita wazazi wake na kuongea nao. Ikishindikana baada ya wazazi kuitwa mara mbili, basi adhabu ya mwisho ni kumfukuza mtoto shule. Suala la nidhamu ni suala la wazazi. Maana mazingira tunayoishi, ndiyo yanayofanya nidhamu zetu.

Adhabu ya viboko ni utumwa. Tena utumwa ambao mimi naupinga kwa 100%
Naomba nikukatalie kuhusu wanafunzi kumiliki simu... Hakuna mwanafunzi anayeweza kuwa na nidhamu katika umiliki wa simu. Tusidanganyane. Watu wazima tu wanashindwa kuji-control sembuse watoto!?
 
Naomba nikukatalie kuhusu wanafunzi kumiliki simu... Hakuna mwanafunzi anayeweza kuwa na nidhamu katika umiliki wa simu. Tusidanganyane. Watu wazima tu wanashindwa kuji-control sembuse watoto!?
Hilo ni kweli kabisa. Utaweza kuona hata kwenye mashirika mbalimbali ya kiserikali na kibinafsi watumishi hawaruhusiwi kuwa na simu wawapo maeneo ya kazi katika muda wa kazi.

Kama ulivyosema ndugu yangu jambo hilo halitoleta tija hata kidogo.
 
Back
Top Bottom