Ni 5% tu ya Watanzania au pungufu ndio walikuwa wanajua kuwa leo ni siku ya Uhuru!

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,141
Hello,

Uzi huu haujabeba chuki au nia mbaya. Nimeweka huu uzi Ili ikiwezekana serikali irekebishe baadhi ya mambo. Watanzania wengi hawajui mambo ya kitaifa sasa.

Mimi katika peruziperuzi mchana huu ndio najua kuwa leo ni Independence day. Sikukuu kubwa ya kitaifa kuliko sikukuu zote.

Nimefanya kautafiti kafupi kuwahoji watu kadhaa inaonyesha Watanzania hawajui nini kinaendelea leo. Wengi wanashangaa habari za sikukuu kuzikuta kwenye TV na mitandao ya simu leo.

Kwakuwa wengi walikuwa wakipata habari hizi kutoka kwa watoto wao ambao walikuwa hawaendi shule kama sikukuu imeangukia siku ya shule unfortunately shule zimefungwa na leo ni Jumamosi hata Wadanyakazi hatujui nini kinaendelea leo.

Miaka 20 mbele kuna uwezekano mpaka viongozi watasahau kufanya maandalizi ya sikukuu hii ya uhuru. Sad!
 
Watu wengi hawako huru kiuchumi kwa hiyo hawaoni cha kuwafurahisha mpaka washerehekee sikukuu ya Uhuru! Kwao wanaona kama ni uhuru wa bendera!
Labda watu wa Dar watuwakilishe uwanja wa Uhuru kushuhudia Askari wetu wakikanyaga ardhi na wale wajamaa wakivunja matofari.
 
Hello,

Uzi huu haujabeba chuki au nia mbaya. Nimeweka huu uzi Ili ikiwezekana serikali irekebishe baadhi ya mambo. Watanzania wengi hawajui mambo ya kitaifa sasa.

Mimi katika peruziperuzi mchana huu ndio najua kuwa leo ni Independence day. Sikukuu kubwa ya kitaifa kuliko sikukuu zote.

Nimefanya kautafiti kafupi kuwahoji watu kadhaa inaonyesha Watanzania hawajui nini kinaendelea leo. Wengi wanashangaa habari za sikukuu kuzikuta kwenye TV na mitandao ya simu leo.

Kwakuwa wengi walikuwa wakipata habari hizi kutoka kwa watoto wao ambao walikuwa hawaendi shule kama sikukuu imeangukia siku ya shule unfortunately shule zimefungwa na leo ni Jumamosi hata Wadanyakazi hatujui nini kinaendelea leo.

Miaka 20 mbele kuna uwezekano mpaka viongozi watasahau kufanya maandalizi ya sikukuu hii ya uhuru. Sad!
Sisi hatuna uhuru na wala hatujawaipata uhuru zaidi ya political propaganda.
 
Habari wanajukwaa!
Nilipokuwa Shule miaka ya 1990s huko nilikuwa nakutana na swali kuwa Tanzania imepata uhuru mwaka gani? basi nilikuwa nakurupuka na kusema mwaka 1961 kumbe sio Tanzani bali ni Tanganyika ila sasa ndo nimekuja kuona watu wajinga na wasio na ufahamu wanaosema kuwa kuna "Uhuru wa Tanzania Bara" yaani Tanganyika ndo imekuwa Tanzania Bara ni jambo la ajabu kweli.
Kuna mtangazaji mmoja wa kutoka kituo cha redio nilibishana naye sana na alidai kuwa jina Tanganyika lilikufa na kuna Tanzania Bara tu, hivyo kuna "Uhuru wa Tanzania Bara" na mimi nikampa swali je tukisema kuna "Mapinduzi ya Tanzania Visiwani itakuwa ni sahihi? akasema kuwa "Mapinduzi ya Zanzibar" na sio "Mapinduzi ya Tanzania Visiwani".
Ila kiukweli historia inapotea taratibu, Mungu tusaidie!
 
Tatizo viongozi wetu wamekabwa na jinamizi la muungano usiojieleza.
Nasi tunapita humo humo
 
Back
Top Bottom