SoC03 Naipenda siku ya uhuru wa taifa langu

Stories of Change - 2023 Competition

Mabula marko

Member
Jul 18, 2022
36
36
Habari ndugu msomaji karibu katika makala hii

Hii ni hadithi iliyokuwa nzuri na ya kusisimua ambayo mzee mwangosi alitushrikisha siku moja tukiwa kundi la vijana watano katika kijiwe cha kahawa ambaye alikuwa mzee mwenye umri wa miaka 89, mzee mwangosi alikuwa akizingumzia namna alivyoshiriki na kuwajibika kama kijana wa wakati huo katika harakati za kulikomboa na kulipatia uhuru taifa letu na pia aliendelea kuzungumzia pia namna wao kama vijana wa wakati huo walijitoa kuhakikisha taifa letu hili tunaloliona leo hii linasimama.

Mzee mwangosi pia hakuishia hapo kwa kuwa yeye alikuwa amekula chumvi nyingi aliweza pia kutoa tathimini ya ufanano wa vijana wa kizazi chao kipindi cha mkoloni, baada ya uhuru na vijana wa leo kisha baada ya hapo alicheka kidogo na kusema wajukuu wangu “Naipenda sana siku ya uhuru wa nchi yangu” kwani kila mara hunikumbusha vijana wa enzi zetu walivyojitoa na kuwajibika kulipigania taifa letu la na Africa yetu hii kuhakikisha inasimama hivi ilivyo leo.

Katika simulizi yake mzee mwangosi alizungumza akitolea pia mifano ya vijana wenzake wa enzi hizo walivojitoa na kuwajibika katika kulipigania taifa kama mwalimu nyerere, kasella bantu, mwapachu na john okello na wenzake(Zanzibar) na wengine ambao walitoa muda wao kuwa walinzi wa wapigania uhuru hao, aliendelea kusema vijana hawa walitumia usomi wao kuwa chachu ya vijana wengine kuwaamsha fikra zao ili kulikomboa taifa na kulifanya taifa liweze kujitegemea kujiendesha na hapo ndipo nae alifikiwa na kuongeza nguvu kwa kuwa yeye alikuwa pia amebahatika kuwa moja ya vijana wenye elimu japo ingawa ilikuwa ya darasa la saba la mkoloni.

Mzee mwangosi alizungumza pia akisimulia namna vijana hawa wachache ambao walijitoa na kuwajibika kila mtu katika nafasi yake ,mzee alisema vijana hawa walikuwa wameweka uzalendo mbele hivo walilitumikia taifa kwa moyo na kwa manufaa mapana ya taifa ,waliacha kazi zao za malipo mengi na kwenda kuwatumikia watu katika ujira mdogo lengo ni kutumia elimu na maono yao chanya kwa manufaa ya watu wengi, wakati akizingumza hayo akili yangu ikanikumbusha katika maonyesho ya siku ya sokoine pale chuo kikuu cha SUA mwezi tano 2023 miongoni mwa wageni waalikwa alikuwa Paul Kimiti mbunge na waziri mstaafu alipopewa nafasi ya kuzungumzia vijana wa enzi hizo na wasifu wa sokoine alianza kujitolea mfano akisema yeye alianza kazi kama bwana shamba wakati wa mkoloni baadae alipewa nafasi na taifa baada ya uhuru kwenda kusoma uholanzi.

Mheshimiwa kimiti alisema alipofika kule alianzisha bendi ya mziki na alikuwa akitumbuiza kama sehemu ya kupata kipato cha kuendesha maisha yake akiwa chuoni alivuna pesa nyingi kisha baada ya hapo alitoa pesa dollar elfu ishirini($20000) siku ambayo mwalimu nyerere alifika nchini uholanzi kwa ziara, miaka ya sitini kwa ajiri ya kuwezesha vijana wengine wa kitanzania waweze kupewa ufadhiri na serikali wa kwenda kusoma nje kama yeye, wakati Mh. Kimiti anamzugumzia sokoine alisema sokoine aliweza kujipunguzia hadi majukumu ya familia yake ili kutimiza majukumu ,aliweza pia kuruhusu akatwe mshahara ambao ulikuwa kama elfu 2000Tsh hivi za kitanzania kuchangia mfuko wa kuwezesha vijana kushiriki katika kilimo na kuwafanya wasikae na kushinda vijiweni hakika vijana hawa walikuwa wazalendo na wenye kuwajibika kwa masilahi ya watu wengi, baada ya kuyakumbuka hayo hadithi hii ya mzee mwangosi ilinigusa sana kama kijana wa wakati huu nikavutiwa Zaidi na nikatamani kuendelea kumsikiliza kisha akasema tena wajukuu wangu “Naipenda sana siku ya uhuru wa nchi yangu” kwani kila mara imekuwa ikinikumbusha yale tuliyo itendea nchi yetu kwa uzalendo na katika uwajibikaji wa hali ya juu na amekuwa akitamani kuona vijana wa leo wakiwajibika ipasavyo katika kila Nyanja.

Katika simulizi yake mzee mwangosi alisema amekuwa akichukizwa sana na kizazi chetu ambacho vijana wengi licha yakuwa dunia ya leo ina fursa nyingi ambazo ni halali ki sheria na ki mila na desturi zetu, serikali yetu pia inafanya kila namna kuwawezesha vijana hawa waweze kujihushughulisha na kuwajibika katika kila sekta kilimo, biashara, na zinginezo kwa kila namna serikali imeweka mifuko mingi ya fedha za kuwawezesha vijana kupata mikopo nafuu vijana wapate mitaji, serikali imetunga sheria ya vijana kupewa ardhi walime ,pia imeweka elimu bure , mzee mwangosi anasema serikali ikajitahidi kuona kuwa vijana hawa ni kizazi cha kidijitali turuhusu mitandao ya kijamii , tuweke pia sheria zinazoruhusu vijana kujikita katika uwajibikaji na bunifu chanya kwa taifa na watu wake kupitia udijitali lakini vijana wenyewe sasa wako bize kutafuta wafuasi katika mitandao ya kijamii na hawajui nama ya kuwageuza biashara hao wafuasi, vijana hawa wa leo hawataki shughuli lakini wanataka mafanikio ya haraka.

Mzee mwangosi anasema jaribuni kuzunguka katika miji na hata vijini utakuta vijana wamekaa tu vijiweni, wako na makundi ya wizi,wengine wanakimbia shule hawataki, akaenda mbali Zaidi na kusema anasikitishwa Zaidi kuona nguvu kazi ya taifa inapotea katika madawa ya kulevya , vijana wanajiingiza katika mapenzi ya jinsia moja na kuuza miili yao, utapeli mitandaoni na kila mahali , rushwa makazini lengo ni kujipatia fedha pasina kufanya kazi na akazidi kusema leo hii wasomi wetu hawana uwezo wa kung’amua mambo kisomi, vijana hawaajiriki kwa uwezo wao mdogo wa kutumia maarifa yao ya darasani kwasababu hawajitumi kuyatafuta maarifa ya ziada wawapo katika masomo yao mzee akatuuliza hivi mlishawahi kufikiri kama ujana wetu ungekuwa kama wenu tungekuwa na taifa la namna gani? Ama kweli sisi wenyewe tuliguswa na maono haya na hadithi hii yam zee huyu.

Ndugu msomaji baada ya kupokea simulizi hii ya mzee mwangosi sisi kama vijana tuliona tumsaidie mzee mwangosi kupaza sauti yake kwa vijana wenzetu ambao ndiyo idadi kubwa ya watanzania ikiwa ni Zaidi ya asilimia 35% ya watanzania ,tunawaomba vijana wenzetu tuwajibike ,tujitokeze,tujishughulishe, tupiganie taifa ,tuwe mabalozi wazuri wa taifa ,tuige kwa vijana hawa wazamani waliolipigani taifa hili tunaloliona leo walitoa maisha yao na shughuli zao kuhakikisha taifa linakuwa huru na wanalikomboa katika maradhi,ukosefu wa elimu na ukosefu wa chakula, vijana tuwe wabunifu mazingira ya kutuwezesha leo hii yapo makubwa sio kama zamani hata teknolojia ilikuwa duni ila leo hii kila kitu kipo na kinafikika tuamke vijana wenzangu.

Hitimisho
Naomba tuungane na mzee mwangosi tuipende siku ya uhuru wa nchi yetu ili itutie chachu ya kuona kuna vijana kama sisi walisimama kidete kuifanya Tanzania
 
Back
Top Bottom