NHIF kuzindua vifurushi vipya vya bima ya afya, sasa kila Mtanzania kuzingatiwa

Nilihitaji huduma ya miwani nikaambiwa NHIF hawalipii gharama za miwani zaidi ya Tsh 20,000 wakati gharama halisi ya miwani ya kusomea ni Tsh 250,000! Nakuambia huduma za NHIF ni za kitutusa sijapata kuona.
Wanasema miwani ni moja kati ya urembo.Kama unaweza pata miwani ya 30k.Lakini kwa kuwa unataka yenye madoido ziko frem za 500k.Unataka bima i cover hio pia?Think
 
Ubunifu mzuri sana, utasaidia watu wengi sana. Angalizo uwe wa gharama nafuu, wasiwe na lengo na kupata fedha kwaajili ya gawiwo serikalini.
Inawezekana lakini nadhani ni mapema mno kuwasifia hawa na Wizara husika. Kwa kutazama haraka haraka, utaona namna wazee (60+) walivyo pigwa na wakati huo huo wanaimba kila siku kuwa wazee wanastahili huruma za Taifa lakini leo vifurushi vya hawa wazee ndio ghali sana! Halafu, hizi huduma sijui za MRI, CT Scan na nyingine eti statolewa baada ya MWAKA MMOJA wa kujiunga!? Yaani ukijiunga 01/12/2019, utapata huduma hizo 01/12/2020 au nimesoma vibaya!? Hii maana yake nini ninyi watu wa NHIF na Wizara husika? Hebu lidadavueni hili, wacheni maneno na mbwembwe za majukwaani.
 
Dhamira ya Mh Rais Magufuli ni njema sana kwenye sekta ya afya ndio maana ameongeza bajeti kubwa kwa kutambua unyeti wake.

NHIF wana kifurushi kwa Mtoto afya ambacho watoto wote chini ya miaka 18 wanalipa 50,400 tu kwa mwaka mzima.

Ulikuwa ukishalipia unakaa ndani ya mwezi mmoja na kupatiwa kadi yako ya matibabu.

Sasa tunaona mabadiliko ambayo kimsingi ndio hoja yangu, iweje mtu alipie halafu anaambiwa asubiri miezi mitatu?

Yaani mtoto amezaliwa leo naenda kumkatia bima yake naambiwa subiri miezi mitatu. Hamuoni mtaleta shida kwa watoto hawa na huenda wengine wakapoteza maisha kisa wanasubiri kadi na huku mtoto ameumwa na wazazi hawana pesa.

Maswula kama haya sio lazima mpaka aje aingilie Mh Rais wakati Waziri Ummy yupo na baadhi ya watendaji wizarani na NHIF wapo.

Chonde chonde NHIF tunaomba mrudishe muda ule ule wa mwezi mmoja mtu awe amepata kadi ya matibabu na sio miezi mitatu kama mnavyofanya sasa

Alex Fredrick
 
NHIF wana huduma za kipumbavu kuliko bima yoyote hapa Ulimwenguni. Wakati watu wanaolazimishwa kujiunga NHIF wakitamani kujitoa, nitawashangaa sana wananchi watakaojiunga na huduma hizi za kijinga za NHIF.
Kifurushi cha chini Ni elfu arobaini hata kea wale walokuwa wanakatwa elfu 23 kwenye mi
Kama kodi tunalipa tunataka huduma ya afya iwe bure kama elimu siyo kuambiana vifurushi alafu mnaweka package za laki moja nini sasa hivi mkulima wa bamia uko anaweza kutoa hizi million ebu tuache kutaniana
Kwa wale watanyakazi kima cha chini kuchangia kwa mwezi itakuwa ni elfu 40 tofauti na zamani ambapo wengne walkuwa wanakatwa 23 elfu
 
Kifurushi cha chini Ni elfu arobaini hata kea wale walokuwa wanakatwa elfu 23 kwenye mi
Kwa wale watanyakazi kima cha chini kuchangia kwa mwezi itakuwa ni elfu 40 tofauti na zamani ambapo wengne walkuwa wanakatwa 23 elfu
Kumbe imekiwa hivyo maana yake mfanyakazi kwa mwaka atalipa 480 na serikali inamlipia 480

NHIF tatizo kubwa serikali ilikopa sana hela kutoka huko na hawana mpanfo wa kurudisha
 
Mkuu utaratibu huo bado upo kwa dar es salaam familia ya watu 6 inategemewa watalipa laki 1 na kwa mtu mmoja mmoja ni elfu 40 kwa mwaka kwa mikoani elfu 30 kwa mwaka mzima kwa huduma za kituo cha afya,hospitali za mikoa na wilaya
Kwa watumishi wa umma unabaki vilevile?
 
Kifurushi cha chini Ni elfu arobaini hata kea wale walokuwa wanakatwa elfu 23 kwenye mi
Kwa wale watanyakazi kima cha chini kuchangia kwa mwezi itakuwa ni elfu 40 tofauti na zamani ambapo wengne walkuwa wanakatwa 23 elfu
Wafanyakazi wakikubali watakuwa wehu
 
Ni kweli hawatibu hayo magonjwa sababu wanasema wengi wanaingia na magonjwa
 
Nawashangaa sana NHIF na wataalaam waliopo serikalini kwa huu mpango wao wa mabei tofauti tofauti, ni "highly complicated".

"Scheme" yoyote inayojikita kwenye vyanzo vya kutafutia pesa ikishakuwa "complicated" inakuwa ni biashara yenye kuhitaji "marketing" na "sales" ili kuiuza.

"Scheme" inayozingatia huduma haiwezi kufanywa kuwa na "complications" hivyo. Ilitakiwa uwe mpango wenye "flat rate" moja tu kwa huduma zote kwa umri wowote. Full stop.

Kwanini serikali ijiingize kwenye biashara kwa kutumia afya za wananchi wake? Imekosa ubunifu wa kutafuta mapato kwa vyanzo vingine?

Nawashauri serikali warudi kwa kichwa kilicholeta wazo hilo serikalini wakati wa Mkapa. Wakae nacho chini kiwape njia nzuri ya kufanya.

Huu mpango kiukweli siyo mzuri na haufai ingawa tutalazimika kuutumia lakini unaweka rehani afya zetu na kutuzidisha kuishi kwa hofu.

Hakika kwa mipango kama hii, Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.

Nnauhakika huu mpango ulipiga hesabu za kibiashara zaidi ya kihuduma kwa jamii.

Muoneni Rostam Aziz awasukie mpango mwema kabisa.
 
Wewe subiria kwenye bei za hivyo vifurushi, ndio utajua neno mnyonge hutumika kisiasa tu, hawana huruma naye!!
Siku zote tunaambiwa wazee wa miaka sitini na kuendelea watatibiwa bure. Nionavyo mimi hakuna kitu kama hicho na sasa watatakiwa ama kukata bima ya afya au kusubiri kifo taratibu. Sera ya Wazee ni hadithi ya kufikirika na hutumiwa kisiasa zaidi kuliko ukweli ulivyo.
 
Kifurushi cha chini Ni elfu arobaini hata kea wale walokuwa wanakatwa elfu 23 kwenye mi
Kwa wale watanyakazi kima cha chini kuchangia kwa mwezi itakuwa ni elfu 40 tofauti na zamani ambapo wengne walkuwa wanakatwa 23 elfu
Cheki hiyo
IMG-20191129-WA0014.jpeg
IMG-20191129-WA0013.jpeg
 
Back
Top Bottom