NHIF kuzindua vifurushi vipya vya bima ya afya, sasa kila Mtanzania kuzingatiwa

Mnaosema hivyo vifurushi ni bei rahisi labda kwa kulinganisha na bima zingine, watoto walikua ni elfu 50, hapo kwenye vifurushi ni karibu laki 2, tunaambiwa wazee wa zaidi ya miaka 60 ni bure lakini hapo wana vifurushi vyao, ni watu wachache sana wenye watoto wanne na umri wao ni chini ya 35, wengi wenye watoto wa4 wanaangukia kwenye fungu la pili 36-59 ambapo gharama zipo juu.
Cha muhimu serikali ingepunguza zaidi hizo gharama angalau kiwango cha juu kabisa kiwe milioni moja, na iongeze fungu kufidia gharama za kutibu wananchi wake, watu wakiwa wazima watafanya kazi na serikali itapata kodi zaidi.

Watoto chini ya miaka 18 bado wanazo package zao zile zile yaani 50,400 kwa mwaka. Mtoto anatibiwa HOSPITALI YOYOTE ile hahitaji barua ya rufaa kwenda Muhimbili....wewe ukiamka unajisikia umpeleke mwanao kutibiwa malaria au kung'oa jino muhimbili ama mwananyamala ama bugando au kcmc unaenda bila uliza/pata barua ya nhif.

Na watoto wanakitengo chao hapo nhif...ukichukua package ya family yaani mume, mke na watoto...unahudumiwa kwy nhif watu wazima...sio kule kwy "toto afya" laa kama ukajitenga wazazi kivyao na watoto kivyao basi watoto watapata account/membership zinazowapa power ya kutibiwa kokote kama nilivoeleza juu.

Naongea kwa experience kwa sbb ninao watoto hivyo nashauri bora watoto uwachukulie kivyao zile za 50.4K
 
Uko sahihi
 
Kama kodi tunalipa tunataka huduma ya afya iwe bure kama elimu siyo kuambiana vifurushi alafu mnaweka package za laki moja nini sasa hivi mkulima wa bamia uko anaweza kutoa hizi million ebu tuache kutaniana
 
Oyaa nauliza tena toto afya card imekufa au nadonipo wakuu mbona sijibiwi au ndio hadoli niende NHIF wakuu nifafanulieni...
 
Bi
Ubunifu mzuri sana, utasaidia watu wengi sana. Angalizo uwe wa gharama nafuu, wasiwe na lengo na kupata fedha kwaajili ya gawiwo serikalini.
Bima hii ya afya kwa viwango vyake ambavyo viko juu sana sidhani kama Serikali hii kweli inawajali sisi wanyonge. Mikakati mikubwa iko kununua na kuboresha miundombinu mbalimbali. Lakini kwa viwango hivi vya bima hii sasa si bima ya afya bali ni bima ya mauaji.

Elfu hamsini ambayo ni titi bima Mh Magufuli hapo tu hatuwezi je sisi wakubwa itakuwaje inafika hadi laki sita kwa mwaka. Hii ni nchi ya wanasiasa na matajiri wakituita sisi ni wanyonge. Nilitegemea hata wangesema familia ya watoto wanne baba na mama wangelipa angalau 25000 ingekuwa nafuu kiasi fulani.
 
Nadhani ni wazo zuri lkn kwa upande wa muda kama kadi itaanza kutumika mwezi 1 baada ya kulipia ...maana yake ni miezi 11 sio mwaka ...na pili toeni vijarida vya ngazi za dawa ili tufanye maamuzi..tusije jikuta tunalipia panadol na paracetamol tu.
 
Hawatatibu hayo magonjwa kama umechukua kadi ukiwa na hayo magonjwa.
Na magonjwa hayo utaanza tibiwa mwaka 1 baada ya kuwa mwanachama
Sahihi mkuu, mimi nilifika pale ofisi zao za tazara kwa lengo la kukata bima na nilivoomba ufafanuzi zaidi wakaniambia kuna magonjwa kadhaa hawagharamii mfano Saratani, Moyo na Figo
 
Sijaelewa wazee kwemye package ya miaka 19-35.

Mume + mke na watoto 3.

Hapo ni nani hatakiwa kuvuka miaka 35.

Ni woote ama??? Watoto tu.
 
Mkuu utaratibu huo bado upo kwa dar es salaam familia ya watu 6 inategemewa watalipa laki 1 na kwa mtu mmoja mmoja ni elfu 40 kwa mwaka kwa mikoani elfu 30 kwa mwaka mzima kwa huduma za kituo cha afya,hospitali za mikoa na wilaya
Naomba unisaidie jinsi ya kujiunga kwa hapo Dar mkuu nnashida sana
 
Ha! Sasa hayo sio ndio magonjwa yanayowaathiri watu wengi? Kwahiyo ulipe laki5 kutibiwa malaria tu? Si ulimbukeni huu?
Sahihi mkuu, mimi nilifika pale ofisi zao za tazara kwa lengo la kukata bima na nilivoomba ufafanuzi zaidi wakaniambia kuna magonjwa kadhaa hawagharamii mfano Saratani, Moyo na Figo
 
Back
Top Bottom